|
Rais Jakaye Kikwete akizungumza jioni ya leo |
|
Prof Tibaijuka aliyetenguliwa uteuzi wake kisa fedha za James Rugemalila |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete amevunja ukimya leo wakati akizungumza na Wazee wa jiji la Da es Salaam na kugusia baadhi ya mambop ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania likiwamo Sakata la akaunti ya Tegeta ESCROW.
Katika hutoba yake ya zaidi ya saa 2 Rais Kikkwete aliweka bayana juu ya kumfuta kazi Prof, Anna Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyuma na Maendeleo ya Makazi, huku akimweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo.
Rais KIkwete alisema kuwa kosa kubwa alilofanya Tibaijuka ni kuruhusu fedha alizopewa na Jamea Rugemalila, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya VIP Engeneering kama msaada kwa shule yake kuingia moja kwa moja kwenye akaunti yake kitu amabcho ni kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma.
Prof. Tibaijuka amekiri mwenyewe mara kadhaa kupokea kiasi cha Bil. 1.6 katika akaunti yake, lakini akijitetea ni kwa ajili ya Shule anazomiliki na hiviu karibuni alinukuliwa akidai hatajiuzulu kwa vile hata Rais Kikwete atamshangaa na pia yeye na JK wanajuana kitambo tangu wakisoma wote Chuo Kikuu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Rais ni kwamba wamemshauri kuwapisha wamteue mwingine kushika nafasi yake kwa kukiuka miiko ya Maadili kwa maana nyepesi ni kwamba amemfuta kazi.
Prof Tibaijuka amekumbwa na sekeseke hilo kutokana na kukubali fedha alizopewa na Rugemalila kama msaada kwa shule yake kuingia kwenye akaunti yake.
Aidha Rais Kikwete amesema kuwa fedha katika akaunti ya ESCROW ni za IPTL na sio za TANESCO (Umma) huku na kuhusu Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mh. Raisi amesema kuwa suala lake linawekwa kiporo kwa bado ucchunguzi juu ya suala hilo unaendelea kufanyiwa kazi.
Pia aliweka bayana namna alivyofurahishwa na uzalendo ulioonyeshwa na Wabunge bila kujali itikikadi zao za vyama na kuwapongeza.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete
alipokuwa akihutubia Wazee wa jiji la Da es Salaam.
Sakata la akaunti ya ESCROW leo limeingia katika sura mpya baada ya
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
kumvua rasmi madaraka Prof, Anna Tibaijuka.
Akizungumza leo na wazee wa Dar es Salaam Raisi Kikwete alisema kuwa
kosa kubwa alilofannya Tibaijuka ni kuruhusu fedha alizopewa na
Rugemalila kama msaada kwa shule yake kuingia moja kwa moja kwenye
akaunti yake kitu amabcho ni kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma.
Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa akishikilia wadhifa wa Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Makazi amekumbwa na sekeseke hilo kutokana na kukubali fedha
alizopewa na Rugemalila kama msaada kwa shule yake kuingia kwenye
akaunti yake jambo lililozua mjadala mkubwa sana miongoni mwa raia wa
Tanzania huku wakihoji kwa nini iwe hivyo.
Hivi karibuni Prof. Tibaijuka aliutangazia umma wa Tanzania kupitia
vyombo mbalimbali vya habari kuwa hawezi kujiuzulu kwa kuwa yeye hana
kosa lolote katika sakata hilo huku akisisitiza kuwa akijiuzulu hata
Raisi mwenyewe atashangaa uamuzi wake.
Prof. Tibaijuka aliendelea kusisitiza kuwa endapo angejiuzulu
asingeitendea haki dhana ya mwanamke kuchakalika na maendeleo has kwa
jamii za Kitanzania.
Katika hatua nyingine Mh Raisi amesema kuwa fedha katika akaunti ya
ESCROW ni za IPTL na sio za TANESCO (Umma) huku na kuhusu Waziri wa
Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mh. Raisi amesema kuwa suala
lake linawekwa kiporo kwa bado ucchunguzi juu ya suala hilo unaendelea
kufanyiwa kazi.
Copy and WIN :##############