STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 24, 2013

Bayern Munich yaigagadua Barca 4-0 Ulaya


Wachezaji Beyern Munich wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Thomas Muller (aliyekunja ngumi hewani)

AIBU GANI HII: Ndivyo anavyoonyesha kusikitika nyota wa Barcelona, Lionel Messi baada ya Bayern Munich kuwapa kipigo cha mabaop 4-0.

LICHA ya kuwa na nyota wake karibu wote akiwamo 'Mchawi Mweupe', Lionel Messi, Barcelona ya Hispania usiku wa kuamkia leo imekiona cha moto ugenini baada ya kunyukwa mabao 4-0 na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich katika pambano la kwanza la Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ushindi huo mnono umeiweka katika nafasi nzuri Bayern kunusa Fainali ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana kucheza hatua hiyo na kuzimwa na Chelsea walioibuka mabingwa.
Bayern wanaofahamika zaidi kama 'Bavarians' wakiwa kwenye dimba lao la nyumbani la Allianz Arena, ilianza kuandikisha ushindi wao kwa bao la kuongoza lililoifungwa dakika ya 25 na Thomas Muller akimalizia kazi kubwa iliyofanywa na Dante.
Bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya Barcelona kucharuka kutakakulirejesha katika kipindi hicho cha kwanza.
Dakika nne baada ya kuanza kwa klipindi cha pili Bavarian waliongeza bao la pili kuputia kwa  Mario Gomez akimalizia pasi ya Thomas Muller aliyekuwa nyota wa mchezo huo wa jana.
Arjen Robben aliiongezea Bayern bao la tatu dakika ya 73 kabla ya Thomas Muller kuhitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne kwenye dakika ya 82 na kuzima ndoto za kiungo wa Barcelona aliyenukuliwa hivi karibuni akitamani fainali ya El Classico.
Ili Barcelona iweze kufua fainali hizo inapaswa kushinda mechi yake ya marudiano wiki ijayo kwa idadi isiyopungua mabao 5-0 kitu ambacho kinaonekana kuwa kigumu kwa namna Bayern walivyo katika kiwango kikubwa cha soka msimu huu chini ya kocha wao anayekaribia kuondoka klabuni hapo, Jupp Heynckes.
Michuano hiyo itaendelea tena leo kwa pambano la nusu fainali ya pili kati ya mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Ulaya, Real Madrid watakaokuwa wageni wa Borrusia Dortmund.
Timu zote hizo zinawania kucheza fainali hizo zitakazopigwa Mei 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Wembley baada ya msimu kadhaa ya kutofanikiwa kufika hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment