MABINGWA watetezi wa Serie A ya nchini Italia, Juventus, imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya usiku huu kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Torino.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye mjini wa Turin, wenyeji walijikuta wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki waoStephan Lichtsteiner kulimwa kadi nyekundu kutokana na kupewa kadi ya pili ya njano.
Wenyeji hao walitangulia kuandika bao mapema kupitia kwa Arturo Vidal kwa mkwaju wa penati iliyotolewa na mwamuzi dakika ya 15 kabla ya wageni wao kurejesha bao hilo dakika saba baadae kupitia kwa Bruno Peres.
Wakati wengi wakidhani matokeo yangeisha kwa sare ya 1-1, kiungo mkongwe Andrea Pirlo aliifungia Juventus bao muhimu la ushindi dakika za lala salama na kuifanya 'Kibibi' cha Turin, kufikisha jumla ya pointi 34 kutokana na michezo 13.
MUda mchache ujao wanaoshikilia nafasi ya pili AS Roma wenye pointi 28 watakuwa nyumbani kuwakaribisha Inter Milan katika pambano linalotarajiwa kuwa kali.
STRIKA
USILIKOSE
Sunday, November 30, 2014
UWAJIBIKAJI! Polisi aliyeua kijana mweusi ajiuzulu!
Daren Wilson Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana
mweusi nchini Marekani amejiuzulu. Wakili wa Darren Wilson ambaye ni
afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mweusi Michael Brown
kwenye eneo la st Louis nchini Marekani mwezi Agosti anasema kuwa polisi
huyo amejiuzulu.
Mapema wiki hii bwana Wilson aliondolewa mashtaka hatua iliyozua
ghadhabu miongoni mwa waamerika weusi.Afisa huyo amekuwa likizoni tangu
mauji hayo yafanyike, mauaji ambayo yalisababisha majuma kadha ya
maandamano.
Michael Brown,kijana mweusi nchini Marekani alipigwa risasi na
kuuawa. Gazeti la St Louis limesema kuwa afisa huyo mwenye miaka 28
aliamua kujiuzulu baada ya kitengo chake cha polisi kupokea vitisho
kwamba ghasia zitafutia iwapo ataendelea kuhudumu kama mfanyikazi.
Gazeti hilo lilichapisha kile lilichodai kuwa barua yake ya kujiuzulu
ambayo ilisoma:''nimearifiwa kwamba iwapo nitaendelea kuwa mfanyikazi
wa idara ya Polisi basi hatua hiyo itawachochea maafisa wa polisi na
raia wa eneo la Furguson kuishi kwa hofu,hali ambayo siwezi kuikubali
hata kidogo.''
Spurs yainyoa Everton mabao 2-1
TIMU ya Tottenham Hotspur imetakata nyumbani baada ya kuinyoa Everton kwa mabao 2-1 katika pambano kali la Ligi Kuu ya England lililomalizika hivi punde.
Spurs iliyokuwa uwanja wa White Hartlane, ilishtushwa na wenyeji waliotangulia kuandika bao dakika ya 15 kupitia Kevin Mirallas kabla ya Christian Eriksen kusawazisha dakika ya 21 na Saldado aliongeza bao la pili dakika za nyongeza kabla ya mapumziko.
Kwa ushindi huo imeifanya Spurs kufikisha jumla ya pointi 20 sawa na wapinzani wao Arsenal isipokuwa wanakamata nafasi ya saba kwa tofauti na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena siku ya Jumanne kwa mechi sita ambapo Burnley itaikaribisha Newcastle United, Leicester itaialika Liverpool, huku Manchester United ikiikaribisha Stoke City na Swansea City ikiumna ana QPR, wakati Crystal Palace itaumana na Aston Villa na West Brom itapepetana na West Ham.
Jumatano kutapigwa mechi nne, Arsenal dhidi ya Southampton, Chelsea itailika Spurs, Everton itapepetana na Hull City na Sunderland itaialika watetezi Manchester City.
AC Milan yaifumua Udinese, Essien alimwa nyekundu
Michael Essien akiwa haamini kama kalimwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano |
Jeremy Menez akifunga bao la Ac Milan |
Milan ikiwa nyumbani hata hivyo kama ilivyokuwa kwa wageni wao, walijikuta wakipoteza mchezaji mmoja baadaya Michael Essien kulimwa kadi mbili za njano, dakika chache tangu Udinese wampoteze Domizzi kwa rafu aliyomchezea Kaisuyke Honda na kusababisha penati ilifungwa na Menez katika dakika ya 65.
Menez aliongeza bao la pili dakikia 10 baadaye akimalizia kazi nzuri ya Boneventura na kuifanya AC Milan kukwea hadi nafasi ya tano ikiwa na pointi 21.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Cagliari ikiwa nyumbani ilijikuta ikifumuliwa mabao 4-0 na Fiorentina nayo Cesena pia ililala nyumbani kwa mabao 3-0 na genoa huku Empoli na Atalanta zilitoshana nguvu kwa kutofungana na Palermo ikitakata nyumbani kwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Parma na hivi sasa watetezi Juventus wapo nyumbani ikiumana na Torino na mpaka sasa ikiwa ni mapumziko matokeo ni 1-1.
Shabiki afa, Atletico Madrid ikiilaza Deportivo la Coruna
SHABIKI mmoja wa soka amefariki dunia huko nchini Hispania kufuatia vurugu zilizotokea muda mfupi kabla ya mchezo kati ya Atletico Madrid na Deportivo La Coruna .
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alifariki dunia baada ya kupata shinikizo la damu wakati akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katikati ya vurugu zilizotokea kati ya mashabiki wa timu zote mbili.
Awali uongozi wa ligi ya Hispania ulijaribu kuahirisha mchezo huo lakini jaribio la kufanya hivyo lilizuiliwa na Shirikisho la soka la Hispania .
Vurugu kati ya mashabiki zilitokea saa tatu kabla ya mchezo kuanza ambapo mashabiki kadhaa waliumia wakiwemo watu 10 ambao walipata majeraha yaliyohitaji kuwahishwa hospitalini .
Viongozi wa juu wa klabu zote 20 za ligi kuu ya Hispania wametoa tamko la kukemea vurugu zilizotokea baina ya mashabiki wa Deportive na Atletico Madrid nab ado haiajfahamika kama kuna hatua zozote zitakazochukuliwa kwa timu hizo kufuatia vurugu zilizotokea .
Mchezo huo uliendelea kama kawaida ambapo Atletico Madrid walishinda 2-0 baada ya mabao yaliyofungwa na Saul Nigez na Arda Turan.
Katika mechi nyingine Sevilla ikiwa nyumbani iliikwangua Granada kwa mabao 5-1 kwa sasa timu za
Cordoba na Villarreal zipo dimbani na baadae Valencia itaikaribisha Barcelona.
Kaka 'amchana' Emmanuel Adebayor kumtuhumu mama yake kumroga
Sakata linaloendela kati ya mshambuliaji star wa Totenham Emmanuel Adebayor na mama yake mzazi anayefahamika kama Alice Adebayor limechukua sura nyingine baada ya ndugu wa mshambuliaji huyo kuingilia kati .
Ndugu huyo anayeitwa Kola Adebayor ambaye ni kaka wa Emmanuel amesema kuwa madai ya mshambuliaji huyo ya kusema kuwa mama yao mzazi amemroga si ya kweli.
Kola amesema kuwa kinachomfanya Adebayor kuamini kuwa mama yake amemfanyizia kwa waganga ili asiwe na bahati ni mawazo anayoyapata toka kwa watu wenye Imani ya dini ya kiislamu ambao wanamshauri vibaya nyota huyo .
Kola mwenye umri wa miaka 42 ambaye kazi ni dereva wa Malorry huko Ujerumani amesema kuwa amekerwa sana na kitendo cha mshambuliaji huyo kumuita mama yao mzazi mchawi kwani inaonyesha jinsi gani alivyokosa heshima kwa mzazi wake .
Kwa mujibu wa Kola , Adebayor aliwafuata watu wanaojiita watakatishaji wa nafasi ambao kwa lugha ya kiingereza huitwa Spiritual Cleansers ili wamsaidie kwa sababu mambo yake hayaendi vizuri na kwa mshangao mkubwa watu hao walimwambia kuwa mama yake mzazi na dada yake ndio chanzo cha mikosi inayompata .
Kola anaendelea kusema kuwa Adebayor alifuata ushauri wa watu hawa na kuwafukuza dada na mama yake kwenye nyumba aliyojenga huko Afrika na tangu siku hiyo amegoma kuwatumia fedha za kujikimu .
Kwa upande mwingine dada wa Emmanuel Adebayor anayeitwa Maggie ndio aliyefichua sakata hili huko Ghana wakati akizungumza moja kwa moja kwenye kipindi cha radio ambapo alisema kuwa mchezaji huyo amemfukuza mama yake na ametelekeza tangu siku hiyo .
Kola Adebayor anadai kuwa mama yao mzazi tangu siku aliyofukuzwa hadi leo hii amekuwa akilia kila siku hali ambayo inahatarisha afya yake .
Mshambuliaji huyo amekanusha sakata hilo akisema kuwa sio kweli kuwa amemfukuza mama yake bali mama huyo ameamua kuondoka yeye mwenyewe , Adebayor ameongeza kuwa hayuko kwenye mawasiliano mazuri na mama yake kwani amekuwa akisambaza maneno kwa watu kuwa mambo hayatamwendea vizuri .
Man City yaipiga Southampton 3-0
Yaya Toure akichuana na mchezaji wa Southampton |
Wachezaji wa City wakishangilia moja ya mabao yao lililofungwa na Lampard |
City, hata hivyo ilimaliza pambano hilo ikiwa pungufu kufuatia beki wake Eliaquim Mangala kulimwa kadi nyekundu baada ya kulimwa kadi mbili za njano.
Wageni walianza kuhesabu mabao yake katika dakika ya 51 baada ya kiungo Yaya Toure kuandika bao akimaliza kazi nzuri ya Sergio kun Aguero.
Bao la pili la City liliwekwa kimiania na mkongwe Frank Lampard dakiia ya 80 kabla ya dakika nane baadaye Gael Clichy kumaliza udhia kwa kuandika bao la tatu.
Ushindi huo umeifanya City kupanda hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 27, nane nyuma ya vinara Chelsea na wakiiporomosha Southampton waliokuwa wameng'ang'ania nafasi hiyo kwa muda mrefu ikiwa na pointi zake 26.
City itasafiri siku ya Jumanne kuifuata Sunderland ambayo jana iliikomaliza Chelsea na kutoka nao suluhu.
Ligi hiyo inaendelea tena muda huu kwa pambano jingine linalopigwa Uwanja wa White Hartlane kwa wenyeji Tottenham Hotspur wakiwa mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Everton.
Diamond aweka historia tuzo za Channel O
MSANII nyota wa muziki wa kizzi kipya nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' juzi Jumamosi aliweka historia baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo tatu za 'Channel O Music Video Awards' (CHOMVA-2014).
Diamond mshindi wa kihistoria wa tuzo za Kili Music Awards 2014 baada ya kunyaku tuzo saba kwa mpigo aliweka rekodi hiyo kwenye ukumbi wa Nasrec Expo Centre, nchini Afrika Kusini zilipotolewa tuzo hizo.
Staa huyo wa 'Nitampata Wapi', 'Mdogomdogo' na 'My Number One', alishinda tuzo tatu kati ya nne alizokuwa akiziwinda katika vipengele vya Most Gifted East, Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer.
Hii tuzo ya tatu ya kimataifa kwa Diamond kwa mwaka huu baada ya awali kunyakua tuzo ya AFRIMMA na Kora Music (ambayo hata hivyo mpaka sasa imekuwa na na utata).
Orodha kamili ya washindi wa tuzo hizo za Channel O ni kama ifuatavyo;
Most Gifted R&B video ni Crazy but Amazing-Donald, Most Gifted West Video
ni ‘Turn Up-Olamidem, Most Gifted Ragga/Dancehall ni Buffalo Soulja na The Most Gifted Kwaito akiwa ni Uhuru ft Oskido & Professor Kalawa -tjukutja.
Tuzo nyingi kama za Most Gifted East Video ni Diamond Platnumz, Most Gifted Dance Video ni Busiswa-Ngoku, Most Gifted Hip Hop Video ni AKA- Congratulate, Most Gifted Newcomer akiwa ni Diamond Platnumz tena.
Katika kipengele cha Most Gifted Male Video mshindi ni Casper Nyovest-Doc Shebeleza, Most Gifted Female Video alikuwa Tiwa Savage-Eminado, Most Gifted Afro Pop Video ni Mtanzania Diamond Platnumz, Most Gifted duo/group/featurning ni KCEE ft Wizkid-Pull Over na Most Gifted Video of the Year alikuwa ni Carsper Nyovest- Dos Shebeleza.
Subscribe to:
Posts (Atom)