STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 6, 2013

IBF yampongeza Francis Cheka kutetea taji

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1652954/highRes/442095/-/maxw/600/-/j60c20z/-/bondia_cheka.jpg
SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) limempongeza bondia maarufu wa kitanzania Francis Cheka kwa juhudi zake za kuwa bondia mzuri mwenye viwango vya kimataifa katika uzito wa Super Middleweight.
Francis Cheka aliweza kutetea mkanda wake wa IBF Africa uzito wa Super Middle baada ya kumshinda kwa KO bondia Thomas Mashali aka “Simba asiyefugika” tarehe 1 Mei, 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
IBF inachukua fursa ya kumpongeza Francis Cheka baada ya ushindi huo ambao umedhihirisha kuwa yeye kweli ni bingwa wa bara la Afrika. Francis Cheka atarudiana na bondia wa Malawi Chimwemwe Chiotcha mwezi wa Agusti katika mpambano la kutetea mkanda wake.
Mpambano wao wa marudiano utafanyika katika jiji la Blantyre nchini Malawi na tayari majadiliano ya mpambano huo yanaendelea vizuri. Kampuni ya “Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi chini ya bwana Stephen Mawezni ndiyoitakayoandaa mpambano huo.
Pambano hili linakuja baada ya wadau kadhaa wa ngumi kuomba mabondia hao warudiane walipoonyesha ujuzi mkubwa na ushindani katika mpambano wao Desemba 26 mwaka jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeidi jijini Arusha siku ya Boxing Day.
Baada ya mpambano huo, IBF itampatia Francis Cheka nafasi ya kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF International Super Middleweight) na mabondia wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha kuwa Francis Cheka hana tena mpinzanai nchini Tanzania na kumpambanisha na mabondia wa kitanzania ni kumpotezea muda na uwezekano wake wa kutengeneza jina na pesa.
Wakati huo huo bondia Thomas Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle kwani mkanda wake haukuwa kati ya mikanda iliyogombewa kwenye mpambano uliomalizika Mei mosi.


Zola D naye atangaza kuwania ubunge 2015

Zola D katika pozi
MSANII nyota wa muziki wa Hip hop nchini, Michael Mlope 'Zola D' ametangaza nia yake ya kujitosa kwenye siasa ili awanie Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Zola D, aliiambia MICHARAZO kuwa, anataka kujitosa kwenye siasa ili kuendeleza harakati zake za kuwazindua na kuwakomboa wananchi kama afanyavyo kwenye fani ya muziki akiwa mmoja wa wanaharakati za kijamii.
Hata hivyo, Zola D ambaye pia ni mwanamasumbwi wa uzito wa juu nchini, hajaweka bayana atawania katika Jimbo gani kupitia chama kipi, licha ya kukiri kwamba atajitosa kwenye mkoa wa Dar es Salaam.
"Natarajia kuwania Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika moja ya majimbo ya jijini Dar es Salaam ila suala la chama na jimbo gani naomba niweke kwanza kwenye mabano mpaka muda muafaka ukifika," alisema Zola D.
Aliongeza kuwa, mpaka sasa vyama vitatu vikuu nchini vimekuwa vikimshawishi kujiunga nao, ingawa alisema chama atakachowani ni kile ambacho kina sera zinazotekelezeka na zitakazowanufaisha wananchi.
"Kiu yangu ni kuona wananchi wanyonge wakipata ukombozi wa kweli wa matatizo waliyonayo, maisha yamekuwa magumu na hakuna wa kuwaonea huruma hivyo nadhani kupitia chama chenye sera zinazotekelezeka naweza kuwasaidia kwani kabla ya kujitosa nimekuwa nikijitolea kwa jamii," alisema.
Kujitangaza kwa Zola D, kumekuja siku chache baada ya msanii mahiri wa filamu, Jacob Stephen 'JB' naye kuweka bayana kuwa atawania ubunge katika moja ya majimboi ya Dar es Salaam akifuata nyayo za Afande Sele aliyeweka bayana tangu mwaka jana na Karapina aliwahi kuwania udiwani Kinondoni.

Shaaban Dihile akiri Ligi Kuu msimu huu kiboko

Kipa Shaaban Dihile akiwa mazoezini na Taifa Stars
KIPA namba moja wa zamani wa Tanzania, Shaaban Dihile anayeidakia JKT Ruvu, amekiri Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012-2013 ulikuwa mgumu kupita kiasi na kushukuru kutoshukwa kwao daraja.
Dihile, alisema kwa hali waliyokuwa nayo msimu huu na ugumu wa ligi ulivyokuwa, anaona ni kama miujiza kwa kikosi chao kusalia kwenye ligi hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na MICHARAZO, Dihile aliyewahi kutamba na timu za Micco Villa, Everet ya Temeke, Dar Newala na Pan Afrika kabla ya kutua JKT mwaka 2005 alisema maandalizi yaliyofanywa na klabu zilizoshiriki ligi ya msimu huu ndiko kulikofanya ligi iwe ngumu na isiyotabirika kirahisi.
"Msimu huu ligi imekuwa ngumu na timu kutotabirika kwa klabu zilizofanya uzembe kwenye maandalizi yake zimejikuta kwenye wakati mgumu, ndiyo maana mpaka sasa siamini kama tumepoina kushuka daraja kutokana na hali tuliyokuwa nayo tangu tunaanza duru la kwanza mwaka jana," alisema Dihile.
Kipa huyo machachari ambaye msimu huu amekuwa akisumbuliwa na majeraha, alisema anaamini JKT watajipanga upya kwa msimu ujao ili warejee kwenye ligi ijayo wakiwa wapya na kuendeleza cheche zao.
Kuhusu kushindwa kufurukuta kwa wazawa msimu huu na kufunikwa na wageni, Dihile alisema ni kitu kinachotokea katika soka, japo alikiri kuyumba kwa wachezaji wa Kibongo kunachangia kufanya Stars nayo iyumbe kwa kukosa wachezaji wa kuaminika kikosi licha ya kuimwagia sifa kocha Kim Poulsen.
"Kung'ara kwa 'mapro' ni msiba wa kikosi cha Stars, kwani wachezaji wengine wanaotegemewa kwenye timu hiyo ni wale wanaotamba kwenye ligi, hata hivyo jambo la kuvutia ni kwamba Tanzania tumebahatika kuwa na kocha mzuri na mwenye kutambua kazi yake," alisema Dihile.
Katika orodha ya wafungaji mabao ya ligi hiyo inayomalizika Mei 18, kinara ni Kipre Tchetche, akifuatiwa kwa mbali na wachezaji kama akina Mcha Khamis Vialli, Paul Nonga, Hussein Javu, ambao wanabanana na akina Didier Kavumbagu, Haruna Niyonzima na Hamis Kiiza.

Thomas Mashali ataka kuzipiga tena na Francis Cheka

 
Cheka na Mashali walipopambana wiki iliyopita ukumbi wa PTA

BONDIA Thomas Mashali amekiri kwamba mpinzani wake Francis Cheka alimzidi ujanja na kumnyuka katika pambano lao la kuwania ubingwa wa IBF-Afrika, lakini akiapa ni lazima arudiane naye ili kulipiza kisasi.
Hata hivyo Cheka amejibu rai ya Mashali kwa kusema kuwa hawezi kurudiana na bondia huyo kwa madai imekuwa desturi kwa kila bondia anayepingwa naye kutaka kurudiana na kuendelea kuwanyuka, hivyo kiu yake ni kucheza na mabondia wa nje ya nchi.
Mashali alichezea kichapo na kusalimu amri katika raundi ya 10 kwa kupigwa KO katika pambano ambalo, Cheka alikuwa akitetea taji lake la IBF kwa mara ya tatu.
Bondia huyo aliyekuwa na rekodi ya kutopigika nchini, alisema anakubali Cheka alizimdi ujanja na kumtwanga, lakini haina maana yeye ni mbaya kwani ni kati ya mabondia wachache walioweza kukaribia kumaliza raundi zote kabla ya kuteleza raundi hiyo ya kumi.
"Nakubali kanizidi ujanja, Cheka ana nguvu mno na ndipo nilipokosea sikufikiria hilo, lakini kwa vile nimeshagundua makosa ninajipanga ili nirudiane naye tena mkoani Morogoro ili nilipize kisasi," alisema Mashali.
Cheka alipoulizwa juu ya tambo za Mashali, alisema hata kama atatokea promota wa kuandaa pambano hilo la pili hatakuwa radhi kupigana na Mashali kwa kuamini atampiga tu kama ilivyuotokea kwa mabondia wengine aliowadunda na kuomba kurudiana nao.
"Naona ni kupoteza muda, alitamba kabla ya kupigana nami kwamba yeye ndiye jibu la kuzuia vipigo kwa mabondia nchini mbele yangu, sasa nimempiga unadhani hata nikirudiana naye atafanya nini, itakuwa ni sawa na wenzake waliomtangulia, nataka kucheza mechi za kimataifa zaidi serikali inasaidie, nyumbani nimeshamaliza kazi," alisema Cheka.

Simba yampa presha King Kibadeni Tatu Bora Ligi Kuu Tanzania Bara

 
Kocha wa Kagera Sugar, King Abdallah Kibadeni

USHINDI wa mabao 3-1 iliyopata Simba jana kwenye pambano lao dhidi ya Ruvu Shooting, imewapa presha Kagera Sugar ambao wameenguliwa katika nafasi ya tatu waliyokuwa wanaishikilia mpaka jana.
Kocha wa Kagera Sugar, Abdallah Kibadeni, alisema ushindi wa Siomba umekuwa mwiba kwao kwa vile wanatishia ndoto zao za kuwepo kwenye Tatu Bora msimu huu.
Kagera wamelazimika kuwapisha Simba kutokana na kuzidiwa pointi mbili, Simba kwa ushindi wa jana imefikisha pointi 42, wakati Kagera wamesaliwa na zao 40.
Timu zote zimesaliwa na mechi mbilimbili kabla ya kufunga msimu, ambapo Kibadeni alisema watapigana kuhakikisha wanashinda zote, huku wakiiombea mabaya Wekundu wa Msimbazi.
"Kipigo cha Polisi na ushindi wa Simba jana umetuvurugia mipango yetu, lakini bado hatujakata tamaa na kumaliza katika Tatu BOra kwani tuna michezo miwili kama Simba, tutahakikisha tunashinda,:" alisema Kibadeni nyota wa zamani wa Simba, Majimaji Songea na Taifa Stars.
Katika mechi ya jana Wekundu wa Msimbazi, alipata ushindi kwa mabao ya Amri Kiemba aliyeanza kuifungia dakika ya 14 na kudumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili Ruvu walisawazisha dakika ya saba tu ya kuanza kipindi hicho kupitia kwa Abdulrahman Mussa kabla ya  Edward Christopher  na Ismail Mkoko kuiongezea Simba mabao mengine baadaye.
Kikosi cha Simba kitashuka dimbani tena keshokutwa kwa kuumana na Mgambo Shooting ya Tanga inayohitaji pointi moja tu kuzishusha rasmi daraja Toto African na Polisi Moro.
Timu hiyo ya Mgambo ndiyo inayoshikilia roho za timu hizo mbili ambazo zina uwezo wa kufikisha pointi 25 ambazo maafande hao wa Mgambo wanazo mkononi kwa sasa.

HII NDIYO ORODHA YA WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2012

Majina ya wanaowania kwa mwaka 2012:
MPIRA WA MAGONGO-WANAUME
1    Sylvester Kigodi
2.   Casto Mayuma
3.   Gurtej Bilu Singh
4.   Vendri Bhamra
5.  Elias Samala
Gofu ya Kulipwa 
1 Hassani Kadio 
   2 Yassin Salehe
  3 Fadhili Nkya
  4 Salimu Mwanyenza
  5 Rajabu Iddy
GOFU YA RIDHAA WANAWAKE:
1:MADINA IDDI
2:ANGEL EATON
3. HAWA WANYECHE
4.AYNE MAGOMBE
GOFU YA RIDHAA WANAUME
Jimmy Mollel
Frank Roman
Nuru Mollel
Martin MacDonald
John Said
NGUMI ZA RIDHAA-WANAUME
  1. Ismail Isack Galiatano
  2. Said Hofu
  3. Selemani Kidunda
  4. Victor Njaiti
  5. Mohamed Chibumbui
NGUMI ZA RIDHAA WANAWAKE:-
1.   Sara Andrew
2.   Irene Kimaro
3.   Easter Kimbe.
4.   Mather George
5.   Mariam Nyerere.
Ngumi za Kulipwa
1.      Francis Miyeyusho
2.     Ramadhan Shauri
3.     Thomas Mashali
4.     Said Mbelwa
5.     Francis Cheka
JUDO-TANZANIA BARA-WANAUME
1)     AHMED MAGOGO
2)    ADREW THOMAS MLUGU
3)    GEOPHREY EDWARD MTAWA
4)    GERVAS LEONARD CHILIPWELI
5)    ABUU SELEMANI MCHETEKO
6)   ABUUBAKAR NZIGE
JUDO TANZANIA BARA WANAWAKE
                             
1.     MATRIDA .H. TEMBA
2.     AMINA MOHAMED
JUDO ZANZIBAR-WANAUME
1.    MOHAMMED KHAMIS JUMA
2.   MASOUD AMOUR KOMBO
3.   MBAROUK SULEIMANI SULEIMAN
JUDO ZANZIBAR-WANAWAKE
1.     GRACE ALPHONCE
2.     LAYLATI MOHAMMED
TENISI-WANAWAKE
 [1] Rehema Athumani
[2] Vailety Petar
 [3] Mkunde iddi
 [4] Edna John
 [5] Zuhura Baraka
TENISI  Wanaume
 [1] Omary Abdalah
 [2] Yassini Shabani
 [3] Hassan Kasimu
 [4] Kiango Kipingu
 [5] Lebric Jacobu
MPIRA WA MIKONO-WANAUME
Faraji Shaibu
Nyuki ZANZIBAR
Hemedi Salehe
JKT
Abinery  Kusena
JKT
Ally Khamis
Ngome
Hassani  Yusufu
Magereza
MPIRA WA MIKONO-WANAWAKE
Catherine    Mapua
Ngome
Dorisi        Mangara
Magereza
Zakia        Mohamed
Ngome
Happy      Mahinya
JKT
Mary       Kimiti
Magereza
RIADHA-WANAWAKE
1.Zakia Mrisho
2. Mary Naali
 3.Jacklin Sakilu
4.Sarah Ramadhani  
 5.Anjelin Tsere
6. Sara Maja
RIADHA-WANAUME
1. Dickson Marwa
 2. Faustine Musa
3. Augstino Sule
4. Bazil John
5. Samson Ramadhan
KRIKETI-WANAUME
1.   Abhik Patwa.
2.     Benson Mwita.
3.     Sefu Khalifa.
4.     Issa Kikasi.
5.   Riziki Kiseto
KRIKETI-WANAWAKE
Monica Pascal.
Mwanaiddi Ibrahim.
Hadija Nasibu
Esther Wales
Mwanaidi Ammy
SOKA-WANAWAKE
FATUMA MUSTAPHA
ASHA RASHID
MWANAHAMISI OMARY
SOPHIA MWASIKILI
ESTER CHABRUMA
SOKA-WANAUME
JOHN BOCCO-AZAM
KELVIN YONDANI-YANGA
SHOMARI KAPOMBE-SIMBA
MCHA KHAMISI-AZAM
MBWANA SAMATTA-TP MAZEMBE
Thomas Ulimwengu-TP Mazembe
WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
EMMANUEL OKWI-SIMBA(SASA ETOILE DU SAHEL)-SOKA
KIPRE TCHETCHE-AZAM-SOKA
HARUNA NIYONZIMA-YANGA-SOKA
HAMISI KIIZA-YANGA-SOKA
MARY WAYA-FILBERT BAYI –NETIBOLI (ALIKUWA KOCHA MCHEZAJI)
KIKAPU-WANAWAKE
Faraja Malaki- Jeshi
Evodia Kazinja-JKT Stars
            Sajida Ahmed-Don Bosco
           Rehema Kilomba-Donbosco
        Tukusubira David-Vijana Queens
KIKAPU-WANAUME
Mussa Chacha-Savio
Lusajo Samuel Mwakipunda-Oilers
Salim Mchemba-ABC
Filbert Mwaipungu-ABC
Steven Atanasio-ABC
NETIBOLI
Lilian Sylidion-Filbert Bayi
Mwanaidi Hassan-JKT
Irene Elias Kanile-Filbert Bayi
Jacqueline Sikozi-Filbert Bayi
Faraja Malaki-Jeshi Stars
WACHEZAJI BORA CHIPUKIZI
Salum Abubakari-Azam-soka
Frank Domayo-Yanga-soka
Edward Cristopher-Simba-soka
Emmanuel Malya-Tenisi Gymkhana Arusha
Tambwe Juma-Kriketi
WATANZANIA WANAOCHEZA NJE
Mbwana Samatta-TP Mazembe
Ivo Mapunda-Gor Mahia
Hasheem Thabeet-Oklahoma
Thomas Ulimwengu-TP Mazembe
Soud Abdulrazak-Uganda (kikapu)
Mohammed Abdallah ‘dulah’-Uganda (kikapu)
TUZO YA HESHIMA--- ITATANGAZWA UKUMBINI
TUZO YA MWANAMICHEZO BORA MWAKA 2012- ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA MCHEZO
Imetolewa na
Haji Manara
Mwenyekiti Kamati ya Tuzo TASWA
05/05/2013

Azam warejea, Hall ajifariji

Azam Fc

WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Azam kilichokuwa kinashiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho kikirejea leo mchana kutoka Morocco, kocha wa timu hiyo, Stewart Hall amesema kwamba wachezaji wake walipambana kusaka ushindi wa ugenini lakini bahati haikuwa yao.
Azam iliyotoka suluhu katika mechi ya ya kwanza hapa nyumbani, juzi ilifungwa magoli 2-1 na AS FAR Rabat ya Morocco katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano hiyo na kutolewa.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Morocco jana mchana, Hall alisema kwamba wanaheshimu matokeo hayo na wanaamini kwamba mwakani wakipata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa watafanya vizuri zaidi ya msimu huu.
Hall alisema kwamba mchezo ulikuwa mgumu katika vipindi vyote na timu zote zilitengeneza nafasi lakini washambuliaji hawakuwa makini na kushindwa kutumia nafasi hizo.
"Tulipambana na tulijitahidi kuwakabili lakini matokeo hayakuwa mazuri katika upande wetu, ila wachezaji na mimi mwenyewe kuna mambo tumejifunza yatakayotusaidia kwa ligi ya nyumbani na mashindano mengine ya kimataifa tutakayoshiriki," alisema Muingereza huyo.
Afisa Habari wa timu hiyo, Jaffer Idd, alisema kuwa kikosi cha timu hiyo kitatua nchini saa 9:00 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates ambapo jana usiku walilala Dubai.
Alisema wachezaji na viongozi wote waliokuwa kwenye safari hiyo wako salama na wanarejea nchini na nguvu mpya kuhakikisha wanashinda mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zilizobaki.
Azam iliyoshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ilifika raundi ya pili baada ya kuzitoa Al Nasri ya Sudan Kusini na baadaye Barrack Young Controllers ya Liberia.
Chanzo: NIPASHE