Ruvu Shooting |
Simba wanaotaka kulinda heshima |
UONGOZI wa klabu ya soka ya Ruvu Shooting ya Pwani imeichimba mkwara Simba itakayovaana nayo kesho kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikitamba kuwa ni lazima 'mnyama' afe wakitaka kulinda heshima yao.
Akizungumza na MICHARAZO Afisa Habari wa klabu hiyo, Masau Bwire, kwamba mchezo huo kwao wanauchukulia kama fainali na hivyo watashuka dimbani kwa nia moja ya kusaka ushindi ili kudhihirisha kwamba wao ni bora kuliko wana Msimbazi.
"Tunahitaji kuutumia mchezo wa kesho (Alhamis) dhidi ya Simbaili kujenga heshima ya kisoka kwa timu yetu na kuwadhihirishia Watanzania kwambatimu yetu ni nzuri na ina vijana wenye vipaji na uwezo mkubwa wa soka, muhimu sheria 17 zizingatiwe," alisema Bwire.
Msemaji huyo alisema wanaiheshimu Simba kama klabu kongwe na timu yenye uwezo mkubwa kiuchumi na yenye kiu ya kutaka kulinda heshima yake angalau kuambulia nafasi ya tatu baada ya kulitema taji la ubingwa, lakini bado watashuka dimbani kwa dhamira moja tu ya kupata pointi tatu.
Bwire alisema kikosi chao kinachonolewa na kocha Charles Boniface Mkwara hawatakuwa tayari kuwa daraja la mafanikio ya Simba hiyo kesho na hivyo kuwaonya wanamsimbazi kwamba wakae chonjo na wasitarajie mteremko.
"Kocha katuhakikishia kwamba wachezaji wake wopte wapo vyema kwa ajili ya pambano hilo kitu ambacho kinatuma matumaini ya kuanya vyema mbele ya Simba," alisema Bwire.
Hata hivyo pambano hilo la kesho halitakuwa na maana yoyote kwa timu hizo kwani zote hazina matumaini ya ubingwa wala kupata nafasi ya uwakilishi wa mechi za kimataifa mwakani ambazo tayari zimeshachukuliw ana timu mbili za juu za Yanga na Azam.
No comments:
Post a Comment