STRIKA
USILIKOSE
Monday, February 23, 2015
Irene Uwoya aibarishia Kisoda kufunika 2015
Irene Uwoya |
Akizungumza na MICHARAZO, Irene anayefahamika kama 'Oprah' au Mama Krish, alisema kuwa kwa namna filamu hiyo ilivyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu ya kushirikisha nyota mbalimbali wa Tanzania na wale wa kimataifa ana imani ya kufunika 2015.
Irene alisema ingawa siyo vema kuanza kujisifia kabla hata filamu hiyo haijainguia sokoni, lakini anawataka mashabiki wake kuisubiri kuipokea kabla ya Pasaka kuweza kuthibitisha maelezo yake.
"Huwa sina utamaduni wa kupenda kujifagilia, lakini mashabiki wangu waisubiri 'Kisoda' waone utofauti, naamini itafunika kuliko hata 'Apple'," alisema Irene ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Apple Film Production.
Irene alisema kuna mambo yaliyokwamisha filamu hiyo kutoka mapema kama alivyokuwa amepanga, lakini mara baada ya kuhaririwa itaachiwa na kufanyiwa uzinduzi wake kabla ya Pasaka inayotarajiwa kuadhimishwa mwanzoni mwa Aprili.
Twiga Stars waingia kambini kujiwinda kimataifa
Kocha wa Twiga Stars |
Baadhi ya nyota wa Twiga Stars walioitwa kambini |
Kaijage ametangaza programu yake ya mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa awali.
Twiga Stars ambayo imeingia kambini jana Jumapili na itakuwa kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume, imefuzu moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji walioitwa na kuingia kambini ni pamoja na Asha Rashid 'Mwalala', Esther Chaburuma 'Lunyamila', Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph, Dawa Haji Vuai, Belina Julius na Amina Ramadhani.
Mwili wa Mez B kuzikwa leo mjini Dodoma
MWILI wa msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Moses Bushagama maarufu kama Mez B aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita wakati akikimbizwa hospitalini unatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Wahanga wa Treni yaliyopo Mailimbili mjini Dodoma.
Taarifa
iliyotolewa na mama yake Mez B, Merry
Katambi alisema shughuli ya kumuaga
mwanae itafanyika Viwanja vya Nyerere Square Mjini hapa.
Mazishi hayo
kwenye viwanja vya Nyerere yataambatana na ibada ya kumuombea na yanatarajiwa
kuanza saa saba mchana.
"Mwanangu tutamzika Jumatatu (leo) katika
Makaburi ya wahanga wa Treni Mailimbili ila ibada pamoja na kuuga mwili wa
marehemu zitafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere’’
Mez B
alikuwa ni mwanzilishi wa kundi la Chemba Squard ambapo alikuwa pamoja na Dar
Master, Noorah na Albert Mangwea huku akitamba na nyimbo za 'Kikuku cha Mama
Rhoda', 'Nimekubali' na 'Kama Vipi iliyomjengea jina kubwa kwa mashabiki wa muziki kabla ya 'kuzimika'.
Mourinho 'alianzisha' tena England, kisa sare na Burnley
KOCHA Jose Mourinho wa klabu ya Chelsea, ameanzisha tena vita ya maneno na chama cha soka England, FA kufuatia kudai kuwa kampeni dhidi yake ya kuhakikisha hachukui ubingwa msimu huu inaendelea na kweli itawagharimu klabu yake.
Mourinho ameyasema hayo baada ya kutoka sare ya 1-1 na Burnley kwenye uwanja wa nyumbani wa Stamford Bridge ambapo amelaumu maamuzi ya mwamuzi Martin Alkinson.
Alkinson alimuonesha kadi nyekundu kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic na atakosa mechi ya jumamosi ya fainali ya kombe la ligi dhidi ya Tottenham baada ya kadi nyekundu ya dakika ya 69.
Mourinho anadai Ashley Barnes alitakiwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Martic na kulikosababisha kiungo wake amsukume mshambuliaji huyo wa Burnley na kuambulia kadi nyekundu.
Pia alitakiwa kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kitendo cha kumsukuma Branislav Ivanovic.
Mourinho anaamini haki haikutendeka ambapo walinyimwa penalti mbili kwani Michael Kightly aliunawa mpira wa shuti la Ivanovic katika dakika ya 33′ na nahodha wa Burnley Jason Shackell alimsukuma Diego Costa eneo la hatari dakika chache kabla ya mapumziko.
Chelsesa bao ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 60, wajkifuatiwa kwa mbali na Manchester City ambao walitoa kipigo cha 'Paka Mwizi' kwa Newcastle United kwa kuizabua mabao 5-0 na kufikisha pointi 55.

Kocha Southampton kumuadhibu Sadio Mane, kisa...!
Sadio Mane akichuana na Coutinho katika mechi yao ya jana dhidi uya Liverpool na kulala nyumbani 2-0 |
Mane alikuwepo katika kikosi kilichowakabili wakali wa Merseyside kwa kufika baada ya nusu saa kupita kutoka muda waliopanga kufika, saa saba mchana.
Pia mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal anakabiliwa na adhabu nyingine ya kutozingatia muda.
“Alichelewa kwa dakika 25-30 kabla ya mechi”, amethibitisha Koeman.
“Tuna kanuni na maelekezo kwa wachezaji. Kila mtu anaweza kuchelewa siku moja asubuhi, lakini huwezi kuchelewa kufika saa saba wakati unacheza dhidi ya Liverpool.
“Hakutoa maelezo? Maelezo hayo ni baina ya kocha na mchezaji, lakini alichelewa.
‘Siwezi na sikubaliani na hilo. Kama ni kulipa faini alipe tu”
Mdudu wa sare ahamia Azam, yabanwa na Prisons
Azam waliolazimishwa sare isiyo na mabao na Prisons-Mbeya |
Sare hiyo ya pili mfululizzo kwa Azam imetoa nafasi kwa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kutanua pengo lake la uongozi hadi kuwa pointi nne licha ya timu zote mbili kucheza mechi 15 kila mmoja.
Yanga inaoongoza ikiwa na pointi 31 baada ya kuvuna pointi 6 jijini Mbeya kwa kuzichapa Prisons na Mbeya City kwa mabao 3-0 na 3-1, wakati Azam kwa kupoteza pointi nne wamekusanya pointi 27.
Pambano hilo la Azam an Prisons lilichezwa usiku kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi na sare hiyo isiyo na mabao imewapa afueni maafande wa Prisons waliofikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi 15.
Subscribe to:
Posts (Atom)