Uongozi
wa klabu ya Young Africans umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusiana na
usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel
Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji imemzuia kuichezea
Young Africana mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.
Young Africans ilikamlisha usajili wa mshambuliaji huyo tangu Disemba
15 mwaka 2013, na kupata hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC)
ambayo iliwasilishwa TFF pamoja na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu ya
Vodacom.
Baada ya kukamilisha zoezi hilo TFF ilipitisha jina lake
kwa kutupatia leseni no: 921225001 ambayo inamruhusu mchezaji kuichezea
Young Africans na kisha kulituma CAF Disemba 31, 2013 kwa ajili ya
mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika ambapo CAF nao walimuidhinisha
kuwa mchezaji halali wa Young Africans kwa mashindano hayo.
Cha
kustaajabisha siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Kamati
ya Maadili na hadhi za wachezaji wakamzuia mchezaji huyo kuichezea
Young Africans ilihali akiwa ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa
mchezaji halali wa Young Africans.
Swali?? walikuwa wapi Kamati ya
Maadili na Hadhi za Wachezaji kujiridhisha juu ya usajili ambao
ulishakamilika tangu Disemba 15 2013?
Wanakuja kutoa maamuzi hayo
mwezi mmoja na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa, ikiwa ni siku
mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom?? YOUNG AFRICANS
No comments:
Post a Comment