STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 6, 2013

Mussa Mgosi atua Mtibwa Sugar kumrithi Javu

Mussa Hassain Mgosi
MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Simba Mussa Hassan Mgosi amejiunga rasmi na klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Morogoro.

Mgosi ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia klabu ya JKT Ruvu amejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Akiongea na mtandao huu, kocha wa Mtibwa Sugar  Mecky Mexime amethibitisha kwamba klabu yake imemsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba.
 
"Mgosi anakidhi vigezo vya mshambuliaji tunayemhitaji baada ya kuondoka wa Javu aliyejiunga na Yanga. Ameshaini mkataba wa mwaka mmoja na atajiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya hivi karibuni."
 
Shafih Dauda

Kumekucha Tamasha la Idd Mosi Dar Live


Meneja wa Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu burudani mbalimbali zitakazokuwepo Dar Live sikukuu ya Idd Mosi.
WASANII wa muziki watakaopanda katika jukwaa la kisasa la Dar Live sikukuu ya Idd Mosi pamoja na mabondia leo wamelonga na wanahabari kwenye mkutano uliowakutanisha ambao umefanyika katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wasanii wametambiana kila mmoja akitamba kuwa atamfunika mwenzake. Vilevile mabondia nao wametunishiana misuli hali inayoonyesha kuwa kutakuwa na bonge la burudani katika sikukuu hiyo ya Idd Mosi.
Katika sikukuu hiyo wasanii Ali Kiba, H-Baba, Chegge, Temba, Dogo Aslay, Bi. Cheka na Bendi ya Mapacha Watatu watashusha bonge la burudani na kuwapa raha mashabiki watakaohudhuria shoo hiyo. Kwa Upande wa masumbwi bondia Francis Miyeyusho atazipiga na Darius Lupupa kutoka nchini Zambia, Chupaki Chipindi atapigana na Ramadhan Kido. Vilevile mabondia wa kike Ester Kimbe na Irene Kimaro wataonyeshana moto siku hiyo.
(PICHA: SHAKOOR JONGO /GPL)
Mwanamuziki H – Baba akitamba mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuwa atafunika mbovu siku hiyo.

Mratibu wa mapambano ya ndondi, Abdallah Yasin ‘Ustaadh’ (kulia) akiongea na wanahabari. Kushoto ni Abdallah Mrisho.

Mwanamuziki Ali Kiba (kulia) akipeana ‘hi’ na Ustaadh wakati wa mkutano huo.
Bondia Francis Miyeyusho akitunisha misuli. Bondia huyu atapigana na Mzambia Darius Lupupa.

Bondia Chupaki Chipindi atakayezipiga na Ramadhan Kido.
Ramadhan Kido atakayepambana na Chupaki Chipindi siku hiyo.
Mabondia wa kike Ester Kimbe (kushoto) na Irene Kimaro wakijaribu kuzipiga.

Mabondia Francis Miyeyusho (kulia) na Ramadhan Kido (kushoto) wakifuatilia mkutano huo.
Chupaki Chipindi kutoka mkoani Iringa akiwa kwenye pozi.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Bondia Ester katika pozi.
Bondia Irene naye akiwa kwenye picha ya pozi.
H – Baba katika pozi la kusimama.
Ester ndani ya gloves.

Rufaa 84 zakatwa Baraza la Ushidani

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/08/IMG_1843.jpg
Na Suleiman Msuya
KWA kipindi cha zaidi ya miaka sita tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushindani (FCT) jumla ya rufaa 84 zimesajiliwa 36 zimesikilizwa na kutolewa uamuzi na jopo la wajumbe waa Baraza hilo.
Hayo yamebainishwa Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa FCT Nzinyangwa Mchany wakati akijibu swali la mwandishi wqa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
Alisema katika rufaa hizo 29 zilisitishwa kutokana na wahusika kuamua kuziondoa baada ya kufikia maamuzi ambayo baraza hilo halina mamlaka yakuingilia ambapo kwa sasa rufaa zinazoendelea kusikilizwa ni 19.
Mchany alisema Baraza la Ushindani limejipangia kusikiliza rufaa 24 kwa mwaka iwapo zitakuwepo lakini bado mwitikio ni mdogo hali ambayo inatajwa kuwa inachangiwa na uelewa mdogo kutoka katika jamii juu ya FCT.
“Baraza la Ushindani FCT limeanza kazi rasmi mwaka 2007 ambapo huwa tunapokea rufaa kutoka katika kwa watu na taasisi mbalimbali ambazo zinakuwa hazijaridhika na maamuzi ambayo yanatolewa na  mamlaka za udhibiti hapa nchini,” alisema.
Kwa upande wake Mwanasheria Mwandamizi Hafsa Said  alisema pamoja na mafanikio hayo madogo ambayo wameweza kuyapata tangu kuanza kwa FCT bado wana changamoto chache ambazo zinawakabili.
Alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni uchache wa majaji wa kusikiliza rufaa ambapo wamekuwa wakifanya kazi kwa muda maalumu (party time) kutokana na ukweli kuwa ni watumishi wa Mahakama ya Kuu nay a Rufaa.
Said alitaja changamoto nyingine ni ufahamu mdogo kwa jamii juu ya FCT ambapo wanajipanga kwa kushirikiana na mamlaka za udhibiti kutoa elimu hiyo ili wananchi na jamii kwa ujumla kutopoteza haki zao pale wanapoona kuna dalili za kuzikosa.
Pia alisema pamoja na changamoto hizo kupitia maamuzi yao wanayotoa ubora wa mamlaka za udhibiti umeongezeka jambo ambalo linaleta tija kwa jamii.
Alisema tangu waanze kupokea rufaa zinazotoka kwa taasisi na watu binafsi asilimia kubwa ya maamuzi yamekubalika ambapo ni maamuzi mawili tu ndio yaliendelea katika ngazi zingine za kimaamuzi.
Mwanasheria huyo Mwandamizi alitoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali ambazo zinasimamiwa na mamlaka kama TCRA, SUMATRA, EWURA, FCC na TCAA kujitokeza kukata rufaa iwapo watakuwa hawajaridhika na maamuzi yao.

MSD yatataka uwekezaji zaidi sekta ya dawa

BOHARI ya Dawa nchini (MSD) imetoa rai kwa wawekezaji kuwekeza katika sekta ya viwanda vya kuzalisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ili kuhakikischa kuwa nchi inapiga hatua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Isaya Mzoro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na ukweli kuwa asilimia 80 ya dawa, asilimia 95 ya vifaa tiba na vitendanishi vya maabara asilimia 100 huagizwa kutoka nje hali ambayo inachangia fedha nyingi kufaidisha nchi zingine.
Mzoro alisema ni vema wawekezaji wan je na ndani wakajitokeza kuwekeza katika viwanda ambavyo vitajihusisha na uzalishaji wa mahitaji yote ambayo yanahusu afya ya binadamu hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kabla ya kuanzishwa MSD hapa nchini kulikuwa na viwanda vya kutengeneza dawa zaidi ya saba lakini hadi sasa ni viwanda viwili ambavyo vinafanyan kazi hivyo kusababisha Serikali kuagiza dawa kutoka nje.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba watu kutoka nje au ndani ya nchi kuwekeza katika sekta hii ya uzalishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwani ni fedha nyingi ambazo zinaenda nje kwa lengo hilo,” alisema.
Aidha alisema pamoja na changamoto hiyo kubwa ya ukosefu wa viwanda MSD imefanikiwa kufikisha huduma za ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa huduma zao kwa asilimia 75 jambo ambalo linawapa matumaini kwa siku za karibuni.
Mzoro alisema MSD kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali ina mpango wa kupanua maghala kwa kukamilisha ujenzi wa awamu ya pili ili kuongeza nafasi za kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
Alisema MSD inatumia mfumo wa EPICOR 9 tangu mwezi Agosti 2012 ambapo wanatoa mafunzo endelevu kwa watumishi wao ili waweze kutoa huduma kwa haraka na kwa ufanisi.
Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi huyo alisema MSD inakabiliwa na changamoto nyingi kama ongezeko kubwa la mahitaji ya dawa ukilinganisha na uwezo serekali, ucheleweshaji wa kufikishwa pesa MSD kutoka hazina, Halmashauri kutotumia vyanzo vingine vya fedha, uhaba wa viwanda vya dawa nchini.
Changamoto nyingine taratibu za ununuzi kuchukua muda mrefu na baadhi ya zahanati na vituo vya afya kutopeleka maombi ya dawa na vifaa tiba katika kanda za MSD kama utaratibu unavyohitaji.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema matarajio yao ni kushirikisha sekta binafsi katika kusambaza dawa na vifaa tiba, kubandika orodha ya dawa na vifaa tiba vilivyokabidhiwa vituoni, kuendelea kuweka nembo ya serikali kwenye vidonge, kushirikisha sekta binafsi katika kutoa huduma ya dawa na vifaa tiba na waganga kuwasilisha maombi mapema.

Shilole kukomaa na jiji videoni hivi karibuni

Zuwena Mohammed 'Shilole'
MUIGIZAJI nyota wa filamu anayejishughulisha pia na muziki, Zuwena Mohammed 'Shilole' yupo mbioni kuachia video ya wimbo wake unaoendelea kutamba wa 'Nakomaa na Jiji'.
Akizungumza na MICHARAZO leo, Shilole alisema video hiyo iliyorekodiwa nchini Marekani alipoenda ziarani hivi karibuni kwa sasa inahaririwa kabla ya kuachiwa hewani mashabiki waone namna anavyokomaa na jiji.
Shilole alisema tofauti na nyimbo za nyuma kama 'Lawama', ' Dada Dume', 'Dudu' au 'Paka la Baa' ambazo zipo katika miondoko ya 'Chakacha' safari hii ametoka kivingine katika Bongofleva kuonyesha uwezo alionao katika fani hiyo ya muziki.
"Wakati wimbo wangu wa 'Nakomaa na Jiji' ukiendelea kuwa gumzo kwa sasa, nakamilisha mipango ya kuachia video yake hivi karibuni ili kuwapa raha mashabiki wangu," alisema Shilole.
Mkali huyo, alisema video hiyo aliipiga katika jiji la New York alipoenda Marekani na kwamba kila kitu kimekamilisha kwa ajili ya kuhakikisha anaiachia mapema iwezekanavyo.
Pia alisema kutoka hadharani kwa video ya 'Nakomaa na Jiji' itakuwa fursa yake nyingine ya kujiandaa kutoa kazi nyingine katika mtindo wa 'bandika bandua'  ili kuwapa raha mashabiki wake.
Shilole alisema ana hazina kubwa ya muziki katika stoo yake na ndiyo maana kila mara anawaangushia mashabiki wake nyimbo mpya kali kama alivyofanya katika kazi zilizopita ambapo kabla ya 'Nakomaa na Jiji' alikuwa gumzo na wimbo wa 'Paka wa Baa'.

Side Boy Usimdharau Usiyemjua

Msanii Side Boy katika pozi
MSANII wa miondoko ya Bongofleva anayejishughulisha na ujasiriamali, Said Salim 'Side Boy Mnyamwezi', anayetamba na wimbo wa 'Hujafa Hujaumbika' yupo mbioni kuachia kazi mpya iitwayo 'Usimdharau Usiyemjua'.
Akizungumza na MICHARAZO, Side Boy alisema wimbo huo aliorekodi katika studio za Pamoja Records, ni utangiulizi wa nyimbo za albamu yake ya tatu anayotarajia kuitoa hivi karibuni.
Side Boy aliyewahi kutamba na nyimbo kama 'Kua Uone', 'Jifungue Salama' na 'Pongezi wa Kikwete', alisema wimbo huo mpya ameuimba peke yake yake tofauti na kazi yake iliyopita ya Hujafa Hujaumbika alioimba na wasanii Best Naso na Aunty Ezekiel 'Gwantwa'.
"Baada ya kutamba na 'Hujafa Hujaumbika' kwa sasa najiandaa kuachia wimbo wa 'Usimdharau Usiyemjua' ambao nimeimba pekee yangu na ni utambulisho wa albamu yangu ya tatu inayokuja," alisema.
Side Boy alisema albamu hiyo ijayo inayofuata baada ya zile za 'Kua Uone' na 'Acha Waseme' itatoka ikiwa na cd mbili kwa moja ikijumuisha video na audio, ili kuwapa raha mashabiki wake na wale wa muziki wa ujumla.
"Albamu yangu ijayo ambayo bado sijaipa jina itatoka ikiwa na CD mbili,. moja video na nyingine au audio ili mashabiki wasisumbuke," alisema.,
Msanii huyo aliyewahi kufanya kazi pamoja na kundi la TMK Wanaume Family, japo hakuwa 'membaz' wa kundi hilo, alisema mashabiki wake wajiandae kupata ladha mpya toka kwake kutokana na albamu hiyo ya tatu anavyoiandaa kwa sasa itakayokuw ana nyimbo nane.

Kibudu cha Msechu kuandaliwa Kenya

Peter Msechu
 Na Elizabeth John

HATIMAYE ngoma inayokwenda kwa jina la ‘Kibudu’ liyoimbwa na mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Peter Msechu, imeanza kutamba katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na ujumbe wa mashairi yaliyomo ndani yake.

Mbali ya kutamba na kibao hicho, mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Relax’, ‘Kumbe’ ambavyo vilifanya vizuri zaidi mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vilimtambulisha katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msechu alisema katika kazi hiyo kamshirikisha mkali wa muziki huo, Ally Nipishe na kwamba tayari imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Alisema kibao hicho kakitengeneza katika studio ya Ufundi Production chini ya mtayarishaji wake mahiri, Fundi Samuel.
“Naomba mashabiki wangu wakipokee vizuri kibao hicho ambacho natarajia kukifanyia video yake Nairobi, Kenya,” alisema.

Msechu aliwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya video hiyo ambayo anatarajia kuitoa mwinzoni mwa mwezi ujao ikiwa ni pamoja na nyimbo nyingine nyingi zinazofuata.

Awamu ya kwanza usajili wa wachezaji wakamilika



Na Boniface Wambura
HATUA ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2013/2014 imefungwa rasmi jana (Agosti 5 mwaka huu) ambapo klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zimewasilisha usajili wa vikosi vyao ndani ya wakati.

Baadhi ya klabu zimefanya makosa madogo madogo katika usajili ambapo zimepewa siku ya leo (Agosti 6 mwaka huu) kufanyia marekebisho kasoro hizo. 

Hivyo kesho (Agosti 7 mwaka huu) majina ya vikosi vyote yatabandikwa kwenye mbao za matangazo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kipindi cha pingamizi kitakachomalizika Agosti 12 mwaka huu.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.

Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 14 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania. 

Hivyo, dirisha la uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya usajili kumalizika Agosti 29 mwaka huu.

TFF yaridhia 3 Pillars ya Nigeria kucheza Bongo



Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa baraka zote kwa timu ya 3Pillars Football Club ya Nigeria kucheza mechi za kirafiki nchini baada ya kupata idhini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nigeria (NFF).

Awali tuliikatalia timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini kwa vile haikuwa na barua kutoka NFF, lakini sasa Shirikisho hilo limetoa idhini hiyo. Pia ziara yake haikuwa inaratibiwa na wakala wa mechi anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) au mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Klabu hiyo kutoka Jimbo la Lagos ilipanga ziara hiyo kwa kuwasiliana na chama cha mpira wa miguu cha jimbo hilo ambacho nacho kilitakiwa kuomba idhini NFF kwa niaba ya 3Pillars.

Hivyo timu hiyo inaweza kucheza mechi, kwani ziara hiyo sasa inaratibiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambaye ni mwanachama wetu.

Tunapenda kukumbusha kuwa watu pekee wanaotakiwa kuandaa mechi za kirafiki za kimataifa ni mawakala wa mechi wanaotambuliwa na FIFA au wanachama wa TFF.