STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 7, 2013

Wanafunzi wafa maji Tabora kisa Bata Mzinga


WANAFUNZI wawili wa shule ya msingi Itobo wilaya ya Nzega mkoani wa Tabora wamekufa maji katika bwawa wakati wakiwinda bata mzinga. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Peter Ouma alisema Massanja Shija (42) ambaye ni baba wa mmoja wa watoto hao waliokufa, amenusurika katika tukio hilo baada ya kunasa kwenye tope.

Kamanda alitaja watoto waliokufa ni Elias Massanja (13) na Shabani Ramadhan (15) wote wanafunzi wa darasa la sita shule ya Msingi Itobo. Tukio hilo ni la Julai 30 mwaka huu, saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Chamwabo, Kata Itobo.

Ouma alisema walikuwa wakiwinda bata mzinga ambaye aliruka na kwenda kwenye bwawa na katika kumfuata, walizama katika kina kirefu cha maji.

Alisema baada ya kuzama, jitihada za kuokoa miili yao ilikuwa ngumu kutokana na kukosa waokoaji. Hata hivyo baadaye iliopolewa.

Mbunge wa Jimbo la Bukene, Selemani Zedi alisema tukio hilo ni la kusikitisha kwa jamii. Aliwataka wananchi kuwa makini na mabwawa.

Shindano la BSS sasa TBC1 siyo ITV tena, kisa....!

 
Epiq Bongo Star Search ya mwaka 2013 haitaoneshwa tena kupitia ITV. Mwaka huu shindano hilo la kusaka vipaji vya kuimba litakuwa likioneshwa kupitia TBC1. 

Kupitia Facebook, Rita Paulsen aka Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na jaji mkuu wa shindano hilo ametoa sababu mbili za kuhamisha matangazo hayo kutoka ITV hadi TBC1.

“Baada ya kusoma maoni yenu, ningependa kufafanua sababu mbili za kurusha Epiq Bongo Star Search 2013 kupitia kituo cha Televisheni cha TBC1. 

Kwanza kabisa ni sababu za kibiashara ndio zimepelekea kipindi cha EBSS kurushwa kupitia TBC1 na sababu ya pili ni kwamba baada ya kwenda kidigitali, TBC1 sasa inapatikana kwenye ving’amuzi karibia vyote vikiwemo Star Times, DSTV na Zuku.

Extra Bongo yanasa wawili toka Congo kuwatambulisha siku ya Eid

 KATIKA kujiimarisha zaidi na kutaka kuendelea kufunika nchini bendi ya Extra Bongo 'Wana Next Level' maarufu kama Wazee wa Kizigo, wamewanyakua wanenguaji wapya wawili wa kike kutoka DR Congo watakaotambulishwa rasmi kwa mashabiki katika maonyesho ya sikukuu ya Eid el Fitri.
Wanenguaji hao walitambulishwa mchana wa leo kwa wanahabari ni Jolie Moncotina Kindu 'Mrinsho Ngassa' na Grace Messu Kamba (Fatuma) au maarufu kama John Bocco waliodai wanatoka katika makundi ya wanamuziki Werrason Ngiama Makanda na Ferre Golla.
Utambulisho huo ulifanyika kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki 'Kamarade' alisema wanenguaji hao tayari walioshaanza mazoezi na wasanii wenzao ila walikuwa wakisubiri vibali vya kufanya kazi nchini.
"Tumekuwa nao kwa muda wakiendelea na mazoezi wakati tukihangaikia vibali vyao na tunashukuru vibali vimepataika ana hivyo watawatambulishwa rasmi katika maonyesho yetu ya sikukuu ya Eid katika kumbi za Meeda Club-Sinza Mori na Dar Live," alisema Choki.
Aidha Choki alisema bendi yao pia itatambulisha siku hiyo kwa mashabiki wao nyimbo mbili mpya za 'Hafidh' uliotungwa na Michael Athanas 'Montanabe' na 'Mwanamke Hapigwi' Papii Catalogue.
"Pia kutakuwa na nyimbo mbili zitakazotambulishwa sambamba na zile mbili za Mgeni wa Khadija Kimobitel na Sagna nilioutunga mimi lakini anaimba sehemu kubwa Kimobitel," alisema.
Nao wanenguaji hao walioonyesha manjonjo yao kwa wanahabari, walisema wamekuja nchini kuonyesha namna ya kunengua, huku wakisema wanajiita majina ya washambuliaji hao nyota wa soka wa Taifa Stars kutokana na kukunwa na umahiri wao dimbani.
"Tangu niko kule Kin, namuonaga Murisho Ngassa namna anavyochezaga nami navutiwa na yeye ndiyo najipa hii jina yake, na nitafunika kama Ngassa," alisema Jolie ambaye angalau anakifahamu kiswahili kuliko mwenzake aliishia kusema yeye ni John Bocco tu.
Naye Rapa Catalogue alisema wimbo wake mpya una lengo la kuleta mabadiliko na utetezi kwa wanawake kutokana na mikstari yake inayoasa wanaume kutowapiga wanawake wala kuwanyanyasa badala yake iwatunze vyema ili wasije wakawaacha na kupata wanaojua kubembeleza.
"Pia kuna rapu mpya nitatitambulisha siku hiyo inayosema tutaishie Dar bila ya kazi, tutaishije Dar es Salaama bila ya kazi wakati taka, maji umeme na kila kitu lazima pesa..." alisema rapa huyo mahiri.
Kiongozi na mwalimu wa uenguaji wa bendi hiyo, Super Nyamwela alisema kutua kwa wasanii hao wawili kumeongeza chachu na kuboresha safu yao na kwamba hataki kusema mengi ila kuwataka mashabiki wajitokeze katika maonyesho yao waone kazi.
"Sitaki kusema sana kwa sababu hakuna asiyemjua Nyamwela na kazi yake, mimi ni mwalimu na mashabiki waje waone kwa nini anaitwa mwalimu, wenzetu wamezoea kuongea sasa ila mimi na bendi yangu ni watu wa vitendo zaidi," alisema Nyamwela.

Majambazi wamuua kwa risasi Mfanyabiashara wa madini Arusha

 
Mwili wa Erasto Msuya ukiwa chini baada ya kupigwa risasi.
 
MFANYABIASHA maarufu wa madini aina ya Tanzanite ambeye pia ni mmiliki wa hotel ya kitali ya S.G Resort ya jijini Arusha anayefahamika kwa jina la Erasto Msuya amefariki dunia leo majira ya alasiri baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wakati alipokuwa akitokea Mirerani akielekea jijini Arusha.
Taarifa kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo zinaeleza kuwa Bwana Erasto Msuya alisimamishwa na watu hao karibu na njia panda ya KIA (Kilimanjaro International Airport) na aliposimama walimtishia kwa kutumia bastola na kumtaka afate matakwa ya watu hao ndipo Erasto alipotoa bastola ili aweze kujitetea ndipo majambazi hao walipo amua kumpiga risia ambazo idadi yake haikuweza kufahamika kwa haraka.

NMB YASHIRIKI FUTARI NA WATEJA WAKE


 Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akishukuru uongozi wa NMB kwa kuandaa wasaa mzuri na kushiriki katika kukamilisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Hii ilikua katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB tawi la Zanzibar  kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean view Zanzibar mwishon mwa wiki.
  Mkuu wa kitengo cha akaunti binafsi wa NMB, Abdulmagid Nsekela akiongoza wageni waalikwa katika kupata futari.
  Meneja Mawasiliano NMB, Josephine Kulwa nae hakubakia nyuma kushiriki futari na wateja wa NMB
Maofisa wa NMB wakiwa wameambatana  kuingia ukumbini na mgeni rasmi (katikati) katika hafla hii ya kushiriki futari na wateja wa NMB mjini Zanzibar.

MKUTANO WA DHARURA WA WANACHAMA WA YANGA AGOST 18



1.   Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu (Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016


2.   Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani na Azam Media.


Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom Premier League katika Azam Television.


3.   Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani


Juu ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu zinazojionyesha wazi.


Inadhihirika wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.


Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.


Kwa kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.

AIRTEL YATOA CHAKULA CHA FUTARI NA IDDI KWA YATIMA DAR

 Afisa mauzo wa Airtel,  Bw Salehe Safi  akimkabidhi  Bibi  Saada Omary
moja ya zawadi zilizotolewa na kampuni za simu za mkononi  ya Airtel
kwenye kituo cha watoto yatima kinachofahamika kwa jina la Mwana
Orphanage Center kilichopo Vingunguti jijini Dar es salaam.   AIRTEL
ilitoa sukari, mchele, mafuta, sabuni, maziwa na Unga wa ngano
kwaajili ya kumalizia mwezi wa Ramadhani na kusheherekea sikukuu ya
IDDI.


Baadhi ya watoto yatima katika kituo cha Mwana Orphanage kilichopo
maeneo ya Vingunguti jijini Dar es salaam, wakiwa wameshikilia baadhi
ya zawadi walizokabidhiwa na kampuni ya simu za mkoni Airtel Tanzania.
AIRTEL ilitoa sukari, mchele, mafuta, sabuni, maziwa na Unga wa ngano
kwaajili ya kumalizia mwezi wa Ramadhani na kusheherekea sikukuu ya
IDDI.