STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Chelsea yarejea kileleni ikiibutua Stoke City 3-1

Mohamed Salah
Mohammed Salah akifunga bao la kuongoza la Chelsea dhidi ya Stoke City
KLABU ya Chelsea usiku huu imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua timu ya Stoke City kwa mabao 3-1 katika pambano lililochezwa uwanja wa Stanford Bridge.
Vijana wa Jose Mourinho wenye kibarua kigumu Jumanne ijayo dhidi ya PSG waliowatandika mabao 3-1 mjini Paris katika mechi ya robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliandika bao la kwanza dakika ya 32 kupitia Mohamed Salah aliyemalizia kazi ya Nimanja. Matić bao lililodu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha vijana vijana wa Darajani walikuja na nguvu mpya na kufanikiwa kuongeza bao la pili lililofungwa na kiungo wake mkongwe, Frank Lampard katika dakika ya 61' kabla ya Willian kuhitimisha karamu ya mabao dakika ya 72 kwa pande la Mohammed Salah.
Kwa ushindi huo Chelsea imefikisha jumla ya pointi 72 na kukalia kiti cha uongozi kwa muda kwa kuing'oa Liverpool ambayo itashuka dimbani kesho kubakabiliana na West Ham Utd katika mechi ya ugenini.
Mechi nyingine kwa mujibu wa ratiba hiyo, Everton itakuwa wenyeji wa Arsenal ya kocha Arsene Wenger.
Jumatatu  Tottenham Hotspur itakuwa ikijaribu kurejea kwenye nafasi yake ya sita baada ya jioni hii kuenguliwa na Manchester Utd itakapokuwa nyumbani kuikaribisha Sunderland.

Messi aizamisha Real Betis Hispania

Barcelona v Real BetisNYOTA wa Argentina, Lionel Messi ameendelea kutisha kwa mabao baada ya usiku huu kuizamisha Real Betis kwa kufunga mabao mawili yaliyoisaidia Barcelona kushinda 3-1.
Mchezaji huyo,  alianza kufunga bao katika dakika ya 14 kwa mkwaju wa penati kabla ya kuongeza jingine katika kipindi cha pili kwenye dakika ya 86.
Beki wa Betis, Jordi Figueras alijifunga bao na kuipa Barca uongozi wa mabao 2-0 katika dakika ya 67 kabla ya Rubén Castro kufunga bao la kufutia machozi dakika moja baadaye ndipo messi akaja kumalizia udhia na kuifanya Barca kuijongeza Atletico iliyopo kileleni.
Kivumbi cha ligi hiyo yta Hispania inaendelea hivi sasa Real Madrid ikiwa ugenini tayari inaoongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad, goli likifungwa na Illarramendi sekundu chache kabla ya mapumziko.

Leicester City yarudi Ligi Kuu ya England

http://legacymedia.localworld.co.uk/275788/Article/images/17264623/4288974.jpg
LEICESTER City imekuwa klabu ya kwanza kupanda Ligi Kuu ya England ikiirejea baada ya miaka 10 tangu iicheze kwa mara ya mwisho mwaka 2004.
Leciester ilijihakikisha nafasi hiyo ya kucheza EPL msimu ujao baada ya jana kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sheffield Wednesday na kuwafanya wafikishe pointi 89.
Pointi hizo zimeihakikishia moja ya nafasi mbili za kupanda moja kwa moja na hasa baada ya matokeo ya mechi zilizochezwa leo katika Ligi Daraja la Kwanza ya nchi hiyo.
Vijana hao wa Nigel Pearson wamepata nafuu zaidi baada ya Burnsley kulazimishwa sare ya 0-0 na kufikisha pointi 80, huku QPR ikikumbana na kipigo na kubakia na pointi zao 70 wakibaki nafasi ya tatu.

Wanafunzi, wazazi walivyoikaribisha likizo ya masomo Joyland

Wazazi walijitokeza kwenye sherehe hizo za kufunga shule

Wazazi wakinasa matukio kwa kamrra za simu zao

Kila mtu hakutaka kupitwa na jambo
Wanafunzi wa Joyland Pre & Primary International School
Wanafunzi wakiwa wamepozi na mmoja walimu
Mkurugenzi wa Joyland, Fredirick Otieno akizungumza kwenye hafla hiyo huku akipigwa na manyunyhu ya mvua
Mvua ilitaka kutibua mambo
Wanafunzi wa Joyland wakipangwa na walimu wao tayari kutoa burudani
Wazazi nao walikuwa wakinasa matukio
Wanafunzi wakiingia uwanjani kuonyesha makeke yao
 

Full heshima kwa wazazi
Wanaimba
Wanafunzi wakiimba
Kipaji cha muziki kipo hapa jamani acheni utani!
Yaani hakuna aloiyetaka kusimuliwa
Kila mmoja anajua anachokifanya uwnajani...Vipaji tupu!
Bendi ya shule ilikuwa kiburudisho tosha, jamaa kama Twanga Pepeta
Kama Victor Mkambi kwa kupapasa kinanda
Wataalam wa klabu ya Lugha ya Kiingereza wakiingia kuonyesha yao
Wakijiweka sawa


Wazazi wakiwa bize
 





 


 
Msosi nao ulikuwa sehemu ya sherehe hizo
Maandalizi ya kugawa msosi yalikuwa yakiendelea
 


Waliofanya vizuri walizawadiwa kama hivi
Wazazi walisaidia kuwapokea zawadi watoto wao
Mkurugenzi Otieno akiomba dua ya kufungia sherehe
Mandhari ya Shule ya Joyland International
Kwa hakika inavutia
 

Watoto wakifurahia mandhari ya shule hapa ni kwenye bwawa la maji
 

Watoto wakifurahia maji kwenye bwawa
 

Watoto wakicheza