STRIKA
USILIKOSE
Monday, March 2, 2015
El Merreikh yamfukuzisha kazi kocha wa Azam
MABINGWA wa soka nchini, Azam imemtimua kocha wake, Joseph Omog na msaidizi wake Ibrahim Shikanda na baadhi ya watendaji baada ya klabu hiyo kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor 'Father' ameweka bayana maamuzi hayo akisema imetokana na makubaliano waliyowekeana na Mcameroon huyo wakati wakiingia naye mkataba.
Father alisema kuwa, wakati wanaingia mkataba na Omog walikubaliana kuivusha mahali ilipo Azam ikiwamo kufanya vema kwenye michuano ya kimataifa, lakini kwa miaka miwili kocha huyo ameshindwa.
"Kwa hali hiyo tumeamua kuachana kwa wema na yeye mwenyewe analifahamu hilo, na hajatoka pekee yake bali na msaidizi namba mbili Ibrahim Shikanda na baadhi ya watendaji wa benchi la ufundi,"alisema.
Aliongeza kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha msaidizi kutoka Uganda, George Nsimbe ambaye atakaimua nafasi hiyo mpaka watakapopata kocha mkuu katika mchakato utakaoendeshwa na klabu yao.
GUINEA YAZIGOMEA CAF, FIFA AFCON 2023
WENYEJI
wa Fainali za Afrika za 2023, Guinea imeweka bayana kwamba hatakubali kuhamisha michuano hiyo toka mwanzoni mwa mwaka na kufanyika katikati ya mwaka kama FUIFA inavyotaka.
Wenyeji hao wamesema kuwahawakubaliani na fainali za Mataifa ya Afrika za
mwaka 2023 kuchezwa mwezi Juni ili kuziwezesha fainali za Kombe la Dunia
kufanyika Qatar, alisema waziri wao wa michezo.
Domani Dore alipingana
na taarifa ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) Jerome
Valcke, ambaye wiki iliyopita alisema kuwa, fainali za Mataifa ya Afrika 2023
zinatakuwa kusogezwa mbele kwa miezi sita hadi Juni kutoka katika muda wake wa
kawaida wa mwezi Januari.
Fainali za Kombe
la Dunia za mwaka 2022 zimepangwa kufanyika Novemba na Desemba, kufuatia
mapendekezo ya kamati ya maandalizi.
Valcke alisema
kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwezi mmoja baadae ni jambo lisilowezekana,
na aliongeza kuwa anakubaliana na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuhamisha
fainali hizo zinazoshirikisha jumla ya timu 16 baadae mwaka huo.
Hatahivyo, Guinea,
imesema kuwa itapinga tarehe hizo mpya.
"hatuwezi
kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika mwezi Juni, ni kipindi cha mvua, “’alisema
Dore alipozungunza na televisheni ya Guinea.
"Caf walitakiwa
kusikiliza ushauri wa Guinea kuwa kama sisi ni taifa tunatakiwa kuamua tarehe
gani zifanyike. Tunaelewa matatizo yanayolizunguka Kombe la dunia na kugongana
na fainali za Mataifa ya Afrika.
"Lakini Caf walitakiwa
kusikilisha maoni yetu. Mwezi juni , haiwezekani, " aliongeza Dore.
Shirikisho hilo la
Soka la Afrika limesisitiza kuhusu fainali Mataifa ya Afrika 2023 nchini Guinea,
likisema kuwa "Uamuzi kuhusu Afcon 2023 utatolewa na Kamati ya Utendaji ya
CAF, na sio mtu mwingine, wakati utakapofika."
MALI YAWEKA REKODI AFRIKA YATWAA UBINGWA U17
MALI imetawazwa
kuwa mabingwa wa Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya
kuifunga Afrika Kusini kwa bao 2-0 katika fainali iliyofanyika jijini hapa.
Mabao ya kipindi
cha pili yaliyowekwa kimiania na Siaka Bagayoko na Aly Malle yaliiwezesha Mali
kutwaa taji hilo.
Hii ni mara ya
kwanza katika historia ya Mali timu yake ya vijana inayojulikana kama Eaglets kushinda
taji la mashindano ya vijana.
Awali, nchi hiyo
ilikaribia kushinda taji mwaka 1997, wakati ilipomaliza ya pili nyuma ya washindi
Botswana.
Timu zote Mali na
Afrika Kusini zilienda katika fainali hiyo ya Jumapili zikiwa tayari zimewahi
kukutana katika hatua ya makundi ya mashindano hayo, wakati Afrika Kusini ikiwa
nyuma kwa bao 2-0 na kulazimisha sare ya 2-2.
Hatahivyo, Mali haikuruhusu
hilo utokea tena, na kuhakikisha inaweka ulinzi mkali baada ya kupata bao la
kuongoza na kuhakikisha inaibuka na ushindi.
Bao lao la kwanza
lilipatikana baada ya dakika 67 wakati Bagayoko alipofunga kwa kichwa mpira wa
kona.
The Eaglets waliongeza
bao la pili zikiwa zimebaki dakika 12 kufuatia juhudi binafsi ya Aly Malle.
Bao
hilo alilifunga kutoka umbali wa kama mita 20 kutoka nje ya boksi na kuibua
furaha kwa mashabiki wao.
Afrika Kusini
walifikiri wangeweza kupata bao la kufutia machozi wakati Khanyisa Eric Mayo alipokaribia
kufunga, lakini alijikuta akiwa ameotea.
Jose Mourinho ataka mataji zaidi Stanford Bridge
Mourinhio akilia kwa furaha |
Mourinho akikia kwa furaha baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa taji la kwanza msimu huu la Capital One |
Mabao yaliyofungwa na John Terry na lingine la kujifunga la Kyle Walker yalitosha kuipa ushindi wa mabao 2-0 Chelsea dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Wembley. Taji hilo linakuwa la 21 kwa Mourinho toka aanze kufundisha soka.
Akihojiwa Mourinho amesema anajiona kama mtoto aliyeshinda kwa mara ya kwanza kwani mara zote imekuwa ngumu kwake kuishi bila mataji.
Mourinho ambaye kwa mara ya kwanza amewahi kuinoa Chelsea mwaka 2004 hadi 2007 kabla ya kurejea tena mwaka 2013, hilo linakuwa taji lake la saba akiwa timu hiyo na pia kuisaidia Chelsea kulipa kisasi kwa Spurs ambao waliwatungua mabao 2-1 katika fainali za michuano hiyo zilifanyika mwaka 2008.
Kwa furaha kocha huyo alijikuta akimwaga chozi kabla ya baadaye kujumuika na wachezaji wake kushangilia mafanikio hayo yaliyokuja wakati Chelsea ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England na pia ikiwa kwenye hatuia nzuri ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
TAIFA STARS KUPASHA MISULI MOTO COSAFA CUP
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano
ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la
vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha runinga cha Supersport 4.
Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali, nchi nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.
Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.
Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros, Lesotho, Madagascar, Malawi, Maurtius, Mayotte, Msumbuji, Namibia, Reunion, Sychelles, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
Michuano ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha runinga cha Supersport 4.
Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali, nchi nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.
Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.
Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros, Lesotho, Madagascar, Malawi, Maurtius, Mayotte, Msumbuji, Namibia, Reunion, Sychelles, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
BASATA LAMLILIA CAPT JOHN KOMBA
Mwili wa Kapteni Komba ukiwasilia Karimjee mapema leo kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwao Lutuhi, Nyasa, wilayani Mbinga. |
Kapteni John Komba enzi za uhai wake katika picha tofauti akiwajibika katika sanaa yake ya uimbaji wa kwaya |
Na Rahim Junior
BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) limetuma salamu za rambirambi kumlilia Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba aliyefarikia wikiendi iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa yake BASATA imekielezea kifo cha Komba kama pigo kubwa katika tasnia ya sanaa.
Taarifa ya BASATA inasomeka hivi;
BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Captain John
Damian Komba kilichotokea jioni ya Jumamosi ya tarehe 28/02/2015.
Captain
John Damian Komba ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini.
Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na
kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.
Mchango
wake katika muziki wa dansi, kwaya na ule wa kiweledi katika kuandaa na kukuza
wasanii mbalimbali nchini hautasahaulika kamwe. Ni mdau aliyeacha alama kuu
katika muziki wa bendi, kwaya na taarabu na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika
kuufikisha muziki wa dansi na kwaya mahali ulipo leo.
Aidha,
pamoja na kujiunga na siasa na hatimaye kuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga
Magharibi, Mheshimiwa Komba hakukoma kuendelea kuipigania sekta ya Sanaa kwani
alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambayo kwa
mujibu wa kanuni za Bunge ndiyo inayoisimamia na kuishauri Serikali katika
masuala yote yahusuyo sekta ya Sanaa na Utamaduni.
Baraza,
wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia
marehemu John Komba hasa katika kutunga nyimbo za hamasa na ujumbe makini na
wenye mashiko kwa jamii yote ya Watanzania.
Hakika
pengo lililoachwa na Marehemu haliwezi kuzibika, kwani imekuwa ni kama mshumaa
uliyozimika ghafla wakati tukiingia kwenye giza.
Baraza
linatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne
Makinda, wabunge na wadau wote wa Sanaa hususan wasanii kwa msiba huu. Ni
matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu,
hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu ya Sanaa na taifa kwa ujumla.
Bwana ametoa na
Bwana ametwaa, Amen
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI
HII NDIYO NGOMA MPYA YA ALI KIBA-CHEKECHA CHEKETUA
Baada ya Mwana, Ali Kiba amekuja kivingine na Chekecha Cheketua ebu isikilize hapo chini; |
KICHUPA KIPYA CHA ZOLA D FT LATINHO.- I DON'T CARE.
Zola D King aliyeachia video ya wimbo wake wa I Don't Care |
Subscribe to:
Posts (Atom)