STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 18, 2014

Real Madrid yatuma salamu Liverpool, yaua 5-0 Ronaldo afunga 2

James Rodriguez
'Wauaji' wengine wa Real Madrid leo ni hawa watatu
Cristiano Ronaldo
Ronaldo akishangilia mabao yake
MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo ameendelea kutupia mabao kambani baada ya jioni ya leo kufunga mabao mawili wakati Real Madrid wakipata ushindi mnono ugenini dhidi ya Levante kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Ronaldo aliyefikisha mabao 15 katika mechi  ya nane, alianza kuaiandikia wageni bao kwa mkwaju wa penati dakika ya 13 baada ya Juanfran kufanyiwa madhambi na Javier Hernandez 'Chicharito' kufunga bao la pili katika dakika ya 38 akimalizia kazi nzuri ya James Rodriguez 'James Bond' .
Ronaldo alirudi tena kambani katika dakika ya 61 kwa kuaindikia Real Madrid bao la tatu akimalizia kazi ya Isco na James Bond akafunga bao la nne dakika ya 66 kwa kazi nzuri ya Ton Kroos na isco akamalizia kazi kwa kufunga bao la tano dakika nane kabla ya pambano hilo kumalizika kwa pande la Chicharito.
Ushindi huo wa Madrid uliowafanya wapunguze pengo la pointi na vinara Barcelona ni kama salamu kwa wapinzani wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool ya England watakaoumana nao siku ya Jumatano.
Katika mechi nyingine Athletic Bilbao ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Celta Vigo na kwa sasa Barcelona wapo nyumbani wakiumana na Elber na m atokeo bado ni 0-0.

Bayern yazidi kuchinja Bundesliga yapiga mtu 6-0

Mario GotzeMABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bayern MUnich wamezidi kuimarisha uongozi wao kwa kuibamiza bila huruma Werder Bremen kwa mabao 6-0.
Phillip Lahm na Mario Gotze walifunga mara mbili, huku Xabi Alonso na  Thomas Muller wakimalizia udhia kwa kuwekwa mingine kimiani na kuifanya vijana wa Pep Guardiola kufikisha pointi 20 baada ya michezo nane ya ligi hiyo maarufu kama Bundesliga.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Mainz 05 ikiwa nyumbani iliitambia     Augsburg kwa mabao 2-1, Hannover 96 ikalala nyumbani kwa mabao 3-0 dhidi ya Borussia Mönchengladbach, huku Freiburg  nao wakilala nyumbani 2-1 kwa Wolfsburg.
Timu za  Stuttgart na Bayer Leverkusen zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 3-3, huku FC Koln ikishinda nyumbani 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund na hivi punde Schalke 04 ikiwa nyumbani iliitambia Hertha Berlin kwa mabao 2-0.

AS Roma yaua Italia, kibabu Totti afunga

http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Roma+v+AC+Chievo+Verona+Serie+97hI1zc0UGix.jpg
AS Roma ikiwa uwanja wa nyumbani wameibuka na ushindi wa mabao 3-0, huku mkongwe Francisco Totti akifunga moja ya mabao hayo na kuzidi kuweka rekodi katika Seria A.
Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na Destro katika dakika ya nne,  Ljajić dakika ya  25'na Totti  aliyefunga kwa penati dakika ya 33.

Newcastle United yaona Mwezi England

Gabriel Obertan
Raha ya ushindi kwa Newcastle United
KLABU ya Newcastle United baada ya kushindwa kupata ushindi wowote katika Ligi Kuu ya England tangu Agosti 30 imezinduka kwa kuichapa Leicester City kwa bao 1-0 katika mechi iliyomaliza hivi punde.
Bao pekee lililotoa afueni kwa timu hiyo iliyokuwa nyumbani lilifungwa na Gabriel Obartan katika dakika ya 71 akimalizia kazi nzuri ya Demba Pappis Cisse na kuifanya timu hiyo kufikisha jumla ya saba japo imeshindwa kuchomoka kwenye eneo la hatari la kushuka daraja.

Huu ndiyo msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjtlvkjDhSlS65-hB-004rsYZJHQE4NobZV403ZyTd0wOSg5y8GsHbLgtIjZMhi54tknwwuuTLLETjNKtUeQgg2XaPMUfzGeIx26H3KEFoxiV0ynG2zxCXwoN3Ms2Tsy19Go4NbKzuhAyk/s1600/HMB_3985.JPG
Coastal Union iliyowaengua Yanga kwenye nafasi ya tatu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjN3yUookRbw5iagyyNOdXVC2x3bCSKEWnMyE3CdD3ClDJbjRMBjlm46wOFkf2vG3QxuVrysM_bG3S082zNzQ77EZ7WFu1gUXfcaatYEYOkE9Hswh57h_eXGh1G5kvKN9Zq5YUG22jzhdM/s1600/YAA.jpg
Yanga waliosimamishwa na Simbaa
Mbeya waliokubali kipigo cha pili nyumbani dhidi ya Azam
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                            P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01. Azam              04  03  01  00  06  01  +5   10
02. Mtibwa Sugar  04  03  01  00  06  01  +5   10
03.Coastal Union   04  02  01  01  06  04   02   07
04.Yanga              04  02  01  01  04  04   00  07
05. Kagera Sugar  04  01  02   01  03  02  +1   05
06. Mbeya City      04  01  02  01  01   01  00   05
07.Stand Utd        04  01  02   01  03   05  -2   05
08.Prisons            03  01  01   01  03   02  +1   04
09.Simba              04  00  04   00  04    04  00  04
10. Ruvu Shooting 04  01  01   02  03   05   -2  04
11. Ndanda Fc       04  01  00   03  07    09  -2  03
12. Polisi Moro       04  00  03  01   03    05   -2  03
13. Mgambo JKT    04  01  00  03   01    04  -3  03
14.JKT Ruvu          03  00  01  02   01   04   -3  01

Wafungaji Bora:
4-
Didier Kavumbagu(Azam)
3-
Ally Shomari (Mtibwa)
2- Shaaban Kisiga (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Ame Ally (Mtibwa), Rashind Mandawa (Kagera), Rama Salum (Coastal), Aggrey Morris (Azam)


Ratiba:
Kesho JUMAPILI
Prisons-Mbeya vs JKT Ruvu

Arsenal chupuchupu, Chelsea yaua, Southampton nouma

Arsenal walipotungulia mapema mabao kabla ya kuyarejesha
Alexis Sanchez (kushoto) akipongezwa kwa kufunga bao la kuongoza la Arsenal
Cesc Fabregas akishangilia bao lake wakati Chelsea wakishinda ugenini
Southampton celebrate
Southampton wakishangilia karamu yao ya mabao
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiJ8gVj4IzJtst16bFSW_FamQning4RDHnfQOlk3S1lv7CaHgAJvnfydlnLb1oqRZ8Y_RYiOcVgXAYzeQqhG40uG3ylSssbREGAk_Z23vGsZQkGAT29YghLNR-XJbx03NmjYbznx1efM9g/s1600/1413638977348_Image_galleryImage_Manchester_City_s_Argenti.JPG
Kun Aguero akishangilia moja ya mabao yake manne mapema leo walipoiua Spurs
MSHAMBULIAJI Danny Welbeck ameendelea kuonyesha jinsi gani alivyo muhimu ndani ya Arsenal baada ya kuifungia timu hiyo bao katika dakika za lala salama na kuwaepushia wapiga mtutu hao wa Emirates kuambulia sare ya mabao 2-2 ikiwa nyumbani dhidi ya Hull City.
Welbeck aliyekuwa hapewi umuhimu wowote katika kikosi cha Manchester United na hivyo kuuzwa kwa Arsenal, alifunga bao hilo dakika za nyongeza kabla ya pambano kumalizika na kumpa nafuu meneja wake, Arsene Wenger.
Mshambuliaji huyo nyota wa England alifunga bao hilo akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Alexis Sanchez, ambaye alianza kuwafungia wenyeji  bao dakika ya 13 kwa kumalizia kazi ya Per Martesacker.
Wageni walifunga mabao yao katika dakika ya 17 kupitia Mohammed  Diamé kisha kuongeza la pili dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia kwa Abel Hernandez.
Katika mechi ya mapema leo, Sergio 'kun' Aguero aliisambaratisha Tottenham Hotspur waliowafuata nyumbani kwenye uwanja wa Etihad baa da ya kufunga mabao manne wakati wakiwazisha vijogoo hao wa London ya Kaskazini kwa mabao 4-1. Mabao mawili yakiwa kwa mikwaju ya Penati.
Chelsea ikiwa ugenini ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace kwa mabao ya Oscar aliyefunga dakika ya sita kabla ya Cesc Fabrages kuongeza la pili dakika ya 51 na Campbell akaipatia bao la kufutia machozi wanyeji katika dakika ya 90.
Nayo Southampton ikiwa nyumbani iliwasambatarisha Sunderland kwa kuwafunga mabao 8-0 ikiwa ni rekodi ya kipigo kikubwa katika msimu huu wa ligi ya England, huku    Burnley ikiwa nyumbani ilifumuliwa mabao 3-1 na West Ham United na Everton walishinda nyumbani kwa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa.
Ushindi wa Southmpton umeifanya timu hiyo kufikia rekodi mojawapo ya mechi iliyokuwa na ushindi mnono ikienda sambamba na mechi nyingine tano tangu Ligi Kuu ilipoanza kutumika rasmi 1992 toka daraja la kwanza nchini humo..
Mechi nyingine za awali ni;
Manchester United 9-0 Ipswich, March 1995
Newcastle United 8-0 Sheffield Wednesday, September 1999
Tottenham Hotspur 9-1 Wigan Athletic, November 2009
Chelsea 8-0 Wigan Athletic, May 2010
Chelsea 8-0 Aston Villa, December 2012
Southampton 8-0 Sunderland, October  2014

Simba, Yanga debe tupu, Azam yaua, Mtibwa yabanwa

Mpambano wa watani ulivyokuwa uwanja wa Taifa leo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnGI0Fa_A1fReGNq630wAe-HUeAeC3CnzyXNWI0OAPfBgI-aka3Ybg_uU2XVpZaMurdewSapeGfrEvocd18umDQjB5vFdhDmsHEVhTWCSFg3rp4vfk7e-UZaT1IRvH4QtZHSFcKp6a8H7v/s1600/Picha+Simba.JPGhttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNPa5lzs3_DyhJWIBPQ4eR7PVVwEV7kBsmZgbFj2NkFWHudak-xT3RA29hwYq_es9UcaOF5fj0I9w9hmoY_GT4jyCWZ2zMxmOX1zN7vws4XBFeRVRUgqalCm9eoug3LZYGSjq7wMFA9_PP/s1600/Yanga+leo+1.JPGWAPINZANI wa jadi wa soka Tanzania, Simba na Yanga zimeshindwa kutambiana katika pambano lao lililochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, licha ya tambo za mapema kabla ya mchezo huo, huku Azam wakijikwea kileleni mwa msimamo wakiipiku Mtibwa Sugar waliobanwa mjini Morogoro.
Simba na Yanga ambazo zilikamiana na kutambiana kwa wiki kadhaa sasa, walishindwa kufungana katika pambano lililoshuhudia mtoto wa nyota wa zamani wa Mtibwa, Yanga na Taifa Stars, Manyika Peter, kipa Peter Manyika Jr aking;ara kwa kuinyima Yanga mabao kwenye uwanja huop wa Taifa.
Timu zote ilifanya kosa kosa za hapa na pale na has akwenye kipindi cha pili huku makocha wao, Marcio Maximo wa Yanga na Patrick Phiri wa Simba wakifanya mabadiliko ya wachezaji bila kuleta tija hadi dakika 90 za pambano lililochezeshwa vema na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 7 na kushuka hadi nafasi ya nne wakiwapisha Coastal Union kukalia nafasi hiyo baada ya jioni ya leo kushinda mabao 2-0 dhidi ya Mgambo na kufikisha idadi kama hiyo ya pointi ila ikiwa na uwiano tofauti ya mabao, huku watani zao hiyo ikiwa ni sare yao ya nne msimu huu na ikifikisha mechi ya 10 katika ligi bila kuonja ushindi imefikisha pointi nne.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Azam waliwafyatua Mbeya City nyumbani kwao kwenye uwanja wa Sokoine kwa bao 1-0 na kufikisha idadi ya mechi 38 bila kupoteza katika Ligi Kuu..
Bao hilo liliwekwa kimiani na beki wake wa kati, Aggrey Morris kwa mkwaju wa adhabu kwenye dakika ya 19 na kuifanya mabingwa watetezi hao kukwea kileleni wakifikisha pointi 10 sawa na Mtibwa Sugar ambao walilazlmishwa suluhu mjini Morogoro na ndugu zao Polisi Moro kwenye uwanja wa Jamhuri.
Azam na Mtibwa zote zimefungana idadi ya pointi zikiwa na 10 kila moja, huku wakiwa na mabao sita kila moja na kufungwa moja, isipokuwa kiherufi Azam inawatangulia Wakata Miwa.
Kutoka Mkwakwani Tanga, Coastal Union imezidi kujiongezea pointi baada ya kuilaza Mgambo JKT kwa mabao 2-0.
Mabao ya washindi yalifungwa na Rama Salim kwa mkwaju wa penati kabla ya Kennedy Masumbuko kuongeleza la pili kwenye kipindi cha pili.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEheu2S3fe_9FoFd7hnk3AwEiXmoOP2ulk9Y13fiRJl12EdBwVuaIaC0y1ulilytUphp2lKiDBXt3tJkB_gfKPzweV4tFKqdIhBe-kGqjPOH6NhkBOCD0sjIxEJ00LhbAeNd57i_xQ_Yrxkh/s1600/20140913_160438.jpg
Ndanda waliopigwa nyumbani na Ruvu Shooting

Nayo timu ya Ruvu Shooting wakiwa ugenini mjini Mtwara wamewatoa nishai wenyeji wao Ndanda Fc kwa kuwalaza mabao 3-1, mabao ya washindi yakiwekwa kimiani na Juma Nade, Abdurahman Mussa na Mathew. ilihali Kagera Sugar wakiwa nyumbani wamelazimishwa suluhu ya kutofungana na Stand United.
Ruvu waliovunja mwiko wa kutofunga bao lolote katika ligi ya msimu huu kwa kuilaza Ndanda mabao 3-1
Mtibwa iliyobanwa mbavu na Polisi na kutoka suluhu

Chelsea katika kibarua kizito England

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/03008/Chelsea4_3008183b.jpgVINARA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea wataelekea kwa wapinzani wao jijini London Crystal Palace Jumamosi wakilenga kupanua mwanya wa alama tano walioweka kileleni mwa Ligi hiyo baada ya mapumziko ya kimataifa.
Palace walishangaza Chelsea, na klabu nyingine katika ligi, kwa kushinda dhidi ya Chelsea msimu uliopita na nahodha wa Blues John Terry amepuuzia mbali madai kwamba tayari mshindi wa ligi msimu huu amejulikana.
“Ni wazi (kwamba kinyang’anyiro cha ligi) hakijaisha,” amesema Mourinho.
“Klabu nyingine zimejipata katika nafasi kama hii. Ni vyema kuongoza lakini ukiwa juu, kila mtu hutaka kukuangusha.
“Hilo ndilo jambo zuri kuhusu Ligi ya Premia na ndio maana kila mtu huipenda. Timu zinalenga kutushambulia kwa sababu tuko juu na twacheza vyema.”
Mabingwa watetezi Manchester City, walio wa pili kwa sasa, watakuwa nyumbani dhidi ya Tottenham Hotspur na kiungo wa kati anayeichezea City kwa mkopo Frank Lampard amewaambia wachezaji wenzake wajihadhari dhidi ya Spur ambao wameanza kuamka.
“Huenda wanapitia kipindi cha mpito lakini nilifurahishwa sana na meneja wao (Mauricio Pochettino) alipokuwa Southampton na ikiwa anaweza kufanya hayo Tottenham, ambao bila shaka wana vipaji kwenye kikosi chao, watafana. Ni timu nzuri sana.”

Gallas atundika galuga kimataifa

http://purelyfootball.com/wp-content/uploads/2014/08/1756906_201007087783881-1.jpg 
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, aliyewahi kutamba na klabu za Arsenal na Tottenham Hotspur, William Gallas ametangaza kustaafu soka rasmi baada ya kupita miaka 19 akicheza mchezo huo. 
Gallas mwenye umri wa miaka 37 amesema alikuwa akijiambia mwenyewe kwamba anaweza kuendelea lakini anadhani wakati umefika sasa wa kuamua kutundika daruga. 
Mkongwe huyo ambaye alianza rasmi soka lake katika klabu ya Caen mwaka 1995, aemcheza mechi 84 za kimataifa akiwa na Ufaransa na kufunga mabao matano likiwemo bao la utata katika ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa mtoano dhidi ya Ireland uliowapa nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2010. 
Gallas pia alicheza katika Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani ambapo Ufaransa ilifungwa na Italia kwa changamoto ya mikwaju ya penati. 
Baada ya kuitumikia klabu ya Olympique Marseille kuanzia mwaka 1997 mpaka 2001, Gallas alihamia Chelsea ambako alishinda mataji ya Ligi Kuu mwaka 2005 na 2006 na kujiunga na Arsenal msimu uliofuata kabla ya kuhamia Tottenham Hotspurs mwaka 2010. 
Octoba mwaka jana Gallas alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Perth Glory inayoshiriki Ligi Kuu nchini Australia maarufu kama A-League.

WASANII WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA KILIMO KWANZA,

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghpa5vbwvmheywlGByFh8o7yO3Lc5-fMZmE0gO73qD27VxUBAhXb1yN7qEolYtIdZPYrCRKFKvR7QrWlUIS7-zb28hnDj9JlTvIe8GHj8K76kVfYhyphenhyphen1izNYfjmIKGjUEfdT4Yi-zGK0-dN/s1600/shiwata.JPG
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib
MCHUNGAJI wa Kanisa la KKKT, John Solomoni, ameshangazwa na kitendo cha idadi ndogo ya wasanii kujitokeza katika kununua mashamba ya bei rahisi yanayotolewa na Shirikisho la wasanii Tanzania(SHIWATA( yaliyopo Kijiji cha Ngarambe Wilayani Mkuranga.
Solomoni  ambaye pia ni Katibu wa kamati ya amani ya viongozi wa Dini mkoa wa Dar es Salaam,aliyasema hayo juzi katika hafla ya kuoneshwa mashamba kwa wasanii hao iliyoendana sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema kitendo kilichofanywa nawasanii inaonesha ni jinsi gani bado haewajaanza kujitambua katika kutengenezamaisha yao ya mbeleni.
Alisema kiasi cha shilingi 200,000 kinachotozwa kwa ajili ya msanii kupata ekari moja na nusu ni kidogo sana ukilinganisha na thamani ya ardhi ilivyo sasa lakini anawashangaa kwa nini wasanii wameshindwa kujitokeza kama ilivyotarajiwa.
“Hapa nimeambiwa shirikisho lina wasanii zaidi ya 8000 wakiwemo wasanii wakubwa wenye majina lakini kwa nini ni 95 tu ndio wanunue mashamba hii ni aibu na kushindwa kujitambua nyie ni kina nani mbele ya jamii,”alisema Mchungaji Solomon.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga,Saada Mwaruka, alisema kama Wilaya watawapa ushirikiano wa hali na mali wasanii waliochukua mashamba hayo ikiwemo kuwakopesha pembejeo za kilimo.
Mwaruka alisema wanataka waone  eneo hilo linakuwa shamba darasa la kuigiwa mfano jambo litakalowaamsha vijana wa Mkuranga nao kujishughulisha na kilimo na kuona kilimo sio kazi ya waliokosa kazi bali ni moja ya njia za kuwainua kiuchumi.
Naye Mwenyekiti wa Shiwata, Cassim Taalib, alisema  wameamua kubuni mbinu hiyo ili kuwaondoa wasanii wa nchi hii katika umasikini.
Taalib alisema katika mashamba hayo kuna jumla ya ekari 500 kwa ajili ya kulima huku awali walitangulia kagawa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba robo ekari kwa kila msanii lililopo maeneo ya Mwanzega huko huko Wilayani Mkuranga ili nao waweze kumiliki nyumba.
Alisema utaratibu huo ndio ulitumiwa na Mwalimu Nyerere wakati wa kuhamasisha vijiji vya Ujamaa ambako mpaka leo watu wameona matunda yake.

SIMBA, YANGA MWISHO WA TAMBO LEO TAIFA

Simba
Yanga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg-gq39K7CdJepat14klzaYSKkbOOhTk4agTfimjq9e_T_i79-pSKFHrC001eHuYXQ6J66Ddn1velG_DzJ9mP9Z6oGjeZC2ZIPr2Rc51jI6a4QvPo15HKLVYLKybQY2AbSGUsgkhBIKlL0/s1600/katuni_watani.jpg
Katuni ya Chris Katembo nayo inazungumza je nani ataibuka mbabe leo Taifa?
BAADA ya tambo, kejeli na majigambo ya muda mrefu baina ya Simba na Yanga, hatma yote inatarajiwa kufahamika leo baada ya pambano lao litakalofanyika kwenye uwanja wa Taifa.
Simba na Yanga zinakutana katika pambano la 78 la Ligi Kuu tangu mwaka 1965, huku Yanga wakiwa wababe wa Simba kwa kushinda mara 29 dhidi ya 22 za watani zao wanaotokea kambini nchini Afrika Kusini.
Timu hizo zinakutana leo kwenye dimba hilo huku Simba wakionekana wachovu zaidi kulinganisha na Yanga msimu huu wakikamata nafasi ya 10 baada ya mechi za raundi tatu, wakati wapinzani wao wakiwa nafasi ya tatu wakitofautiana kwa pointi tatu.
Simba haijashinda pambano lolote kati ya 9 iliyochezwa kumalizia msimu uliopita na katika mechi za msimu huu, zaidi ya kuambulia sare tu.
Hata hivyo pambnano la watani huwa haliamuliwi kwa kuangalia rekodi kama hizo, kwani lolote huweza kutokea na kushangaza wale wanaotabiri labda kwa kuangalia udhaifu wa timu.
Mashabiki wa Yanga kwa sasa ni kama wanashangilia ushindi dhidi ya watani zao, lakini soka ni baada ya dakika 90 kwani lolote linaweza kutokea na kushangaa Simba wanaoonekana wanyonge kuibuka na ushindi dhidi ya watani zao.
Yanga inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na matokeo waliyoyapata kwenye michezo mitatu ya kwanza ya ligi kuu ya Bara ukilinganisha na sare tatu mfululizo za mtani Simba.
Yanga iliyoshinda michezo miwili, ina ponti tatu zaidi ya Simba kutokana na kufungwa na viongozi wa ligi Mtibwa katika mechi ya ufunguzi wa msimu.
Tayari makocha wa timu zote mbili wamekuwa wakitoa kauli tofauti kwa wiki kadhaa kuonyesha namna pambano hilo lisivyotabirika kirahisi.
Marcio Maximo amekuwa akisisitiza kuwa mashabiki waende uwanjani kuona kitakachotokea, bila kuweka bayana kama ana hakika Yanga kushinda ila anasisistiza kuwa wamejiandaa vya kutosha, wakati Patrick Phiri  ametadharisha na kusema ni mchezo huo utakuwa wa aina yake.
"Wenzetu wana matokeo mazuri zaidi yetu kwa kuwa wameshinda michezo miwili mfululizo laikini hilo haliwapi uhakika wa ushindi," alinukuliwa Phiri.
Phiri alisema anajua mapungufu ya wapinzani wao na kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo huku 'akiita' mashabiki kujaa kwa wingi uwanjani.
"Mashabiki (wa Simba) wasiwe na wasiwasi... tumejipanga vizuri kwa mchezo huu na kambi yetu ya Afrika Kusini imetusaidia.Tutapambana kupata ushindi.," alisema.
Kwa matokeo ya hivi karibuni, Simba tangu walipoifunga Yanga mabao 5-0 katika mechi ya kufungia msimu wa 2011-2012 haijashinda tena zaidi ya kuambulia sare na kuchapwa kama ilivyokuwa ligi ya kufungia msimu wa 2012-2013 walipolala mabao 2-0.
Timu hizo zinakutana huku kila moja ikiwa na idadi kubwa ya majeruhi ambao huenda wakakosekana uwanjani.
Simba ina uhakika wa kumkosa golikipa wake Hussein Sharif 'Casillas' huku pia mlinda mlango namba moja, Ivo Mapunda akiwa na uwezekano mdogo wa kuanza hivyo golikipa yosso Manyika Peter anatarajiwa kuanza golini.
Kwa upande wa Yanga, huenda ikamkosa kiungo wao nyota Haruna Niyonzima aliyeumia enka kwenye mazoezi ya timu hiyo wakati nahodha Nadir Haroub 'Canavaro' ambaye aliumia Jumapili akiwa na kikosi cha timu ya taifa na kushonwa nyuzi tatu ataangaliwa afya yake mpaka muda mfupi kabla ya mechi.
Katika mbili za msimu uliopita, timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya mechi ya awali kuisha kwa sare ya 3-3 na waliporudiana Aprili mwaka huu walifungana bao 1-1, Yanga wakilazimika kuchomoa 'usiku' kwa bao ya Simon Msuva, kama watani zao walivyochimoa mabao matatu katika ligi ya duru la kwanza.

HIZI NDIZO RATIBA ZA LEO ZA LIGI KUU TANO MAARUFU DUNIANI


http://modelsportsfan.com/wp-content/uploads/2013/08/EPL-La-Liga-Bundeliga-Serie-A-Logo.jpghttp://www.informationng.com/wp-content/uploads/2012/10/63751112_5738e41b-fd90-4ceb-bf30-b450f5664095.bmp 
LONDON,
Ratiba ya ligi kuu ya soka ya Uingereza ya LEO 

Man City        v Tottenham    (8:45) 
Arsenal        v Hull City    (11:00) 
Burnley        v West Ham
Palace       v Chelsea    (11:00) 
Everton        v Aston Villa
Newcastle    v Leicester
Southampton    v Sunderland

MADRID,
Mechi katika ratiba ya La Liga, ligi kuu ya soka ya Hispania, LEO:
Levante        v Real Madrid    (11:00) 
Athletic        v Celta Vigo
Barcelona    v Eibar        (3:00) 
Cordoba        v Malaga

ROME,
Ratiba ya ligi kuu ya soka ya Italia, Serie A, LEO: AS Roma        v Chievo Verona
Sassuolo        v Juventus

MUNICH,
Mechi za Bundesliga, ligi kuu ya soka ya Ujerumani, LEO:
Cologne        v Dortmund
Bayern        v Werder Bremen
Mainz        v FC Augsburg
Hanover 96    v Gladbach
Freiburg        v VfL Wolfsburg
Stuttgart    v Leverkusen 
Schalke 04    v Hertha Berlin

PARIS,
Mechi za Ligue 1, ligi kuu ya soka ya Ufaransa, za LEO:
FC Lorient    v St Etienne
Monaco        v Gaillard
Metz            v Stade Rennes
Nantes        v Stade Reims
Lille        v Guingamp
Nice            v Bastia

DAVIDO WA NIGERIA AZUA SONGOMBINGO BONGO

http://www.redpepper.co.ug/wp-content/uploads/2014/07/Davido-1.jpg
MSANII nyota wa Nigeria, Davido ameibua songombingo la aina yake baada ya kuvifanya vituo maarufu vya redio nchini Times FM na Claoud's FM kuburuzana mahakamani.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam imemzuia msanii kutoka
Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama 'Davido' kuperform katika tamasha la
Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na Prime Promotion, October 18,2014.
Amri hiyo imetolewa jana (October 17) na hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu mheshimiwa D. Kisoka kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa
mahakamani hapo na Times Fm Radio na Times Fm Promotion.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion walipeleka maombi ya dharura
mahakamani hapo wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika
tamasha hilo kwa kuwa licha ya BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa
kutoa kibali cha msanii huyo kwa maelezo kuwa tayari alikuwa
ameshachukuliwa kibali cha kuperform nchini November 1 kwenye tamasha
lililoandaliwa na Times Fm Radio,  Clouds Fm na Prime Times Promotion
waliendelea na taratibu zote bila kujali zuio hilo la BASATA.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion waliiomba mahakama kuidhinisha madai
yao dhidi ya Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni
inayomsimamia Davido, HKN Music.
Madai hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama na usumbufu
waliosababishiwa na walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama imetoa amri kuwa msanii huyo amezuiwa kufanya onesho hilo October
18,2014 hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana mhakamani hapo.
Awali, Davido alisikika katika matangazo ya Times Fm Radio akieleza kuwa
atakuja Tanzania November 1 kwa ajili ya kufanya onesho linaloandaliwa na
kituo hicho cha radio lililopewa jina la 'The Climax'.