Semera |
Aisha Bui |
Semera aliiambia MICHARAZO kuwa alikuwa kimya akifanya shughuli nyingine za kiuchumi na sasa amerejea upya akiwa mbioni 'kuuza sura' kupitia kazi ambayo hata hivyo hakuitaja jina.
"Nilikuwa kimya kwa sababu ya kutingwa na majukumu mengi, sasa nimerejea upya na mashabiki wangu wasubiri kuniona katika kazi mpya itakayotoka mapema mwezi huu," alisema.
Kabla ya kutoweka mwanadada huyo alifanya vyema kwenye filamu za 'Mateka wa Kiroho', 'Mateso Kama Haya', 'Uyoga', 'Chozi' na nyingine.
Katika hatua nyingine muigizaji nyota, Aisha Bui aliyerejea nchini hivi karibuni baada ya kuwa Afrika Kusini kwa muda mrefu, amewataka mashabiki wa filamu kukaa tayari kumpokea akiwa amezaliwa upya.
Mwanadada huyo alisema anataka kuutumia mwaka 2014 kuwapa burudani mashabiki wake waliomkosa kwa muda mrefu akiwa nje ya Tanzania.
Wakati huo huo nyota wa muziki wa Hiphop, Emmanuel Elibariki 'Ney wa Mitego' ameacha video ya wimbo wake mpya uitwao 'Nakula Ujana'.
Video hiyo tayari imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kutokana na kutazamwa na wengi tangu ilipoachiwa hewani na staa huyo wa vibao kama 'Muziki Gani', Salamu Zao' na nyingine ilirekodiwa hivi karibuni jijini Nairobi.