STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 2, 2015

News Alert! Polisi Dar wanasa Panya wawili, yatoa hofu wakazi Dar

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWuSZq8hYuK9PCN1VrRQiyUvXtvljEAjuMAv3svwJWRxL-3XQwVyxUZlubZ41CcD93C401JPyYVoRTTb30RoQxxjonlkBoNwXZhZUDvLp1oypp_HowlFLw3ixI6eUKsEf9YfcftNzAgLsq/s1600/Kova1(30).jpg
Kamanda Kova
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewaondoa hofu wakazi wa jiji hilo juu ya kuzagaa kwa habari za uvamizi wa kundi la vijana wahuni la Panya Road, ingawa Kamanda wa Polisi Suleima Kova amekiri kutokea tukio hilo na vijana wawili wameshatiwa mbaroni mpaka sasa.
Akihojiwa muda mfupi na kituo cha TBC1, Kamanda Kova alisema kuwa usambazaji wa taarifa juu ya kundi hilo zimekuzwa sana na kuleta hofu kutokana na uvumi uliosambazwa na kuwataka wananchi wasiwe na hofu.
Kamanda Kova alisema jeshi la Polisi limedhibitiwa tangu walipoanzisha fujo zao na wawili walishatiwa mbaroni na sasa wanaendelea kuwataja wenzao ili kuwasaka walioibua taharuki hiyo.
"Uvumi huu wa kutumiana meseji na kutumia mitandao ya kijamii imeleta taharuki na kukuza jambo kinyume na uhalisia, lakini nataka kuwamabia wakazi wa Dar wasiwe na hofu jeshi la Polisi limewadhibiti na vijana wapo kazini kuhakikisha mambo yanaendelea kuwa shwari,'" alisema Kamanda Kova.
Tangu jioni kulikuwa na taarifa za kuwepo kwa matukio ya uporaji na uvamizi uliokuwa ukidaiwa kufanywa na Panya Road, ingawa DC wa KIinondoni, Jordan Rugimbana alifafanua mapema kabla ya Kamnada Kova kumaliza utata hivi punde. akisisitiza kuwa Dar ni shwari na watu walale kwa amani na utulivu kwa kuwa yeye Kamanda na vijana wake wapo kazini na Panya Road au wahalifu wengine hawawezi kuwazidi ujanja.

Yanga yafanya mauaji Mapinduzi Cup

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/IMG_0557-0.jpgPAMBANO la Kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Taifa Jang'ombe limeisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku Simon Msuva aliyeifungia mabao matatu akichaguliwa kuwa Man of the Match sambamba na kuondoka na mpira.
Bao jingine la nne liliwekewa kimiani na Kpeh Sean Sherman.

WACHEKI MASTAA WALIOCHEZA FILAMU YA WAKE UP

 
BAADHI ya Mastaa wa filamu Tanzania wakiwa katika pozi. Hao ni kati ya wakali walioshiriki filamu mpya ya Manaiki Sanga 'The Don' iitwayo Wake Up. Muongozaji wake, Leah Richard Mwendamseke 'Lamata' ameidokeza MICHARAZO kwamba filamu hii ni kama The Expendables iliyoshirikisha nyota mbalimbali wa filamu ulimwenguni.
 
Mzee Majuto akiwa kazini na wasanii wengine ndani ya Wake Up.

 
Mastaa nyota wa filamu nchini Irene Uwoya na Hemed Suleiman kama wanavyoonekana wakiigiza filamu hiyo ya Wake Up huko Mkoani Morogoro
 
Jackline Wolper vs Irine Uwoya ambao wamechuana vikali ndani ya filamu hiyo ya Wake Up ya msanii Manaiki Sanga " The Don"


 
Frola Mvungi na Mama Abdul wakiwa mzigoni kumalisha sehemu ya filamu hiyo ya kwanza nchini Tanzania kuchezeswa mastaa zaidi ya 30 pamoja haijawahi tokea
 
Wasanii Kajalia Masanja na mwenzake wakikamua ndani ya filamu ya Wake Up, ambapo kulikuwa na upinzani mkali sana wakati wa kuigiza ili kila mtu asionekane kucheza ndani ya kiwango.

Yanga waongoza Mapinduzi Cup, Simba kujiuliza kesho

Yanga X1HABARI kutoka Zanzibar kwa sasa kwenye mfululizo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi,, Yanga wapo mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Jang'ombe.
Mabao yote yakiwekwa kimiani na Winga, Simon Msuva.
Mapema leo mchana KMKM na Mtende zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu na Azam iliwabana mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda na kufungana nao mabao 2-2.
Kesho kutakuwa na mechi mbili za kundi A, Simba ikitarajiwa kurudia tena dimbani baada ya jana kulala bao 1-0 kwa Mtibwa Sugar.
Simba itavaana na Mafunzo, wakati JKU yenyewe itavaana na Wakata Miwa wa Mtibwa Sugar.

DC Kinondoni akanusha taarifa za Panya Road

https://24tanzania.com/wp-content/uploads/2013/02/a24aJordan-Rugimbana2.jpg
DC Rugimbana
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana amesema kuwa taarifa kuhusu uvamizi wa kundi la Panya Road ni uvumi tu.
Akizungumza moja kwa moja na Cloud's FM, Rugimbana amesema kuwa uvumi huo umetokea baada ya kundi la vijana hao kutoka kumzika mwenzao eneo la Magomeni Kagera na walipotaka kuanzisha fujo kabla ya kutawanywa na mabomu ya machozi.
"Hata mimi nimesikia taarifa hizo, lakini ni uvumi tu ambao unaweza kuleta taharuki, na hata hao wanaovumisha ukiwaluliza ukweli watakujibu wamesikia, ila tyukio hilo lilianza saa 10 wakati vijana hao walipokuwa wametoka kumzika mwenzao," alisema DC Rugimbana.
Hata hivyo wakati DC Rugimbana akinausha taarifa hizo mashuhuda wameeleza kuwashuhudia vijana hao, ingawa Dc amesisitiza kuwa RPC Suleiman Kova atatoa tamko

Chelsea waweweseka kipigo cha Spurs

http://www.tottenhamhotspur.com/uploadedImages/Shared_Assets/Images/News_images/SEASON_14-15/All_matches/First_team/Chelsea_H_Jan_1/chmc1.jpg?n=1826&targetTypeID=MatchdayGalleryKIPIGO cha mabao 5-3, kimeendelea kumuuma Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ambapo amenukuliwa akidai anaamini kikosi chake kingeweza kuichapa Tottenham Hotspurs kama wangezawadiwa penati ambayo ingewafanya kuongoza katika mchezo huo.
Baada ya Diego Costa kuifungia Chelsea bao la kuongoza, timu hiyo ilinyimwa penati na refa Phil Dowd wakati Jan Vertonghen aliposhika mpira katika eneo la hatari, na baadae kuja kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 5-3.
Mourinho alimlaumu mwamuzi huyo kwa kushindwa kutoa penati hiyo kwani ingewapa nafasi nzuri ya kushinda mchezo huo.
Hata hivyo baadhi wachambuzi wa soka wameshindwa kukubaliana na Mourinho wakidai kuwa haikustahili kuwa penati hivyo mwamuzi alikuwa sahihi.
Chelsea ambao walikuwa wakiongoza kwa tofauti ya alama nane katika msimamo wa Ligi Kuu Novemba mwaka jana sasa wako juu ya Manchester City kutokana na mpangilio wa herufi kufuatia kipigo hicho cha jana.
Ligi hiyo ya England itaendelea tena wiki ijayo baada ya wikiendi hii kuwa mapumziko kupisha michuano ya Kombe la FA.

Podolski awindwa Inter Milan

http://1nildown2oneup.net/wp-content/uploads/2013/12/LukasPodolskiMontpelliervArsenalpa_2830453.jpg
Lucas Podolski
OFA kutoka klabu ya Inter Milan imetua mezani mwa uongozi wa klabu ya Arsenal kwa ajili ya kumwinda, Lucas Podolski na klabu hiyo itafikiria ofa hiyo iliyoimarishwa.
Podolski, 29 ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal msimu huu huku akiukosa mchezo dhidi ya Southampton jana kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyonga.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ofa ya kwanza waliyotoa Inter ilikuwa ndogo hivyo kama wakirudi tena na fungu la kueleweka wataangalia uwezekano wa kufanya biashara.
Podolski alinunuliwa na Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 11 akitokea klabu ya Cologne mwaka 2012 lakini amefanikiwa kuanza kucheza mechi 39 pekee katika akiwa chini ya Wenger.
Mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao 31 katika mechi 82 alizoichezea Arsenal katika mashindano yote.
Pazia la dirisha dogo la usajili nchini England linatarajiwa kufunguliwa kesho Jumamosi na tayari tetesi zimeshaanza juu ya nani na nani anawindwa wapi. 

Breaking News! Panya Road waleta taharuki jijini Dar

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/05/mwitu_2.jpg
Picha ya Maktaba mmoja wa vijana wa kundi la Panya Road akiwa amepewa kipigo mapema mwaka jana walipofanya uvamizi kama huu
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mitaa kadhaa jijini Dar es Salaam 'kimenuka' baada ya kundi la vijana wahuni lifahamikalo kama 'Panya Road' limesambaa mitaani likipora na kufanya uhuni mwingine.
Mitaa ambayo inadaiwa kuvamiwa na kundi hilo linaloundwa na vijana zaidi ya 20 wakipora kwenye nyumba maduka na magari wakiwa na silaha ni Sinza, Magomeni, Tandale , Kinondoni na Mwananyamala.
Pia Tabata, Ubungo na Yombo inadaiwa vijana hao wameshika hatamu na kufanya vurugu, na kuleta taharuki kwa wakazi wa jijini, ingawa mpaka sasa jeshi la Polisi halijatoa taarifa zozote kuhusu matukio hayo.
Hata hivyo watu wlaioidokeza MICHARAZO wanasema kundi hiloi limeamua kuingia mitaani baada ya mmoja wao kuuwawa usiku wa kuamkia jana na ni kama wanalipa kisasi wakivamia na kujeruhi watu kwa silaha za jadi.
MICHARAZO inaendelea na juhudi za kusaka taarifa toka jeshi la polisi na juhudi wanazofanya kulizima kundi hilo ambalo linadaiwa ni kama limeteka jiji kwa sasa.

Vumbi la Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea bila vigogo

Kagera Sugar watakaoifuata Ruvu Shooting
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyEobPE20ZtNi1R-UopKnA1am4dMWYZsa7756AEyfSHcvOosRNMAP-efMmHJrvyF7Ow87HahcM35Mc0PHS1WKnJYrQVgpIPDUG7wM0AXLdLATZWM_FgJbvsrDo8w3YZiZ3RL3zmCrX9Dff/s640/DSC_0125.JPG
JKT Ruvu ambao watavaana na Coastal Union jijini Tanga

Ruvu Shooting

Prisons Mbeya watakaoikaribisha Ndabnda Fc Jumapili
Ndanda watakaojiuliza tena mjini Mbeya
KIPUTE cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuendelea wikiendi hii, bila kushuhudiwa vigogo, Simba, Yanga, Azam na Mtibwa Sugar ambazo zipo visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo kesho kutakuwa na michezo mitatu tu itakayozikutanisha timu za Coastal Union itaikaribisha JKT Ruvu kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Pambano jingine la kesho litazikutanisha timu za Ruvu Shooting watakaovaana na Kagera Sugar kwenye dimba la Mabatini, Mlandizi Pwani.
Mchezo wa mwingine utakaopigwa kesho Jumamosi ni Stand United itakayokuwa nyumbani mjini Shinyanga kuikaribisha Polisi Morogoro waliotoka kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo JKT ambao wapo likizo kwa vile mpinzani wake, Simba yupo Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015.
Ratiba hiyo hiyo ya ligi inaonyesha kuwa siku ya Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja tu utakaozikutanisha maafande wa  Prisons-Mbeya dhidi ya Ndanda ya Mtwara kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Msimamo wa ligi hiyo upo hivi;
                                           P   W    D    L    F   A   GD  Pts
 01. Mtibwa Sugar              08  04   04   00  11  04   07   16
02. Yanga                           08  04   02   02  11  07   04   14
03.  Azam                           08  04   02   02  10  06   04   14
04.  Kagera Sugar               08  03   04   01  07  04   03   13
05.  Coastal Union              08  03   03   02  09  07   02   12
06.  Polisi Moro                  08  03   03   02  08  07   01   12
06. JKT Ruvu                     08  03   01   04  07  08    -1   10
07. Ruvu Shooting              08  03   01   04  05  07    -2   10
08.Stand Utd                       08  02   04   02  06  10    -4   10
09.Simba                             08  01   06   01  07  07    00  09
09. Mgambo JKT                08  03   00   05  04  09    -5   09
12. Mbeya City                   08  02   02   04  03  06    -3   08
13. Prisons                          08   01   04  03   06  07    -1  07
14. Ndanda Fc                     08  02   00  06   08  13    -5  06
Wafungaji Bora:
5-
Didier Kavumbagu (Azam)
4-
Rama Salim (Coastal), Danny Mrwanda, Simon Msuva (Yanga) Ame Ally (Mtibwa), Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
3-
Ally Shomari, Emmanuel Okwi (Simba)

2- Shaaban Kisiga, (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Salum Kanoni (Kagera), Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Samuel Kamuntu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo),  Malimi Busungu (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi) 
Mechi za Ligi Kuu; Jan 03, 2014
Coastal Union vs  JKT Ruvu
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Azam vs Mtibwa Sugar (Imeahirishwa)
Stand United vs Polisi Moro
Mbeya City  vs  Yanga (Imeahirishwa)

Jan 4, 2015 
Mgambo JKT vs  Simba (Imeahirishwa) 
Prisons vs  Ndanda

Lampard awakera Wamarekani kuamua kubaki Manchester City

http://assets.nydailynews.com/polopoly_fs/1.1947373!/img/httpImage/image.jpg_gen/derivatives/article_970/lampard22s-1-web.jpg
Add caption

KITENDO cha kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya England, Frank Lampard ya kuongeza muda wa kuendelea kuichezea Manchester City kwa mkopo hadi mwisho wa msimu "umewachefua" mashabiki wa timu yake mama ya New York City FC inayoshiriki ligi kuu ya Marekani.
Lampard awali alijiunga na Man City kwa mkopo wa miezi sita akitokea New York City FC baada ya kuondoka Chelsea mwisho wa msimu uliopita.
Lakini dili lake na klabu hiyo ya England, ambayo kwa sasa ni ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, limeongezwa hadi Mei au Juni, jambo linalomaanisha kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 atakosa miezi mitatu ya kwanza ya msimu mpya wa ligi ya MLS.
"Tunapenda kupinga hadharani... maamuzi ya Frank Lampard kuongeza muda wake wa kucheza kwa mkopo Manchester City hadi mwisho wa msimu wa Ligi kuu ya England," umoja wa mashabiki wa New York City wajiitao 'Third Rail' ulisema katika taarifa yao.
"Mashabiki wengi, wakiwamo wanachama, wameamua kuisapoti timu,kununua tiketi za msimu, na kununua bidhaa za timu zikiwamo jezi kutokana na imani kwamba Frank Lampard ataichezea New York City Football Club, siyo Manchester City."
"Mashabiki wengi kati ya hao wamekerwa na maamuzi hayo, na tunasapoti hatua zozote watakazochukua katika kupinga maamuzi haya.
"Tunapinga mitazamo ya aina yoyote kwamba sisi NYCFC ni watoto wa Manchester City FC, bila ya kujali chanzo, na tumefadhaishwa na jumuiya ya City Football Group kuweka mtazamo huo."
New York City inamilikiwa kwa pamoja na klabu za Manchester City na timu ya baseball ya New York Yankees na itatumia Uwanja wa Yankee kama uwanja wake wa nyumbani wakati msimu wa 2015 wa ligi ya MLS utakapoanza Machi.
Lampard (36) ameifungia Man City magoli sita na tarehe ya kujiunga kwake New York City itategemea mechi ya mwisho ya Man City.
Ligi Kuu ya England itamalizika mwisho Mei 24, wakati mechi ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya itachezwa Juni 6. Manchester City itawavaa Barcelona katika mechi ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi ujao.

Chelsea, Arsenal zagongwa, Man City yaikamata Chelsea

Danny Rose akifunga bao la Spurs
Harry Kane hunts down Chelsea's Cahill as the central defender knocks the ball back towards his goalkeeper
Vita ya Chelsea na Spurs
Alexis Sanchez, played up front in the absence of Danny Welbeck and Olivier Giroud, tries to escape the attentions of Steven Davis 
Arsenal ilipokufa kwa watakatifu wa Southampton
Fabricio Coloccini rises above Danny Ings during the 3-3 draw at St James' Park on New Year's Day
Newcastle United walipolazimishwa sare ya 3-3 na Burnley
LIGI Kuu ya England (EPL) iliendelea usiku wa jana kwa kushuhudiwa vigogo vya ligi hiyo vikishindwa kutamba kwa vinara Chelsea ikinyukwa mabao 5-3 na Tottenham Hotspur.
Ukiachana pambano la mapema liliikutanisha Stoke City iliyoikaribisha Manchester United na kumalizika kwa sare ya 1-1, Arsenal walikumbana na kipigo toka kwa Southampton.
Chelsea wakiwa wageni wa Spurs uwanja wa White Hart Lane walipoteza mchezo huo kwa kunyukwa kwa mabao 5-3.
Mshambuliaji Diego Costa alitangulia kufunga bao la mapema katika dakika 18 baada ya kumalizia mpira wa shuti uliopigwa na Oscar na kugonga mwamba.
Spurs walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 30 mfungaji akiwa mshambuliaji kijana Harry Kane aliyefunga kwa shuti la umbali wa karibu mita 25 baada ya kumpita Oscar .
Spurs walipata bao la pili kupitia kwa beki wa kushoto Danny Rose ambaye alimalizia mpira wa Nacer Chadli uliogonga mwamba .
Winga Andros Townsend alifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki Gary Cahill kumchezea vibaya Danny Rose kabla ya Spurs walipata bao la nne kupitia kwa Harry Kane kabla ya kumalizia karamu kwa bao safi la Nacer Chadli.
Mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Eden Hazard na John Terry .
Mara ya mwisho kwa Chelsea kufungwa idadi kubwa ya mabao kwenye ligi kuu ya England  ilikuwa mwaka 1991 ambapo walifungwa na Nottingham Forest 7-0.
Arsenal wakiwa kwenye uwanja wa St Mary’s walikubali kipigo cha 2-0 mbele ya Southampton huku mabao yote mawili yakifungwa kutokana na makosa ya kizembe ya kipa Wojciech Szczesny.
Wafungaji wa Saints kwenye mchezo huo walikuwa Sadio Mane na Dusan Tadic .
Katika michezo mingine Manchester City walishinda  mchezo wao dhidi ya Sunderland kwa 3-2 , Liverpool  na Leicester City wakitoka sare ya 2-2  wakati Newcastle  na Burnley nao walifunga 3-3.
West Ham United na West Brom wakiendeleza mfululizo wa sare baada ya kufungana 1-1.
Kwa matokeo hayo yameifanya Chelsea kubaki kileleni  mwa msimamo lakini ikilingana kila kitu na Manchester City.
Timu zote zina pointi 46 wakifunga mabao 44 na kufungwa mabao 19.
MATOKEO YA EPL MWAKA MPYA HAYA HAPA
Stoke 1-1 Man Utd
Aston Villa 0-0 Crystal Palace
Hull City 2-0 Everton
Liverpool 2-2 Leicester City
Man City 3-2 Sunderland
Newcastle Utd 3-3 Burnley
QPR 1-1 Swansea City
Southampton 2-0 Arsenal
West Ham 1-1 West Brom
Tottenham 5-3 Chelsea

Bosi wa Wigan afungiwa kwa ubaguzi

http://cdn.images.express.co.uk/img/dynamic/67/590x/Dave-Whelan-538904.jpgMMILIKI wa klabu ya Wigan Athletic Dave Whelan amefungiwa kwa wiki sita kujishughulisha na masuala yeyote ya michezo na kutozwa faini ya paundi 50,000 kwa kutoa kauli ya kibaguzi kuwalenga watu wenye asili ya Uyahudi na Wachina. 
Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 78 ambaye amepewa wiki moja kukata rufani kuhusiana na adhabu hiyo pia ametakiwa kuhudhuria darasa la ushauri litakalokuwa likiendeshwa na Chama cha Soka cha Uingereza. 
Mwezi uliopita Whelan alikubali tuhuma hizo lakini alikataa kauli alizotoa wakati akihojiwa na gazeti moja kuwa za kibaguzi. 
Novemba mwaka huu Whelan alidai kuwa atajiuzulu kama akikutwa na hatia ya kuwa mbaguzi.

Simba bado gonjwa, yapigwa na Mtibwa Mapinduzi Cup

KIKOSI cha Simba kikiwa tayari na vita dhidi ya Mtibwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo Mnyama alikubali kipigo cha bao 1-0 lililowekwa kimiani na Nahodha wao wa zamani, Henry Joseph katika dakika ya 44. Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa Simba baada ya wiki iliyopita kupigwa baoa 1-0 na 'ndugu' wa Mtibwa, Kagera Sugar kartika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara. (Picha kwa hisani ya ZanziNews
Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar wakipasha moto misuli kabla ya kukaguliwa na Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo iliyoanza jana Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Kamisaa wa Mchezo huo Muhsin Kamara, wakati wa uzinduzi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi yaliozinduliwa leo na Balozi Seif, katika uwanja wa Amaan.    
Makamu wa Pili wa Rais wac Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaan usiku jana.
Makamu wa Pili wa Rais wac Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sigar,kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaan usiku wa jana
Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa ufunguzi uliofanyika uwanja wa Amaam. Timu ya Mtibwa imeshinda bao 1--0
Kikosi cha Simba kilichokubali kipigo cha bao 1-0 kwa mara ya pili mchezo wa mwanzo dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya msimu uliopita kunyukwa mabao 4-2.
Kikosi cha  timu ya Mtibwa Sugar kilichotoka kifua mbele dhidi ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Simba wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika usiku wa jana uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Simba, Nyange Kaburu alikuwa akishuhudia kipigo kando ya kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi.
KOcha mpya wa Simba, Goran Kapunovic akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba wakifuatilia mchezo huo wa jana
Makocha wa Yanga, Hans van der Pluijm na Boniface Mkwasa walikuwapo uwanjani

Yanga yamtosa Kaseja Kombe la Shirikisho Afrika

Kipa Juma Kaseja
Yanga
Azam
KLABU ya Yanga imemtosa rasmi kipa wao waliye kwenye mgogoro naye, Juma Kaseja baada ya kutolituma jina lake kwenye kikosi cha timu hiyo kwa ushiriki wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Jina la Kaseja si miongoni mwa wachezaji 24 waliopo kwenye orodha iliyotumwa ofisi za CAF kwa usajili wa michuano hiyo ambayo itakayoanza katikati ya mwaka huu kwa Yanga kuumana na BDF IX ya Botswana.
Kaseja amekuwa na mgogoro na klabu hiyo ya Jangwani kutokana na kutochezewa kwenye mechi za Ligi Kuu hivyo kuomba kupitia wakili wake kuachwa na timu hiyo, huku Yanga wakitangaza kuendelea kumkomalia kwa kuwa wana mkataba naye.
Wakati Yanga ikituma majina 24, nao mabingwa wa Tanzania Azam watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika wakianza kibarua chao kwa kuumana na El Merreikh imetuma pia idadi ya wachezaji kama hiyo kwa ajili ya ushiriki wa michuano hiyo watakayoicheza kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Kikosi cha Yanga kilichowasilishwa CAF kwa mujibu wa taarifa ambazo MICHARAZO inayo ni Makipa: Ally Mustafa 'Barthez' na Deogratius Munishi 'Dida', Mbuyu Twite, Juma Abdul, Nadir Haroub 'Cannavaro', Edward Charles, Kelvin Yondani, Salum Telela, Rajab Zahir, Andrey Coutinho na Haruna Niyonzima.
Wengine ni Said Juma, Hassan Dilunga,  Sherman Kpah, Jerson Tegete, Pato Ngonyani, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa, Alphonce Matogo, Amissi Tambwe, Hussein Javu, Said Juma,  Danny Mrwanda na Simon Msuva.
Kikosi cha Azam kilichopelekwa CAF ni; Mwadini Ali, Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Kelvin Friday, Salum Abubakar 'Sure Boy', Khalid Haji, Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu, David Mwantika, Aggrey Morris na Amri Kiemba.
Wengine ni Said Morad, Frank Domayo, John Bocco, Yahya Mudathir, Brian Majwega, Khamis Mcha, Himid Mao, Gaudence Mwaikimba, Waziri Salum, Aishi Manula na Wilfred Michael Bolou.