Steven Gerrard akishangilia bao lake usiku wa jana |
Nahodha akionyesha maujuzi yake |
Fellaini akichuana na mchezaji wa Stoke City |
Nahodha huyo ambaye aliwekwa benchi katika mechi iliyopita dhidi ya Stoke City, alianzishwa katika pambano hilo la ugenini lililochezwa kwenye uwanja wa King Power dhidi ya 'vibonde' Leicester City na kufunga bao moja kati ya mabao matatu yaliyozidi kuifufua Liverpool katika ligi hiyo.
Wenyeji ambao walimaliza pambano hilo wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja kutokana na Wes Morgan kulimwa kadi nyekundu katika dakika ya 63, ndiyo wlaikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 22 baada ya kipa Simon Mignolet kujifunga kufuatia shuti la Leonardo Ulloa kugonga mwamba na katika harakati za kuokoa akajikuta akijifunga.
Hata hivyo dakika nne baadaye Adam Lalana aliisawazishia Liverpool bao hilo dakika nne baadaye kutokana na kushirikiana vyema na Ricky Lambert na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe sare ya 1-1.
Gerrard aliiandikia Liverpool bao la pili dakika ya 54 kabla ya Jordan Henderson kuongeza la tatu dakika ya 83 na kumfanya Kocha Branden Rodgers kupumua baada ya Liverpool kuchupa kutoka nafasi ya 11 hadi ya 8 ikiwa na pointi 20.
Katika mapambano mengine ya ligi hiyo yaliyochezwa juzi, Manchester United ikiwa uwanja wa Old Trafford walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stoke City, huku West Ham United ilitokana nyuma ugenini na kuichapa West Bromwich Albion mabao 2-1 katika pambano jingine.
Vijana wa Luis Van Gaal walipata mabao yao kupitia kwa Marouane Fellaine aliyemaliza pasi safi ya Ander Herrera katika dakika ya 21 na Juan Mata aliyefunga kwa mkwaju wa adhabu ndogo katika dakika ya 59, huku bao la wageni lilifungwa na Stephen N'Zonzi katika dakika ya 39.
Nao West Ham walipata ushindi wa mabao 2-1 ugenini baada ya kutanguliwa kufungwa, huku Burnley na Newcastle United zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, Swansea City ikiwa nyumbani ilitakata kwa kuichapa QPR kwa mabao 2-1 na Aston Villa kuiduwaza nyumbani Crystal Palace kwa kuinyuka bao 1-0.
Ligi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena usiku wa leo kwa michezo minne Arsenal itakuwa nyumbani kuwakabili
Southampton, vinara Chelsea wataialika Tottenham Hotspur, huku Everton na Hull City zikionyeshana umwamba na Sunderland kuwakabili Mabingwa watetezi Manchester City.
Vumbi jingine litaendelea Jumamosi kama hivi;
Newcastle United vs Chelsea
Hull City vs West Bromwich Albion
Liverpool vs Sunderland
QPR vs Burnley
Stoke City vs Arsenal
Tottenham Hotspur vs Crystal Palace
Manchester City vs Everton