HAWAAMINI KAMA WAMETUNGULIWA! |
Hata Bale alishindwa kuibeba Real Madrid leo kwa Athletic Bilbao |
Bao pekee lililowazamisha Mabingwa wa Ulaya, liliwekwa kimiani kwa kichwa na Aduriz katika dakika ya 26 akimalizia kazi nzuri ya Mikel Rico.
Madrid ilikuwa na wakali wake wote akiwamo Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Karim Benzema, Isco, Ton Kroos na wengine ilishindwa kabisa kufuruka kwa wenyeji na kukubali kichapo hicho kilichowafanya wasaliwe na pointi zao 61 na kutoa nafasi kwa wapinzani wao wakuu Barcelona kuwapiku kama watashinda katika mechi yao ya kesho. Barcelona wana pointi 59,wakiwa wana mchezo mmoja pungufu zaidi ya Real Madrid.
Katika mchezo mwingine wa mapema, Deportivo la Coruna wakiwa nyumbani walizamishwa mabao 4-3 na Sevilla, huku kwa sasa pambano la ligi hiyo Elche ikiwa nyumbani inaongoza bao 1-0 dhidi ya Almeria na baadae Granada itaikaribisha Malaga.