STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 20, 2014

Salum Madadi amrithi rasmi Sunday Kayuni

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7lMjEEmEOrbOo3NqhCxqIZxBddDdVIq5fPd1o1fFxk2KIKlr1Mf0Q6YP2Rh7BrSOhe0-Xqdu2qW3TYN15c57hT9sd1N14lefruxLXFqmI2tM9gMNpnpg4NA1nmisrq0h3GluJNpFSLJRM/s1600/Salum+Madadi.jpg
Salum Madadi

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemteua Salum Madadi kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi. Uteuzi huo umefanya na Kamati ya Utendaji katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi, Madadi alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Januari mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Ufundi aliyekuwepo kumaliza mkataba wake Desemba 31 mwaka jana.
Madadi mwenye leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ni kocha mwenye uzoezi wa zaidi ya miaka 30 ambapo alianza kufundisha mpira wa miguu mwaka 1980 katika klabu ya Maji SC ya Lindi.
Ana elimu ya sekondari aliyoipata katika shule ya Chidya na diploma ya ukocha wa mpira wa miguu aliyoipata nchini Ujerumani. Pia ni Mkufunzi wa makocha wa CAF, na alijiunga na TFF mwaka 2006 akiwa Ofisa Maendeleo.
Alikuwa Kocha wa Taifa Stars mwaka 2000. Mbali ya Maji SC, amewahi kufundisha timu za Nyota Nyekundu, Ushirika ya Moshi, Simba, Shangani ya Zanzibar, Malindi ya Zanzibar, Cardif ya Mtwara na Kariakoo ya Lindi.
Pia amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Wakati huo huo: CAF imewateua Watanzania Alfred Rwiza na Leslie Liunda kusimamia mechi zake za wikiendi hii na mwezi ujao.
Liunda ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) kati ya How Mine ya Zimbabwe na Bayelsa United ya Nigeria itakayochezwa Jumamosi (Machi 22 mwaka huu) jijini Bulawayo.
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Eritrea, na wanaongozwa na Maeruf Kherseed. Wasaidizi wake ni Angeson Ogbamariam, Berhe O’Michael na Luelseghed Ghebremichael.
Naye Rwiza atasimamia mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Lesotho na Swaziland itakayochezwa kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Maseru.
Mechi hiyo ya marudiano itachezwa na waamuzi Duncan Lengani, Innocent Kaundula, Hendrix Maseko na Jones Makhuwira, wote kutoka nchini Malawi.

Liunda, Lwiza waula CAF

Liunda
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua Watanzania Alfred Rwiza na Leslie Liunda kusimamia mechi zake za wikiendi hii na mwezi ujao.

Liunda ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) kati ya How Mine ya Zimbabwe na Bayelsa United ya Nigeria itakayochezwa Jumamosi (Machi 22 mwaka huu) jijini Bulawayo.

Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Eritrea, na wanaongozwa na Maeruf Kherseed. Wasaidizi wake ni Angeson Ogbamariam, Berhe O’Michael na Luelseghed Ghebremichael.

Naye Rwiza atasimamia mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Lesotho na Swaziland itakayochezwa kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Maseru.

Mechi hiyo ya marudiano itachezwa na waamuzi Duncan Lengani, Innocent Kaundula, Hendrix Maseko na Jones Makhuwira, wote kutoka nchini Malawi.

TFF yamlilia shabiki aliyekufa uwanja wa Taifa

Rais wa TFF, Jamal Malinzi
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mshabiki Deodatus Mwakyangula kilichotokea jana (Machi 19 mwaka huu) wakati ya mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Msiba huo ni mkubwa kwa familia ya Mwakyangula na kwetu, kwani umetokea wakati akiwa uwanjani kushuhudia mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Mwakyangula, na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

TFF yazilima Simba, Yanga faini ya Sh Mil 25

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXh18KznrT-bI44ZT6UDlvtGHm8OX01YCYjWAinLTkgudNbXhAnmcuplm3XGy_c3fIIzspHL-oGxQVibqfeiNkmqh2EBnvKnsodBCumWzI4Gnyp9EzIJy0b5hk0Z9zkeubFBYor3r48Rkj/s1600/11.jpg
KLABU za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh. Milioni 25 kutokana na uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika vurugu hizo.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
TFF imetoa onyo kwa washabiki wa mpira wa miguu kujiepusha na vurugu viwanjani ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya viwanja ikiwepo viti, na imeahidi kuchukua hatua kali zaidi kwa klabu na washabiki wake iwapo vitendo hivyo vitajitokeza tena.

Casillas achekelea kuibania Yanga, ila alilia Mtibwa kupepesuka

KIPA tegemeo wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharrif 'Casillas' amesema pamoja na kufurahia kuibania Yanga na kuwalazimisha suluhu wakiwa pungufu uwanjani, bado hajaridhika na mwenendo wa timu yake na kuwataka wachezaji wenzake kupigana ili angalau imalize kwenye Top 4.
Casillas aliyekuwa mwiba kwa washambuliaji wa Yanga kwenye mechi iliyochezwa wiki iliyopita katika uwanja wa Jamhuri, alisema anajisikia faraja kuweza kuwanyiuma mabao nyota wa Yanga wakiongozwa na Emmanuel Okwi, Kiiza Hamis na Didier Kavumbagu,.lakini furaha yake ni kuona Mtibwa ikimaliza pazuri.
Kipa huyo wa zmaani wa Villa Squad alisema nafasi waliopo timu yao hailingani na hadhi ya ukongwe wake na kuwaomba wachezaji wenzake wakomae katika mechi zilizosalia kufungia msimu ili wamalize nadani ya Top 4.
"Nimefurahia kumbania tena Okwi na wenzake kama nilivyofanya wakati akiwa Simba na tulipokutana na watetezi hao msimu uliopita, lakini hii haisaidii kama tutaendelea kuporomoka kenye msimamo," alisema.
Alisema ni lazima wachezaji wa Mtibwa wapigane kuiwezesha timu yao kuwa kwenye nafasi za juu hata kama wameshapoteza nafasi ya kuwa mabingwa.
Mtibwa waliowahi kunyakua taji la ubingwa wa soka nchini kwa misimu miwili mfululizo mwaka 1999-2000 na 2000-2001, msimu huu imekuwa urojo kiasi cha kuondolewa kwenye mbiuo za ubingwa zilizobakia kwa timu za Azam, Yanga na Mbeya City.

Acheni Ronaldo awe Mwanasoka Bora wa Dunia

MABAO mawili aliyofunga juzi wakati akiivusha Real Madrid klwenye robo fainali, yamemfanya Cristiano  Ronaldo kufikia rekodi ya gwiji Ferenc Puskas ya kuifungia magoli katika klabu hiyo akiwabakisha wakali wengine watatu .
Ronaldo alifunga mabao hayo wakati wakiiangamiza  Schalke 04 na kumfanya Mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia kufikisha jumla ya mabao 242 katika mechi 236 - idadi sawa ya mabao kama gwiji huyo wa Hungary.
Ronaldo (29) ameifikia rekodi ya mabao ya Puskas akiwa amecheza mechi 25 pungufu ya gwiji huyo huku pia akiwa ameichezea klabu hiyo kwa miaka mitatu pungufu (mitano) ukilinganisha na Puskas (minane).
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno sasa anafukuzia rekodi ya ufungaji bora wa zama zote wa klabu hiyo, akiwa amewabakisha Santillana (aliyefunga magoli 290), Alfredo di Stefano (307) na Raul (323).
Nyota huyo bado ana nafasi ya kuvunja rekodi ya mabao kutokana na kiwango alichonacho na pia umri ukiw aunamruhusu huku akiwa na bahati ya kutokumbwa na majeraha ya mara kwa mara kama baadhi ya wachezaji nyota wengine.

kun Aguero awindwa Barca, Martino ataja wengine saba

Kun Aguero
MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester City, Sergio 'kun' Aguero ni kati ya wachezaji wanaomezewa mate na kocha mkuu wa Barcelona, Tata Martino.

Kocha huyo amewasilisha majina ya wachezaji nane anaotaka kuwasaji katika majira ya joto kwa Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, Andoni Zubizarre.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, wakati mkongwe wa Lazio Miroslav Klose naye akiwamo
Winga wa Atletico Madrid, Arda Turan na wa Borussia Dortmund,  Ilkay Gundogan watakuwa ni viungo wawili kwa Martino, wakati Santiago Vergini (anayecheza kwa mkopo Sunderland), Filipe Luis (Atletico Madrid), Doria (Botafogo) na Neven Subotic (Borussia Dortmund) wakitarajiwa kuimarisha safu yake ya ulinzi.
Barceloina imepania kujiimarisha zaidi ili kuendeleza kutamba kwenye ligi ya nchini mwao na michuano ya Ulaya.

TASWA yateua 12 Kamati Tuzo za Wanamichezo Bora

Katibu Mkuu wa TASWA. Amir Mhando ;Mgosi'
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) iliyokutana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita imeteua majina ya watu 12 kwa ajili ya kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa kila mwaka na chama hicho huku ikizifanyia mabadiliko makubwa tuzo hizo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mwenyekiti TASWA, Egbert Mkoko, kamati hiyo ya tuzo ambayo itakuwa chini ya uenyekiti wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Rehure Nyaulawa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio 100.5 Times FM, ina wajumbe wengine 10 ambao si viongozi wa TASWA, lakini ni waandishi wazoefu wa habari za michezo.
"Jukumu la kamati hiyo pamoja na kuandaa mchakato wa upatikanaji wa Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2013 na kupanga tarehe ya kufanyika tuzo hiyo mwaka huu, lakini pia imepewa mamlaka ya kutazama mfumo wa tuzo ulivyo na ikiwezekana kuubadili kwa namna itakavyoona inafaa kwa maslahi ya chama na maendeleo ya michezo kwa ujumla," ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza: "Ni nia ya Kamati ya Utendaji ya TASWA ni kuona tuzo inakuwa bora na ambayo wadau wa michezo wataendelea kuiheshimu kwa kila hatua. Ndiyo maana TASWA ikaamua kuipa kamati hiyo mamlaka ya kuamua mambo ya msingi katika kuiboresha kwa mipango ya muda mfupi na mrefu."
Pamoja na mwenyekiti Nyaulawa, wengine walioteuliwa kuunda kamati hiyo na vyombo vyao katika mabano ni Amour Hassan (Mhariri wa habari za Michezo - NIPASHE), Elizabeth Mayemba (Mwandishi wa Majira), Dominick Isiji (Mhariri wa michezo - The African) na Rais wa Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU), ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Daily News, Mbonile Burton.
Wengine ni Mahmoud Zubeiyr (mmiliki bongostazblogspot), Athanas Kazige (Mwandishi Uhuru), Suleiman Jongo (Mwandishi-Citizens), Angela Msangi (Mwandishi TBC1) na Cosmas Mlekani (Mwandishi - Spotileo) na Tulo Chambo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) na pia Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Tanzania Daima.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa katibu wa kamati hiyo atakuwa Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando na kwamba kikao cha kwanza cha kamati kitafanyika jijini Dar es Salaam Jumatatu Machi 24 na kitafunguliwa na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, ambaye kwa sasa yupo safarini.

Robin van Persie 'aibeba' Man Utd, Borussia ikifa nyumbani kwao 2-1

Van Persie akifunga mkwaju wa penati
Kitu, Hulk akiifungia Zenit bao la kuongoza
MASHAMBULIAJI nyota wa Kiholanzi, Robin van Persie usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kuibeba Manchester United na kuivusha Roibo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bada ya kufunga hat trick wakiizamisha Olympiacos ya Ugiriki.
Manchester ambayo haikupewa nafasi kubwa miongoni mwa timu za England, ilipata ushindi huo kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford na kufuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 3-2 kwani katika mechi ya kwanza walichezea kichapo cha mabao 2-0 ugenini.
Mfungaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England, van Persie, alifunga utepe wa mabao kartika ya 25 kwa mkwaju wa penati kabla ya kuongeza jingine sekunde chache kabla ya mapumziko na kwa pasi ya Wayne Rooney na kuipeleka Mashetani Wekundu mapumziko wakiwa mbele kwa 2-0.
Kipindi cha pili wageni wakilisaka bao la kuwatibulia wenyeji, walishindwa kuhimili vishindo baada ya van 'Magoli' kuongeza bao la tatu dakia saba baada ya kuanza kipindi cha pili.
Katika mechi nyingine iliyochezwa nchini Ujerumani wanafainali wa mwaka jana wa michuano hiyo, Borussia Dotmund walijikuta wakichezea kichapo nyumbani chja mabao 2-1 dhidi ya Zenit.
Wageni waliwashtukiza Dotmund kwa bao la dakika 16 kupitia kwa Hulk kabla ya kuchomoa baadaye katika dakika ya 38 kupitia kwa Kehl aliyemalizia kazi ya Schmetzer na kufanya timu ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa hata jhivyo kipindi cha pili Zenith waliandika bao la ushindi kupitia Rondon.
Hata hivyo ushindi huo ulishindwa kuibeba Zenit kwa vile katika mechi ya kwanza nyumbani kwao walilala mabao 4-2, hivyo kuwapisha Wajerumani kufuzu robo fainali kwa jumla ya mabao 5-4.
Ratiba ya hatua hiyo kwa timu nane zilizofuzu inatarajiwa kutangazwa kesho, ingawa kuna hofu ya Chelsea kuangukia mikononi mwa Barcelona, Bayern Munich au Atletico Madrid.