Wadhamini wa mbio hizo za magari za Juni 14 |
Na Seleman Msuya
KAMPUNI ya Busara Agro Machinery Tanzania imesema
itafungua mashindano ya mbio za magari za jijini Dar es Salaam kwa kutumia
magari yao ya Polaris Range RZR ili kuweza kuyatambulisha magari hayo hapa
Tanzania.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Mhandisi
Oded Kit wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi huyo alisema lengo lao ni kuhakikisha
kuwa magari hayo yanatambulika katika mashindano ambapo watakuwa wakifanya
maandalizi ya kushiriki mashindano mbalimbali ambayo yatakuwa yakiandaliwa hapa
nchini.
Alisema wameshashiriki katika mashindano yaliyopita
hivi karibuni ya Arusha Enduro ambapo pia walikuwa kama wafunguzi wa njia ya
mashindano lengo likiwa ni kutambulisha magari yao ambayo yamekuwa yakishiriki
mashindano ya kimataifa.
Mhandisi Kit alisema Polaris Range RZR ni magari
ambayo yanakimbia na imara hivyo wana uhakika kuwa yatafanya vizuri kwa siku za
karibuni.
Alisema kampuni yao imedhamiria kuwawezesha madereva
ambao wanahitaji kushiriki mashindano ambapo wametoa punguzo la asilimia 30% ya
bei ya magari hayo ambayo yanatoka nchini Marekani.
Kit alisema mashindano ya magari yanahitaji
maandalizi ya kutosha kuanzia dereva mwenyewe gari, na mahitaji mengine
kutokana na ukweli kuwa ni kazi ngumu na ya kuhatarisha maisha.
“Tumesikia kilio chao hivyo tunawaomba waje ili
waweze kupata magari imara kwa bei ndogo ambayo tumetoa punguzo la asilimia 30%
hivyo tunaamini mtu yoyote akitaka anaweza kununua”, alisema.
Kwa upande wake Fundi Mkuu wa Busara Agro Machinery
Denis Gastelleir alisema katika kuonyesha ubora wa magari yao wanatarajia kuwa
na magari matatu ambayo yatashiriki katika mashindano ya magari ya PUMA ambayo
yatafanyika kuanzia 14 hadi16 mwezi huu kwa kulometa 400 hapa jijini Dar es
Salaam.
Alisema magari hayo ambayo yanatokea nchini Marekani
yamekuwa yakishiriki katika mashindano mbalimbali kama Dakar Rally na mengine
mengi yanayofanyika hapa duniani.
Katika hatua nyingine Kampuni ya mafuta ya PUMA Tanzania imejitolea
kudhamini mashindano yam bio za magari zitakazofanyika
jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 14 hadi 16.
Hayo yamesemwa na Rais wa Chama Cha Magari Tanzania
Nizar Jivan wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema pamoja na kampuni hiyo ya mafuta ya PUMA pia
zipo kampuni zingine ambazo zimejitokeza kudhamini mashindano hayo ambayo
yatashirikisha madereva kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika.
Rais huyo alizitaja kampuni tanzu katika kudhamini
mashindano hayo kuwa ni pamoja na SUNVIC Express, D.B Shapriya , A TO Z, NIC,
CMC, Automobile Ltd, Knight Support, M/S Busara Agro Machinery, New Africa
Hotel, Monster Energy Drink, Hari Singh and Sons Ltd, Waljis Travel Bureau and
Tazara Reailway.
Jivan alisema hadi sasa ni madereva 25 ambao
wamethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ambapo 18 ni Watanzania na 7
wanatoka nje ya nchi ambapo amewataka madereva wengine wenye sifa wajitokeze
ila.
“Tarehe 14 hadi 16 tunatarajia kuwa na mashindano ya
kukimbiza magari ambayo yatakuwa ni ya kilometa 400 na yatafanyika hapa Dar es
Salaam ambapo tutatumia barabara mbalimbali tukianzia Tazara”, alisema.
Rais huyo alisema katika mashindano hayo kutakuwa na
magari mbalimbali kama Subaru Impreza R14, Mistubish Evolution X, Subaru Impreza
N12, Mistubishiu Evolution 8, Subaru Impreza MY04, Subaru Impreza MY03,
Mistubish Evolution IX, Subaru Impreza MY06, Subaru LEGACY, Mistubish Galant
VR4, Toyota CelicaGT-4, Mistubish EvolutionIV, Subaru Impreza GC8, Range Rover,
Toyota Land Cruser, VW Beetle, Nissan 240Z na Toyota Spinter.
Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya PUMA
ambao ndio wadhamini wa kuu wa mashindano hayo Philippe Consaletti alisema
wao wamejipanga kuendelea kudhamini mashindano hayo kama moja ya sehemu ya
faida yao ambayo wanaipata hapa nchini.
Consaletti alisema katika kutekeleza hilo
wanatarajia kudhamini mashindano ya mwaka ujao ambapo wameahidi kuwa
yatafanyika mkoani Arusha wakati ukifika.
Kwa upande wake Kamanda wa Usalama Barabarani
Kamishna Mohammed Mpinga amewahakikishia madereva na raia ambao watakuwa katika
maeneo ambayo magari yatapita kuwa usalama utakuwepo.
Mpinga aliwataka raia kuzingatia na kufuata
utaratibu ambao utakuwa unatumika ili kuepusha kero mbalimbali ambazo zinaweza
kutokea.