TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano
ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la
vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya
mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya
makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa
za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha runinga cha Supersport 4.
Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi
nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi
wataingia hatua ya robo fainali, nchi nyingine zitakazoanzia kwenye
makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles,
Swaziland.
Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila
kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali
itakayozijumuisha nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi,
Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na
nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.
Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama
kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha
nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros,
Lesotho, Madagascar, Malawi, Maurtius, Mayotte, Msumbuji, Namibia,
Reunion, Sychelles, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment