STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 22, 2013

Simba kurejea kileleni kesho, Yanga kuvuna nini kwa Rhion Rangers

Yanga inayodaiwa baadhi ya wachezaji kesho wakawekwa benchi baada ya sare ya 3-3 ma Simba
Simba iliyolazimisha sare na Yanga Jumapili
Coastal Union watakaivaa Simba kesho Mkwakwani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfKSZcZys5ESjlNhn6Du0VkOqGFVkb8gUCv3UzZirPkcebsNYfANbRVhAOAl1OqftHcSm5puEpVqo5axdm__Ah1pbye4T7d3Eg-l_zw18-_m9V3fncdtkMQFlUkVN689pvjUj0mNOjNsc/s1600/TIMU+YA+RHINO.JPG
Vijana wa Rhino Rangers watakaoivaa Yanga Taifa
BAADA ya kulazimisha sare ya maajabu ya 3-3 na watani zao Yanga, Simba kesho itakuwa na kibarua cha kutaka kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara watakapoikabili Coastal Unioni nyumbani kwao.
Pambano hilo la Wagosi wa Kaya na Wekundu wa Msimbazi litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ni kati yua mapambano matatu yatakayochezwa kesho katika mfululizo wa ligi hiyo.
Simba yenye pointi 19 iwapo itaikwangua Coastal ambayo imerejea jijini humo ikitoka kupoteza mechi mbili mfululizo, itakwea kileleni na kuziondoa Azam na Mbeya City zenye pointi 20 kila mmoja.
Hata hivyo Simba haipaswi kuchukulia kirahisi mchezo huo wa kesho kutokana na ukweli Coastal ipo nyumbani na isingependa kufanywa asusa kwa mara ya tatu tena katika ligi hiyo.
Simba iliyotua salama jijini humo ikiwa imewaacha baadhi ya nyota wake kwa sababu mbalimbali wakiwemo Abdulhalim Humud 'Gaucho' na Haruna Chanongo waliopewa adhabu ya kujiunga na timu ya vijana, itakuwa na kazi kubwa ya kusaka ushindi kwa Wagosi wa Kaya.
Mbali na mechi hiyo, mabingwa watetezi Yanga wenyewe watakuwa dimba la Taifa kupepetana na Rhino Rangers katika pambano linalotarajiwa kuwa gumu kutokana na maafande hao wa JWTZ kufanya vibaya hivi karibuni.
Ushindi wowote kwa Yanga utawafanya wafikishe pointi 19 na kuendelea kusalia kwenye nafasi yake ya nne, japo inategemea na matokeo ya mechi nyingine inayochezwa hiyo kesho kati ya Kagera Sugar na Prisons-Mbeya.
Iwapo Yanga itazembea katika mechi hiyo ya Rhino kama ilivyofanywa ilipocheza na Simba, kisha Kagera ikashinda mchezo huo wa ugenini basi inaweza kuwang'oa mabingwa hao watetezi katika nafasi hiyo.
Kagera yenyewe ina pointi 14 na kama itailaza Prisons itafikisha pointi 17, japo hakuna anayeamini Yanga kama itakubali kufa kwa Rhino Rangers.
Kocha wa Yanga Ernie Brandts amenukuliwa na mtandao wa klabu yake kwamba amesikitishwa sana na sare dhidi ya Yanga na kwamba anajipanga kwa ajili ya mechi ya kesho akiamini vijana wake hawatamuangusha tena.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014      
                                  P    W   D   L    F    A   GD   PTS
1.   Azam                   10   5    5   0   15   6    9     20
2.  Mbeya City           10   5    5   0   13   7   6     20
3.  Simba                     9    5    4    0   20  8  12    19
4.  Yanga                     9    4    4    1   18  11  7    16
5. Mtibwa Sugar        10   4    4    2   16  12  4    16
6.  Ruvu Shooting       10   4    3    3    12   9   3    15
7. Kagera Sugar          9    4    2    3    10   7   3    14
8.  JKT Ruvu              10   4    0    6     9   11 -2   12
9.  Coastal Union         9    2    5    2     7    6    1   11
10.Ashanti                  10   2    3    5    10  19 -9     9
11.Rhino Rangers        9    1     4    4     8   12 -4     7
12.Prisons                   9     1    4    4     5    12 -7    7
13. Oljoro                  10    1    3    6     8    16 -8    6
14.Mgambo               10    1    2    7     3    18 -15  5
 
Wafungaji:

8- Tambwe Amisi (Simba)
7- Elias Maguri (Ruvu Shooting), Juma Luizio ( Mtibwa Sugar)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Hamis Kiiza (Yanga)
4-
Didier Kavumbagu (Yanga), Peter Michael (Prisons), Kipre Tchetche (Azam),
3- Jerry Tegete, Mrisho Ngassa (Yanga), Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union),
2- Haruna Moshi (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John (Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary (JKT Oljoro), Khamis Mcha (Azam), Shaaban Nditti (Mtibwa Sugar), Betram Mombeki (Simba)

No comments:

Post a Comment