STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 24, 2013

Ruvu Shooting yaichimba mkwara Simba

Ruvu Shooting

Simba wanaotaka kulinda heshima

UONGOZI wa klabu ya soka ya Ruvu Shooting ya Pwani imeichimba mkwara Simba itakayovaana nayo kesho kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikitamba kuwa ni lazima 'mnyama' afe wakitaka kulinda heshima yao.
Akizungumza na MICHARAZO Afisa Habari wa klabu hiyo, Masau Bwire, kwamba mchezo huo kwao wanauchukulia kama fainali na hivyo watashuka dimbani kwa nia moja ya kusaka ushindi ili kudhihirisha kwamba wao ni bora kuliko wana Msimbazi.
"Tunahitaji kuutumia mchezo wa kesho (Alhamis) dhidi ya Simbaili kujenga heshima ya kisoka kwa timu yetu na kuwadhihirishia Watanzania kwambatimu yetu ni nzuri na ina vijana wenye vipaji na uwezo mkubwa wa soka, muhimu sheria 17 zizingatiwe," alisema Bwire.
Msemaji huyo alisema wanaiheshimu Simba kama klabu kongwe na timu yenye uwezo mkubwa kiuchumi na yenye kiu ya kutaka kulinda heshima yake angalau kuambulia nafasi ya tatu baada ya kulitema taji la ubingwa, lakini bado watashuka dimbani kwa dhamira moja tu ya kupata pointi tatu.
Bwire alisema kikosi chao kinachonolewa na kocha Charles Boniface Mkwara hawatakuwa tayari kuwa daraja la mafanikio ya Simba hiyo kesho na hivyo kuwaonya wanamsimbazi kwamba wakae chonjo na wasitarajie mteremko.
"Kocha katuhakikishia kwamba wachezaji wake wopte wapo vyema kwa ajili ya pambano hilo kitu ambacho kinatuma matumaini ya kuanya vyema mbele ya Simba," alisema Bwire.
Hata hivyo pambano hilo la kesho halitakuwa na maana yoyote kwa timu hizo kwani zote hazina matumaini ya ubingwa wala kupata nafasi ya uwakilishi wa mechi za kimataifa mwakani ambazo tayari zimeshachukuliw ana timu mbili za juu za Yanga na Azam.

JKT Ruvu yazishusha rasmi daraja Lyon, Toto African

JKT Ruvu waliozishusha daraja Lyon na Toto Africans

TIMU ya maafande wa JKT Ruvu wamezishusha rasmi timu za African Lyon na Toto African baada ya jioni ya leo kupata ushindi uliowavusha kwenye hatari ya kurudi Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Maafande hao waliokuwa wakiuguza kipigo cha mabao 3-0 toka kwa vinara wa ligi hiyo Yanga, ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lyon katika pambano lililofanyika kwenye uwanja wa Chamazi na kuifanya kufikisha pointi 26 ambazo haziwezi kufikiwa na timu za Toto na Lyon.
Lyon na Toto zikishinda mechi zao zilizosalia katika ligi hiyo zitazifanya zifikishe pointi 25 tu na hivyo kuwa vigumu kwao kupona kwenye timu tatu za kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Lyon imesaliwa na mechi mbili ikiwa na pointi 19, ilihali Toto imesaliwa na mechi moja tu ikiwa na pointi zake 22, hali ambazo inazipa tiketi ya kurudi Ligi Daraja la Kwanza na kusubiri timu ya mwisho ya kuungana nao.
Miongoni mwa timu zilizopo katika janga hilo la kuzifuata klabu hizo ni Polisi Moro iliyosaliwa mechi tatu ikiwa na pointi 19, Mgambo Shootinmg yenye pointi 25 na kusaliwa na mechi mbili ikiwamo dhidi ya Simba.
Pamoja na ushindi huo wa bao 1-0 jioni ya leo bado haijaiweka salama JKT Ruvu kwani italazimika kupata ushindi kwa mechi zake mbili zilizosalia ili kuvuna pointi zaidi zitakazowatoa eneo hilo la hatari.
JKT Ruvu, Mgambo JKT, Polisi Moro na Prisons moja wapo inaweza kuungana na Lyon na Toto iwapo itazembea katika mechi zao zilizosalia.
Kipute cha ligi hiyo kitaendelea tena kesho kwa pambano moja kati ya Simba na Ruvu Shooting pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa, kabla ya Ijumaa kushuhudiwa kipute kingine ambacho kinaweza kutangaza bingwa mpya nchini iwapo Azam itachemsha mbele ya wenyeji wao Coastal Union ya Tanga.
Pambano la timu hizo litachezwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo Azam italazimika kupata ushindi iwapo itataka kuwatia presha Yanga wanaosubiri kulitwaa taji hilo.
Azam wana pointi 47 na kama itashinda mechi zake tatu zilizosalia itafikisha pointi ambazo tayari Yanga imeshazikusanya ikiwa ina michezo miwili mkononi ukiwamo dhidi yua mahasimu wao Simba.

KWA WADAU WA MASUALA YA SHERIA

Laws of Tanzania (CD-ROM) (Principal and subsidiary legislation revised edition 2002

Inline image 1
This is the first complete revision of the laws of Tanzania since 1966 and
comprises principal legislation and subsidiary legislation in force on 31
July 2002. The principal legislation consists of 415 chapters arranged
numerically. There are ten main volumes and a supplementary volume, which
contains the index, alphabetical and chronological tables and certain
omitted Acts which were not in force at the completion of the Law Revision
of 2002. The revised edition of the subsidiary legislation has been
arranged in a similar fashion and consists of ten volumes. The edition
consists of various tables of content; the Constitution (in Kiswahili); and
the ordinary laws of the country (Acts and subsidiary legislation), set out
in numbered chapters.

*Contents Include:*

   - Statutes of Tanzania, revised edition 2002
   - Principal legislation consisting of 415 Chapters in 10 volumes
   - Supplementary Volume with alphabetical and chronological Table of Acts
   - Subsidiary Legislation consisting of 10 volumes

Pricing for single-user, main work archive only). Publication not updated.
Multiple-user pricing available on request.

*Of Interest and Benefit to:*

   - Judicial officers
   - Prosecutors
   - Legal practitioners
   - Libraries
   - Academics

*Key Benefits:*

   - Powerful electronic searching allows for easy and rapid access to
   information
   - Handy hyperlinks facilitate easy navigation within the product

ORDER TODAY!

contacts : WIGO
Mob: +255 655 308308,
        +255 767 102102,
email: cerengeti@gmail.com


TAIFA STARS KUSHIRIKI MICHUANO YA COSAFA

Kocha Kim Poulsen kati
Na Boniface Wambura
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashiriki michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika Julai mwaka huu nchini Zambia.

Taifa Stars inashiriki michuano hiyo ya timu za Taifa za nchi wanachama wa COSAFA ikiwa timu mwalikwa. Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoro, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.

Michuano hiyo itafanyika kuanzia Julai 6 hadi 21 mwaka huu katika miji ya Lusaka, Ndola na Kabwe. Ratiba ya makundi ya michuano hiyo itapangwa Mei 3 mwaka huu jijini Lusaka.

Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika miaka mitatu iliyopita. Hii itakuwa mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo baada ya kucheza ya kwanza iliyofanyika mwaka 1996 nchini Zimbabwe.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajia kuingia kambini mwishoni mwa mwezi ujao kujiandaa kwa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Juni 16 mwaka huu Taifa Stars itacheza na Ivory Coast jijini Dar es Salaam katika mechi nyingine ya mchujo ya Kombe la Dunia wakati Juni mwishoni na Julai mwanzoni itacheza mechi ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.

Wakati huo huo, waandishi wa habari wanaotaka kuripoti michuano hiyo wanatakiwa kuwasilisha majina yao TFF kabla ya Aprili 27 mwaka huu ili maombi yao yatumwe COSAFA kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho (Accreditation).

AMCHINJA MAMA YAKE AKIMTUHUMU UCHAWI


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman.

WATU wawili wameuawa katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya, likiwamo la kijana kumchinja mama yake kwa kutumia kisu kama kuku baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi aliyemloga mkwe wake.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki, jana aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio la kijana kumchinja mama yake mzazi limetokea juzi majira ya saa 1:00 jioni katika kijiji cha Chobwe wilayani Ileje.

Alimtaja mwanamke aliyetuhumiwa kuwa ni mchawi na kisha kuchinjwa na mwanae kuwa ni Anna Panja (60) mkazi wa kijiji cha Chobwe.

Akisimulia tukio hilo, Masaki aliema kijana huyo aitwaye Michael Panja akiwa na mwenzake ambaye bado hajafahamika, walimvamia mama huyo nyumbani kwake akiwa amelala na mumewe Basale Panja (76), wakamchukua mama huyo na kumchinja shingoni kwa kutumia kisu na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema baada ya kutenda unyama huo, Michael na mwenzake walitoroka na kwenda kusikojulikana.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Aidha, alitoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wajenge utamaduni wa kufikisha malalamiko na kero zao kwa vyombo husika ili yaweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Katika tukio la pili, kundi la wananchi wenye hasira wakitumia silaha za jadi walimuua Lufingano Nsinge (32), baada ya kumtuhumu kujihusisha na matukio ya mauaji ya watoto wadogo yaliyokuwa yakitokea katika kijiji chao.

Kamanda Masaki alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3:00 usiku katika kijiji cha Ndala, kata ya Kandete kwenye kitongoji cha Katumba wilayani Rungwe.

Akisimulia tukio hilo, Masaki alisema marehemu Nsinge siku ya tukio aliingia ndani ya nyumba ya John Mwansamaleba (53) kwa nia ya kufanya uhalifu na ndipo alipokutwa na wananchi hao.

walioamua kuchukua sheria mkononi kwa kumshambulia kwa silaha za jadi kama vile mipini, shoka, kuni na mapanga na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanne kuhusiana na tukio hilo.

Aliwataja watu hao kuwa ni John Mwasamaleba, Angolisye Mwakalinga (30), Lukas Mwasamaleba (40) na Leah Ndemange (45), wote wakazi wa kijiji cha Ndala.
 
CHANZO: NIPASHE

Kamati ya Utendaji Simba yamaliza mzozo wa makocha wao


Makocha wa Simba, Julio na Liewig waliosuluhishwa na kamati ya utendaji ya Simba
KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba imemaliza mzozo uliokuwepo kati ya makocha Patrick Liewig na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelu 'Julio' baada ya kuwakutanisha na kutoa maamuzi katika kikao chao kilichofanyika jana.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani za klabu hiyo zinasema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa kamati hiyo kuliweka sawa benchi lake la ufundi kutokana na makocha hao kubwatukiana kwenye kikao kila mmoja akitaka kuwa juu ya mwenzie.
Chanzo cha habari ndani ya Simba kiliiambia MICHARAZO kuwa, licha ya majibizano yaliyoibuka kwenye kikao hicho, lakini mwishoe ilitolewa maamuzi kwamba Liewig ndiye anayepaswa kusikilizwa kama kocha mkuu na wasaidizi wake wakipaswa kumtii kwa manufaa ya klabu yao.
"Kikao kikubwa kizito kutokana na makocha hao kubwatukiana mbele yetu kabla ya kuwaweka sawa na kuwasuluhisha ambapo maamuzi yaliyofikiwa ni kwambna maamuzi yote katika timu yafanywe na kocha mkuu peke yake na wasaidizi ni kufuata baadaye ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima," chanzo kilisema.
Pia kikao hicho kiliamua kwa pamoja kwa kukubaliana na benchi lao la ufundi kuiingiza timu kambini huko Bamba Beach kwa ajili ya pambano lao la kesho dhidi ya Ruvu Shooting na kwa mechi nyingine zilizosalia kza Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni huku wenyewe wakiwa wameshatemesha ubingwa.
Makocha Mfaransa Patrick Liewig na Julio waliingia kwenye mzozo baina yao kutokana na kile kilichoelezwa kutofautiana na kusababisha kuigawa timu jambo lililohatarisha klabu yao ambayo ipo nafasi ya nne kwa sasa ikiwa na pointi zake 36 ikisaliwa na mechi tatu.

Bondia Star Boy ajifua kumkabili Jibaba Mei Mosi

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Shabani Mhamila 'Star Boy'  katika kambi ya Ilala iliyopo Amana CCM jana Sta Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' (kushoto) akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' mabondia wote wanajiandaa kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba .
Shabani Mhamila 'Star Boy'
Ibrahimu Class 'King Class Mawe akioneshana ujuzi wa kutupiana makonde na Shabani Mhamila 'Star Boy'
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Chalo Issa wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya ngumi Ilala Star Boy ana jiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba uatakaofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya ngumi Ilala Star Boy ana jiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba uatakaofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba .

BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' anaendelea kujifua kwa ajili ya 


kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na  Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa
bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya  kujiandaa kumchakaza Jibaba ili
kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta Boy mwenye rekodi ya kushinda 14 (KO 5) + kupoteza  7 (KO 4) + droo 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga  Theodor Luanda
Frebruary 2,1996 na kutetea vema
10 Februari 1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa 
Super D
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila,Japhet Kaseba,Hassani Matumla,Rashidi Matumla dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' pamoja na mabondia mabingwa wa dunia

Bayern Munich yaigagadua Barca 4-0 Ulaya


Wachezaji Beyern Munich wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Thomas Muller (aliyekunja ngumi hewani)

AIBU GANI HII: Ndivyo anavyoonyesha kusikitika nyota wa Barcelona, Lionel Messi baada ya Bayern Munich kuwapa kipigo cha mabaop 4-0.

LICHA ya kuwa na nyota wake karibu wote akiwamo 'Mchawi Mweupe', Lionel Messi, Barcelona ya Hispania usiku wa kuamkia leo imekiona cha moto ugenini baada ya kunyukwa mabao 4-0 na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich katika pambano la kwanza la Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ushindi huo mnono umeiweka katika nafasi nzuri Bayern kunusa Fainali ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana kucheza hatua hiyo na kuzimwa na Chelsea walioibuka mabingwa.
Bayern wanaofahamika zaidi kama 'Bavarians' wakiwa kwenye dimba lao la nyumbani la Allianz Arena, ilianza kuandikisha ushindi wao kwa bao la kuongoza lililoifungwa dakika ya 25 na Thomas Muller akimalizia kazi kubwa iliyofanywa na Dante.
Bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya Barcelona kucharuka kutakakulirejesha katika kipindi hicho cha kwanza.
Dakika nne baada ya kuanza kwa klipindi cha pili Bavarian waliongeza bao la pili kuputia kwa  Mario Gomez akimalizia pasi ya Thomas Muller aliyekuwa nyota wa mchezo huo wa jana.
Arjen Robben aliiongezea Bayern bao la tatu dakika ya 73 kabla ya Thomas Muller kuhitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne kwenye dakika ya 82 na kuzima ndoto za kiungo wa Barcelona aliyenukuliwa hivi karibuni akitamani fainali ya El Classico.
Ili Barcelona iweze kufua fainali hizo inapaswa kushinda mechi yake ya marudiano wiki ijayo kwa idadi isiyopungua mabao 5-0 kitu ambacho kinaonekana kuwa kigumu kwa namna Bayern walivyo katika kiwango kikubwa cha soka msimu huu chini ya kocha wao anayekaribia kuondoka klabuni hapo, Jupp Heynckes.
Michuano hiyo itaendelea tena leo kwa pambano la nusu fainali ya pili kati ya mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Ulaya, Real Madrid watakaokuwa wageni wa Borrusia Dortmund.
Timu zote hizo zinawania kucheza fainali hizo zitakazopigwa Mei 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Wembley baada ya msimu kadhaa ya kutofanikiwa kufika hatua hiyo.