STRIKA
USILIKOSE
Sunday, November 30, 2014
Kaka 'amchana' Emmanuel Adebayor kumtuhumu mama yake kumroga
Sakata linaloendela kati ya mshambuliaji star wa Totenham Emmanuel Adebayor na mama yake mzazi anayefahamika kama Alice Adebayor limechukua sura nyingine baada ya ndugu wa mshambuliaji huyo kuingilia kati .
Ndugu huyo anayeitwa Kola Adebayor ambaye ni kaka wa Emmanuel amesema kuwa madai ya mshambuliaji huyo ya kusema kuwa mama yao mzazi amemroga si ya kweli.
Kola amesema kuwa kinachomfanya Adebayor kuamini kuwa mama yake amemfanyizia kwa waganga ili asiwe na bahati ni mawazo anayoyapata toka kwa watu wenye Imani ya dini ya kiislamu ambao wanamshauri vibaya nyota huyo .
Kola mwenye umri wa miaka 42 ambaye kazi ni dereva wa Malorry huko Ujerumani amesema kuwa amekerwa sana na kitendo cha mshambuliaji huyo kumuita mama yao mzazi mchawi kwani inaonyesha jinsi gani alivyokosa heshima kwa mzazi wake .
Kwa mujibu wa Kola , Adebayor aliwafuata watu wanaojiita watakatishaji wa nafasi ambao kwa lugha ya kiingereza huitwa Spiritual Cleansers ili wamsaidie kwa sababu mambo yake hayaendi vizuri na kwa mshangao mkubwa watu hao walimwambia kuwa mama yake mzazi na dada yake ndio chanzo cha mikosi inayompata .
Kola anaendelea kusema kuwa Adebayor alifuata ushauri wa watu hawa na kuwafukuza dada na mama yake kwenye nyumba aliyojenga huko Afrika na tangu siku hiyo amegoma kuwatumia fedha za kujikimu .
Kwa upande mwingine dada wa Emmanuel Adebayor anayeitwa Maggie ndio aliyefichua sakata hili huko Ghana wakati akizungumza moja kwa moja kwenye kipindi cha radio ambapo alisema kuwa mchezaji huyo amemfukuza mama yake na ametelekeza tangu siku hiyo .
Kola Adebayor anadai kuwa mama yao mzazi tangu siku aliyofukuzwa hadi leo hii amekuwa akilia kila siku hali ambayo inahatarisha afya yake .
Mshambuliaji huyo amekanusha sakata hilo akisema kuwa sio kweli kuwa amemfukuza mama yake bali mama huyo ameamua kuondoka yeye mwenyewe , Adebayor ameongeza kuwa hayuko kwenye mawasiliano mazuri na mama yake kwani amekuwa akisambaza maneno kwa watu kuwa mambo hayatamwendea vizuri .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment