TIMU za soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC
na Taswa Queens kesho Jumamosi zitapamba katika bonanza la muziki la bendi
ya Msondo Ngoma kwa kupambana na timu za veterans za Bandari wanaume na
wanawake.
Mchezo
huo umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa TCC, Chang’ombe kuanzia saa
8.00 mchana na maandalizi yake yamekamilika kwa mujibu wa mwenyekiti wa
Taswa SC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa mechi hizo zinatarajiwa kuwa
ngumu na za kusisimua kutokana na rekodi ya timu zote mbili.
Majuto
alisema Taswa FC na Taswa Queens hazijawahi kupoteza mechi yoyote mwaka
uliopita na kuweza kutwaa vikombe mara mbili mkoani Arusha na hivi
karibuni waliweza kuzichapa timu ya wanamuziki wa Twanga Pepeta,
Kombaini ya Leaders Club na shirika la maendeleo ya mafuta (TPDC).
Alisema
kuwa timu zake zitakuwa zinacheza kwa mara ya kwanza mwaka huu kwenye
uwanja wa TCC na hivyo mashabiki watarajie kupata burudani safi ya mpira
na muziki kutoka kwa bendi ya Msondo Ngoma ambayo itatambulisha nyimbo
zake mpya ambazo zitakuwa zinatambulishwa kwa mara ya kwanza.
“Tutaanza
kutoa burudani kwa mashabiki na baadaye kuamia kwa Msondo Ngoma,
tunatarajia kuwapa burudani safi ambayo itakuwa ya kwanza mwaka huu,
mbali ya mechi yetu, timu ya Mass itapambana na Farion, ambapo timu ya
maveterani wa Temeke inayojiita kwa jina la Kamazamani itapambana na
timu ya Tall, “ alisema Majuto.
Wakati
huo huo; bendi ya Msondo ngoma na Twanga Pepeta, jumapili zitatumbuiza
jukwaa moja kwenye ukumbi wa CCM Kata 14, Temeke. Burudani hiyo itakuwa
ya kwanza mwaka huu kwa wakazi wa Temeke na vitongoji vyake kwa bendi
hizo kupiga pamoja. Twanga itaonyesha shoo na nyimbo zake mpya.
No comments:
Post a Comment