|
Uwanja wa Taifa ambao utaendelea kukamua kikawaida |
VIWANJA vyote ambavyo
tayari vimefungwa mfumo wa elektroniki vitatumia tiketi za elektroniki
isipokuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao wenyewe utachelewa
kidogo ili kuangalia kwanza mfumo huo unavyofanya kazi katika viwanja
vingine.
Kwa viwanja
vinavyotumia mfumo huo tiketi zinanunuliwa kupitia mtandao wa Vodacom ambapo mteja
ni lazima awe amesajiliwa katika MPESA. Ataanza kwa kupiga *150*03*02#
ambapo atapewa namba ya kumbukumbu anayotakiwa kuihifadhi kwani
ataulizwa wakati anafanya malipo kwa kupitia MPESA ambapo ataingia kama kawaida
kwa kutumia *150*00#.
Baada ya kulipa
atapewa namba ya tiketi ambapo atakwenda kwenye mashine maalumu za kuchapa
(printer) ambazo ziko katika vituo mbalimbali na kuchapa tiketi hiyo ambayo
ndiyo atakayokwenda nayo uwanjani.
Njia nyingine ya
kununua ni kwa wateja wa benki ya CRDB ambayo wamejisajili kwenye simbanking.
Wao wataingia kwa kutumia *150*03# na kufanya malipo ya tiketi. Nao baada ya
kupata namba watakwenda ku-print tiketi kwenye mashine hizo maalumu.
Vilevile tiketi
zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo katika maeneo
mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo watapata tiketi na
kwenda moja kwa moja uwanjani.
*DAR ES SALAAM*
Kwa mechi za Dar es
Salaam (Uwanja wa Azam) ambao ndiyo unaanza kutumia tiketi za elektroniki
maduka ya CRDB Fahari Huduma yanayouza tiketi hizo ni;
1 Shs
Distributors Limited (Mtoni Kwa Aziz Ally),
ABC Computer (Mtaa wa Samora), Abdi Ally
Abdi (Kariakoo), Aika- El Traders (Africana), Amaly Investment (Mtaa wa
Sikukuu, Kariakoo), Athuman Fakhi Adam (Kongowe, Mbagala) na Bemuda
Supplies Agency (Tegeta- Kibo Complex).
Benedict Traders
(Barabara ya Uhuru/Lumumba), Ellytex Investment (Mtaa wa Indira Gandhi), Fedha
Investment Limited (Pamba Road), Fuya Godwin Kimbita (Tegeta Block E),
Hakika Limited (Mtaa wa Swahili, Kariakoo), Irice Stationary (Tegea Kwa
Ndevu), Joshua Andrew Kisamo (Mtaa wa Kongo, Kariakoo), LB
Pharmacy (Mtoni Kijichi) na Lista Phares Barnabas (Tabata Segerea).
L.M.S. Agro Chemical
(Sokoni Kariakoo), Matei Laurent Kiria (Mbuyuni,
Kinyerezi), Michael
Elisante Mchomvu (Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo), Palmall General Supplies
(Barabara ya Shekilango), Rafabi Communications (Mtaa wa Livingstone,
Kariakoo), Therry Inestment Limited (Tegeta Kibaoni) na Wemerick Independent
Vehicle Diagnostic Company Limited (Mtaa wa Boko).
Mashine za kuchapia
tiketi zipo matawi ya CRDB Azikiwe, Holland House (mashine mbili),
Kariakoo, Tabata, Tegeta, Mbezi beach, Vijana na Quality
Center. Mashine
nyingine maeneo ya ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo (mbili), Kawe Oilcom, Tabata Camel,
Manzese, Ubungo Oilcom, Sabasaba na Mbagala Oilcom.
*BUKOBA*
Maduka ya CRDB Fahari
Huduma ni Tak-Biir Investment Company (Mtaa wa
Jamhuri, Bilele),
Mary Mother of Peace Buhembe School (Sido Block,
Rwamishenye), Muleba
Secretarial Bureau (Nyerere Road), Akimu Abdallah
Tirutoijwa (Mtaa wa
Forodhani), Jamila Rajabu Songoro (Mtaa wa Jamhuri, Bilele), Rukia Kassim
Mohamed (Mtaa wa Kashai, Kashenye) na Novath Michael Kibira (Uganda Road,
Majengo).
Mashine tatu za
kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi laBukoba.
*TANGA*
Maduka ya CRDB Fahari
Huduma ni Fax Auction Mart (Sabasaba Ground, Korogwe Road) na Rozalia
Aloyce Masanja (Usagara, Block K). Mashine tatu za kuchapia tiketi
(printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Tanga.
*MBEYA*
Maduka ya CRDB Fahari
Huduma ni Blue Bird Bureau de Change (Lupa way), Meenda Pharmacy
Limited (Maendeleo), Access Computer Limited (Lupa way,
Sisimba) na Japhes
James Mwanjisi (Mtaa wa Njisi). Mashine za kuchapia tiketi (printers)
zipo Benki ya CRDB Tawi la Mbeya (mbili), Tawi la Mwanjelwa na Uyole.
*MOROGORO*
Duka la CRDB Fahari
Huduma ni Shambani Graduates Enterprises Limited (Kihonda) na pia
kutakuwa na gari za CRDB (Mobile bank). Mashine za kuchapia tiketi
(printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Morogoro, Msamvu na Morogoro Agency.
*ARUSHA*
Maduka ya CRDB Fahari
Huduma ni Fanuel John Andrew (Arumeru, Maji ya Chai),
Robert William Maeda
(Arumeru, Usa River), Wakwetu General Supplies (Mtaa
wa Ngongongare,
Arumeru), Wallace Ndawonga Mtawa (Kimandolu Suye), Side
Corner Multi Business
(Levolosi, Makao Mapya Street) na Albertha Ibrahimu
General (Usa River
Bus Stand).
Mashine za kuchapia
tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Arusha
(mbili), Tawi la
Meru, TFA, TRA Mapato na Ngaramtoni.
*MWANZA*
Maduka ya CRDB Fahari
Huduma ni Majura General Supplies (Mecco Street),
Prisca Joachim Kitani
(Gilishi Street), Niche Consult (Nyerere Road),
Deogratias Just
Silayo (Malimbe, Mkolani), Yohana Ndili Mahago (Igoma
Mashariki), Emily
Elias Sambo (Sweya Street), Y Financing Limited
(Kilimahewa) na
Mangare Office Solutions (Station Road).
Makoye E. Serikali
(Ilemela, Kiseke Street), Elizabeth George Kiwia (Uhuru
Road), Mwalimu
General Services (Kitangiri Road), George Edward Mulambo
(Pasiansi), Nginila
Office Solutions (Rufiji Street), Elvando IT Solutions
(Nkrumah, Nyamagana),
Sarimosa Company Limited (Kaluta Street) na Sahara
Trasport and
Scrappers Dealers (Mission, Pamba Road).
Mashine za kuchapia
tiketi (printers) zipo CRDB matawi ya Mwanza, Nyerere
na Mwaloni wakati
nyingine zipo Nyanza, Buzuruga na Ilemela.