Na Boniface Wambura
KIINGILIO
cha chini kwenye mechi ya wanawake chini ya miaka 20 katika ya Tanzania
na Msumbiji itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 1,000.
Mechi
hiyo itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho ni kwa
ajili ya viti vya rangi ya kijani, bluu na chungwa. Viingilio vingine ni
sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh.
10,000.
Timu
ya Msumbiji inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Oktoba 23 mwaka huu) saa
8 kamili mchana kwa ndege ya LAM. Msumbiji yenye msafara wa watu 25
itafikia kwenye hoteli ya Sapphire.
***
UCHAGUZI TPL BOARD KUFANYIKA IJUMAA
Uchaguzi
wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) utafanyika Oktoba 25 mwaka huu
kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Golden Jubilee Tower.
Kwa
mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) wajumbe wanaounda Mkutano wa Uchaguzi ni wenyeviti kutoka klabu 24
za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na 14 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL).
Wagombea
kwenye uchaguzi huo ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Said Muhammad
Said Abeid (Makamu Mwenyekiti) wakati wanaoumba ujumbe wa Kamati ya
Uendeshaji ni Khatib Omari Mwindadi na Kazimoto Muzo.
***
RAMBIRAMBI MSIBA WA JIMMY MHANGO
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha mjumbe wa Bodi ya klabu ya Ashanti United, Jimmy Mhango
kilichotokea jana (Oktoba 21 mwaka huu).
Msiba
huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani Mhango aliutumikia
mpira wa miguu kwa muda mrefu, tangu akiwa mchezaji, kocha na baadaye
kiongozi.
Kabla
ya kuingia kwenye Bodi ya Ashanti United, enzi za uchezaji wake
alichezea timu za Mapinduzi ya Dodoma, Ushirika ya Moshi na Pan African
ya Dar es Salaam. Pia aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Ashanti United.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Mhango, klabu ya Ashanti United na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), na kuwataka kuwa
na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko
yamefanyika leo mchana katika makaburi ya Abeid (Mchikichini) Dar es
Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Mhango mahali pema peponi. Amina.