MWILI wa msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Moses Bushagama maarufu kama Mez B aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita wakati akikimbizwa hospitalini unatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Wahanga wa Treni yaliyopo Mailimbili mjini Dodoma.
Taarifa
iliyotolewa na mama yake Mez B, Merry
Katambi alisema shughuli ya kumuaga
mwanae itafanyika Viwanja vya Nyerere Square Mjini hapa.
Mazishi hayo
kwenye viwanja vya Nyerere yataambatana na ibada ya kumuombea na yanatarajiwa
kuanza saa saba mchana.
"Mwanangu tutamzika Jumatatu (leo) katika
Makaburi ya wahanga wa Treni Mailimbili ila ibada pamoja na kuuga mwili wa
marehemu zitafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere’’
Mez B
alikuwa ni mwanzilishi wa kundi la Chemba Squard ambapo alikuwa pamoja na Dar
Master, Noorah na Albert Mangwea huku akitamba na nyimbo za 'Kikuku cha Mama
Rhoda', 'Nimekubali' na 'Kama Vipi iliyomjengea jina kubwa kwa mashabiki wa muziki kabla ya 'kuzimika'.
No comments:
Post a Comment