STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 2, 2015

Jose Mourinho ataka mataji zaidi Stanford Bridge


Mourinhio akilia kwa furaha
Mourinho akikia kwa furaha baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa taji la kwanza msimu huu la Capital One
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amedhamiria kutafuta mataji zaidi baada ya kunyakuwa taji la Kombe la Ligi  (Capital One) jana ikiwa ni la kwanza kwa kocha huyo toka achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo kwa mara ya pili.
Mabao yaliyofungwa na John Terry na lingine la kujifunga la Kyle Walker yalitosha kuipa ushindi wa mabao 2-0 Chelsea dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Wembley. Taji hilo linakuwa la 21 kwa Mourinho toka aanze kufundisha soka.
Akihojiwa Mourinho amesema anajiona kama mtoto aliyeshinda kwa mara ya kwanza kwani mara zote imekuwa ngumu kwake kuishi bila mataji.
Mourinho ambaye kwa mara ya kwanza amewahi kuinoa Chelsea mwaka 2004 hadi 2007 kabla ya kurejea tena mwaka 2013, hilo linakuwa taji lake la saba akiwa timu hiyo na pia kuisaidia Chelsea kulipa kisasi kwa Spurs ambao waliwatungua mabao 2-1 katika fainali za michuano hiyo zilifanyika mwaka 2008.
Kwa furaha kocha huyo alijikuta akimwaga chozi kabla ya baadaye kujumuika na wachezaji wake kushangilia mafanikio hayo yaliyokuja wakati Chelsea ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England na pia ikiwa kwenye hatuia nzuri ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment