STRIKA
USILIKOSE
Thursday, December 4, 2014
Mgendi aachia Wema ni Akiba, 'audio' albamu kabla ya X-mass
MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi ameachia wimbo mpya uitwao 'Wema ni Akiba' ikiwa ni utambulisho wa albamu yake mpya ijayo.
Tayari wimbo huo wa Mgendi umeanza kutamba kwenye vituo vya redio na katika mitandao ya kijamii baada ya kuuachia mapema wiki hii.
Akizungumza na MICHARAZO Mgendi alisema kuwa albamu yake ijayo itakuwa na nyimbo saba na ameutanguliza uliobeba jina kwa nia ya kuitambulisha kabla ya kuja kuiachia rasmi baadaye.
"Nimeachia wimbo wangu mpya ambao ni utambulisho wa albamu ijayo itakayofahamika kwa jina la 'Wema ni Akiba' itakayokuwa na nyimbo saba," alisema Mgendi.
Muimbaji huyo alizitaja baadahi ya nyimbo za albamu hiyo kuwa ni 'Wema ni Akiba', 'Usiniache Njiani', 'Nimempata Yesu', 'Nani Kama Mungu' na 'Kimbilia Msalabani'.
Albamu hiyo mpya imekuja wakati albamu ya msanii huyo iitwayo 'Hongera Yesu' ikiwa bado haijachuja sokoni ambayo aliiachia mapema mwaka huu.
Kuhusu video ya albamu hiyo, Mgendi, amesema ataanza zoezi la upigwaji picha za video Januari mwakani kabla ya albamu hiyo kuachiwa sokoni Juni, 2015.
Alisema uchukuaji wa video utahusisha nyimbo zote saba zitakazokuwa katika albamu hiyo inayokuja baada ya kutamba na 'Hongera Yesu'.
Jennifer alisema ataanza kurekodi video ya wimbo wa 'Wema ni Akiba' ambao tayari ameshauachia hewani ili kuitambulisha albamu hiyo ambayo ni ya nane kwake.
"Mchakato wa kurekodi video ya albamu yangu ijayo utaanza mapema Januari na nitaitoa rasmi Juni 2015, ila kwa sasa nimeachia 'audio' ili kuwapa ladha mpya ya Jennifer Mgendi," alisema muimbaji huyo ambaye pi ni muigizaji, mtayarishaji na muongozaji filamu.
jennifer alifafanua kuwa 'audio' albamu ya Wema ni Akiba itaachiwa ndani ya mwezi huu kabla ya Sikukuu ya Xmass.
"Audio albamu ya Wema ni Akiba nitaiachia sokoni kabla uya Krismasi ila video yake ndiyo itatoka Juni baada ya kuanza kurekodi mwezi ujao," alisema Jennifer.
Jennifer ambaye kitaaluma ni mwalimu, alianza kutamba kwenye muziki wa Injili mwaka 1995 akitoa albamu saba sambamba na filamu zilizomjengea jina kubwa miongoni mwa wasanii wa kike nchini.
Sami Khadira atolewa hospitalini, majaliwa yake bado...!
KIUNGO nyota wa klabu ya Real
Madrid, Sami Khedira ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kulazwa kwa
siku moja kwa uangalizi kutokana na mtikisiko katika ubongo wakati
wa mchezo wa Kombe la Mfalme dhidi ya Cornella.
Khedira aligongana na kiungo wa Cornella David Garcia muda mfupi baada ya mapumziko katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu kabla ya kucheza kwa dakika chache na baadae kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Jese.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, Khedira alifanyiwa vipimo zaidi jana na kuruhusiwa lakini haijajulikana na muda gani atakaa nje ya uwanja.
Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo walitinga hatua ya timu 32 bora bada ya kushinda mchezo wao wa mkondo wa pili kwa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo ya daraja la tatu hivyo kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 9-1.
Madrid sasa inakabiliwa na mchezo mwingine wa La Liga Jumamosi hii dhidi ya Celta Vigo huku wakiwa na matumaini ya kushinda na kuendelea pengo lao la alama mbili dhidi ya mahasimu wao Barcelona.
Make Money at : http://bi
Khedira aligongana na kiungo wa Cornella David Garcia muda mfupi baada ya mapumziko katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu kabla ya kucheza kwa dakika chache na baadae kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Jese.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, Khedira alifanyiwa vipimo zaidi jana na kuruhusiwa lakini haijajulikana na muda gani atakaa nje ya uwanja.
Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo walitinga hatua ya timu 32 bora bada ya kushinda mchezo wao wa mkondo wa pili kwa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo ya daraja la tatu hivyo kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 9-1.
Madrid sasa inakabiliwa na mchezo mwingine wa La Liga Jumamosi hii dhidi ya Celta Vigo huku wakiwa na matumaini ya kushinda na kuendelea pengo lao la alama mbili dhidi ya mahasimu wao Barcelona.
Make Money at : http://bi
Dokii Hakuna Kama Mwanamke videoni
MSANII Ummy Wenceslaus 'Dokii' ameachia video ya wimbo wake mpya wa 'Hakuna Kama Mwanamke' huku akianza mchakato wa kutengenezea video ya wimbo wake mwingine uitwao 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
Akizungumza na MICHARAZO, Dokii alisema video yake mpya imetengenezwa na Pablo ambaye pia ndiye aliyepewa jukumu la kuitengeneza video ya wimbo wa 'Nampenda Dereva wa Bodaboda'.
"Tayari nimeshaiachia video ya wimbo wangu wa 'Hakuna Kama Mwanamke' ambao 'audio' yake imetengenezwa studuio za Recho Records chini ya mtayarishaji aitwaye Shivo," alisema Dokii.
Alisema wimbo wake wa Nampenda Dereva wa Boda Boda' uliotengenezwa Akhenato Records chini ya Lil Ghetto, utaanza kurekodiwa video yake wiki ijayo kabla ya kuachiwa hewani.
"Video hiyo nayo itatengenezwa na Pablo, hivyo mashabiki wangu wajiandae kushuhudia kazi hiyo mapema kabla ya kumalizika kwa mwezi huu," alisema Dokii.
Muigizaji na mwanamitindo huyo alisema, ameamua kutoa kazi hizo mfululizo kuthibitisha alivyoelekeza nguvu zake katika fani ya muziki akiipa kisogo kwa muda kazi ya uigizaji filamu.
Hatari! Cameroon, Ivory Coast kundi moja AFCON 2015
SHIRIKISHO la Soka Afrika, CAF, imetangaza droo ya makundi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea kwa kuziweka kundi moja timu za Ghana, Algeria, Afrika Kusini na Senegal.
Kwa mujibu wa droo iliyofanywa usiku wa jana, timu hizo zimewekwa kundi moja la C ambalo ni la kifo kama lilivyo kundi D lenye timu za Ivory Coast, majirani za Cameroon, Guinea na Mali.
Makundi mengine mawili ya A na B yanaonekana siyo ya kutisha ingawa timu zote 16 zitakazochuana kwenye fainali hizo za mwakani zinapewa nafasi sawa ya kutwaa ubingwa huo ambao hauna mwenyewe baada ya Nigeria kuvuliwa hatua ya makundi.
Katika Kundi A zimepangwa timu wenyeji Equatorial Guinea sambamba na Burkina Faso, Gabon na Congo, huku Kundi B likiwa na timu za zambia, Tunias, Cape Verde na DR Congo.
Fainali hizo zinatarajiwa kuanza kuchezwa Januari 17 na kufikia tamati kwa bingwa kufahamika Februari 8.
Subscribe to:
Posts (Atom)