STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 2, 2015

Wife wa Ali Kiba avuja mtandaoni, msikilize hapa


Maradhi ya Moyo ya Diamond hadharani usikilize hapa


Newz Alert! Francis Cheka ahukumiwa miaka mi3 jela

Cheka (kulia) katika mikutano ya mapambano yake pembeni yake ni promota Omar Kimbau
BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa nchini aliyewahi kuwa Bingwa wa Dunia wa WBF, Francis Cheka 'SMG' mwenye maskani yake mjini Morogoro amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Kwa mujibu wa kituo cha redio cha EFM kipindi cha Sports Headquarter, Cheka amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga meneja wake katika shughuli zake za biashara ya ukumbi wa Vijana Social mjini Morogoro anayedaiwa kumuingiza mjini kiasi kikubwa cha fedha kiasi cha kufikia kuchapana naye.
Akizungumza na kituo hicho baba mzazi wa Francis Cheka amesema haikuwa sahihi kwa mwanae kupewa hukumu hiyo na badala yake wangekaa na kuzungumza ili kuyamaliza matatizo hayo.
Mzee huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kuna watu wenye chuki na mwanae wameitumia kesi hiyo ya muda mrefu kutimiza malengo yao lakini pia mzee huyo ameelezea hisia zake kwa wakazi wa Morogoro kutoa sapoti ndogo kwa mwanae.
Taarifa zinasema kuwa Cheka amehukumiwa adhabu hiyo leo JUmatatu Februari 2, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
EFM.

Shaa kutoa mpya, video ya Subira bado yakwama

WAKATI video ya wimbo wake wa 'Subira' ikiwa inaendelea kupigwa danadana bila kuachiwa tangu itengenezwe, msanii Sarah Kais 'Shaa' yupo njiani kuachia kazi mpya.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo, Meneja wa msanii huyo Said Fella 'Mkubwa' alisema kuwa katikati ya mwezi huu Shaa ataachia kazi mpya kulingana na utaratibu waliojiwekea.
Akiwa chini ya Mkubwa na Wanae, Shaa ameshaachia nyimbo mbili za 'Sugua Gaga' na 'Subira' na hivi karibuni akiwa Kenya kikazi alitoa wimbo mpya uitwao 'Njoo' akishirikiana na mkenya Redsan.
"Tupo katika maandalizi ya mwisho kabla ya Shaa kuingia studio kutengeneza kazi mpya," alisema Fella na kufafanua juu ya video ya wimbo wa 'Subira' ambao ina muda mrefu tangu itangazwe itaachiwa hadharani bila mafanikio.
"Video hiyo imeshakamilika kitambo ila bado ipo mikononi mwa Adam Juma aliyeitengeneza, tukikabidhiwa tutaiachia mara moja," alisema Fella.
Alipoulizwa sababu ya kucheleweshwa kwa video hiyo alisema kuna mambo ambayo hawajaridhishana katika video hiyo ya 'Subira' ambayo ilitengenezwa mwishoni mwa mwaka jana kabla ya Shaa hajaenda Kenya.

Chegge, Mhe Temba, Madee kuzindua video zao Escape One

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRcuFMHdCOMH-6MJo0M0ke2rBniv8pPETU5_l3lk5chotAEkEwbjahckMWz6qtRuRnbCvvvfPLQcoQci2-PeTusKm9ik3rwx6oDiF6JkqNCZ27dc2yH8EhHF2u85Rr1GwBubQzST4gDeI/s1600/Madee+-+Vuvula.jpgWASANII nyota nchini Mhe Temba, Chegge na Madee wanatarajiwa kuzindua rasmi video ya nyimbo zao mpya walizorekodiwa nchini Afrika Kusini wakimshirikisha Dj Maphorisa wa Uhuru.
Meneja wa wasanii hao, Said Fella aliliambia MICHARAZO kuwa, uzinduzi wa video hizo utafanyika siku ya Jumamosi  kwenye ukumbi wa Escape One, Mikocheni.
Fella alisema Madee atazindua video ya wimbo wake uitwao 'Vuvula' wakati Chegge na Mhe Temba watazindua 'Kaunyaka' ambazo zinafanya vema kwenye vituo vya radio na televisheni.
Meneja huyo alisema uzinduzi huo utapambwa na burudani za wasanii kadhaa nyota watakaousindikiza akiwataja baadhi kuwa ni Diamond, Yamoto Band, Jux, Vanessa Mdee, Shaa na wengine.
"Madee, Chegge na Mheshimiwa Temba wanatarajia kuzindua video za nyimbo zao zinazoendelea kutamba hewani kwa sasa, uzinduzi utafanyika Escape One na utasindikizwa na wasanii kadhaa nyota akiwamo Diamond, Shaa, Vee Money na wengine," alisema Fella.

Costa ajitetea, adai hakukanyaga kwa makusudi

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/03178/CostaButt_3178918b.jpg
Diego Costa akizinguana na Martin Skrtel
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa amesema hakuwa na nia yeyote ya makusudi kumkanyaga mchezaji wa Liverpool Emre Can.
Chama cha Soka Uingereza-FA kilimtwanga adhabu kwa vurugu kutokana na tukio hilo lililotokea katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili wa Kombe la Ligi Jumanne iliyopita jambo ambalo Costa amelipinga.
Costa mwenye umri wa miaka 26 amesema jambo kubwa ni wakati akienda nyumbani kwake kulala na kujua kuwa hakufanya jambo lolote baya.
Strika huyo wa kimataifa wa Hispania amesema hakuwa na nia ya makusudi kutenda kitendo kile kwani ilikuwa bahati mbaya.
Hata hivyo Costa amesema amekubali na kuheshimu adhabu aliyopewa, japo  amesisitiza hakufanya vile kwa makusudi.

Baada ya kuwakosa Ndanda, Yanga kumalizia hasira Mkwakwani

Yanga
BAADA ya jana kushindwa kupata ushindi kama walivyoahidi mbele ya Ndanda Fc ya Mtwara, Yanga itaifuata Coastal Unioni nyumbani kwa Mkwakwani Tanga wakiwa na dhamira moja tu ya kupata pointi tatu.
Yanga ililazimishwa suluhu na Ndanda jana katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa jkwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuwafanya washindwe kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo unaoshikiliwa na Azam waliopo DR Congo, japo imerejea katika nafasi ya pili walioshushwa Jumamosi na Mtibwa Sugar.
Sare hiyo ya jana imeifanya Yanga kufikisha pointi 19 baada ya mechi 11, mbili nyuma ya Azam waliolingana nao kimichezo ambao kesho wanatarajiwa kumalizia mechi zao nchini Congo baada ya juzi kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya wenyeji wao TP Mazembe.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema wanatarajia kwenda Tanga kwa mechi tyao ya Jumatano wakiwa na nia mopja ya kuhakikisha wanapata ushindi kama ilivyofanya wiki iliyopita mjini Morogoro walipowafunga maafande wa Polisi kwa bao 1-0.
Muro alisema wanatambua pambano hilo litakuwa gumu kutokana na ukweli Coastal Union watakuwa nyumbani na hawajafanya vema katika mechi zao za karibuni, lakini wao hawatajali hilo zaidi ya kupata ushindi ili kujiweka katika nafasio nzuri ya kunyakua taji hilo.
"Matokeo dhidi ya Ndanda ni ya kawaioda katika mchezo na sasa tunajipanga kwa mechi ijayo dhidi ya Coastal Union tutakaowafuata Mkwakwani kwa dhamira moja ya kuvuna pointi," alisema Muro.
Tangu ligi iendelee tena baada ya mapumziko ya Novemba 9, Yanga imevuna pointi  sita tu katika mechi nne ilizocheza mpaka sasa baada ya kutoka sare ya 2-2 na Azam kisha kulazimishwa suluhu na Ruvui Shooting kabla ya kuwazabua Polisi Moro na kubanwa na Ndanda.

Renard awasifu Algeria licha ya kuwang'oa AFCON

http://zambianintelligencenews.com/wp-content/uploads/2013/08/Renard.jpg
Kocha wa Ivory Coast
KOCHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast Herve Renard amedai kuwa, wapinzani wao Algeria walikuwa wazuri zaidi yao licha ya kuwafunga bao 3-1 katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Renard ambaye aliwahi kuipa Zambia ubingwa wa michuano hiyo alisema kuwa, kikosi chake jana usiku kilikuwa dhaifu licha ya ushindi huo ulioiwezesha kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Washindi wa mchezo huo ndio walikuwa wa kwanza kupata bao lililowekwa kimiani na mchezaji mpya wa Manchester City Wilfried Bony, ambaye pia ndiye aliyefunga la pili baada ya Mualgeria El Arbi Hillel Soudani kusawazisha.
Gervinho aliihakikishia Ivory Coast ushindi baada ya kufunga bao la tatu katika dakika za majeruhi katika mchezo huo uliofanyika jijini hapa na kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kusonga mbele.
Renard alisema kuwa wapinzani wao hao kutoka Afrika ya Kaskazini walikuwa wazuri, lakini walishindwa kutumia nafasi zao vizuri.
"Kwa upande wa soka, mbinu, Algeria walikuwa bora zaidi yetu, " alisema Renard alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo.
Timu hiyo sasa itavaana na DR Congo walioiondosha Congo kwa mabao 4-2, timu nyingine iliyofuzu nusu fainali ni Ghana iliyoicharaza Guinea kwa mabao 3-0 na sasa watacheza na wenyeji Guinea ya Ikweta keshokutwa.
Naye Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Algeria Christian Gourcuff aliunga mkono maneno ya mwenzake, ambapo alisisitiza kuwa timu iliyoshinda haikuwa bora.
"Hii sio timu bora iliyoshinda. Kwa upande wa mchezo, tulicheza vizuri lakini bahati haikuwa yetu, " alibainisha Gourcuff.
"Wachezaji wa Ivory Coast hawakupata nafasi nyingi. Hawakustahili kushinda."
Gourcuff pia alitupia lawama ubora wa kiwanja, na kusema kuwa lilikuwa kosa lao kukubali kufungwa na Ghana baada ya kukubali bao la dakika za mwisho na kumaliza wa pili katika Kundi C kwani wangeshinda wangekuwa wa kwanza na wangeikwepa Ivory Coast katika robo fainali.
"Lakini ikiwa tumecheza mechi 10, lakini haujafungwa mara 10, ni wazi sisi ni timu bora…”