STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, October 23, 2014

Wolfsburg watakata ugenini Europe League



http://www.uefa.com/MultimediaFiles/Photo/competitions/Comp_Matches/02/15/88/77/2158877_w2.jpg
KLABU ya Wolfsburg ya Ujerumani jioni hii imepata ushindi mnono ugenini baada ya kuibamiza FK Krasnodar ya Russia katika mechi ya Kundi H ya michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya Europe League.
Wageni hao walianza kwa kuzawadiwa bao na beki wa Krasnodar, Andreas Granqvist kujifunga dakika ya 37 bao lililodumu hadi mapumziko.
Washindi hao waliongeza bao la pili kupitia Kelvin De Bruyne dakika ya 46 akimalizia kazi na Naldo kabla ya Granqvist kusahihisha makosa yake kwa kuifungia timu yake bao kswa penati dakika ya 51.
Mshambuliaji Luiz Gustavo aliiongezea Wolfsburg bao la tattu dakika ya 64 kabla ya Bruyne kuongeza jingine dakika ya 79 na wenyeji kupata bao la pili la kufutia machozi lililofungwa na Wanderson katika dakika ya 86.
Mechi nyingine za makundi kwa michuano hiyo ya Ulaya inaendelea usiku huu.

RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA DAR

Rais wa TOC, Gullam Rashid (kushoto)
RAIS wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi ya makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Hafla ya ufungaji kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Kozi hiyo ya wiki mbili iliyoanza Oktoba 12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli. Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita). Wengine ni Edna Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma). Pia wapo Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa). Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa vyeti vya ushiriki tu.

Liverpool kujaribu kwa Lavezzi, baada ya Balotelli kuchemsha

Ezequiel Lavezzi 2014BAADA ya Mario Balotelli kushindwa kuvaa vyema viatu vya Luis Suarez, klabu ya Liverpool imesema inajiandaana kutenga pauni milioni 30 kwa ajili ya kumnasa wa PSG, Ezequiel Lavezzi katika usajili wa mwezi Januari.

Vijogoo hao wa Anfield wamekuwa wakidaiwa kumnyemelea Strika huyo katika sehemu kubwa ya kipindi cha uhamisho wa wachezaji cha kiangazi lakini mpango huo ulikwama.

Hata hivyo kwa mujibu duru za soka nchini humo zimedai kuwa, meneja Brendan Rodgers anajipanga kujaribu tena mpango huo kwa mabingwa wa soka wa nchini Ufaransa wakati dirisha la usajili litakapo funguliwa tena mapema mwakani.

Liverpool imekuwa ikihaha kusaka mshambuliaji tangu mapema kutokana na pengo lililoachwa na Suarez aliyeuzwa Barcelona na pia kuumia kwa Daniel Sturridge.
Ilimsajili Mario Balotelli kwa Pauni Milioni 16, lakini mpaka sasa dau hilo halijaleta matunda kutokana na Muitalia huyo mwenye asili ya Ghana kushindwa kufunga mabao na huku akiwa mwingi wa vituko.
Liverpool iko katika nafasi ya sita katika ligi ikiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea kwa alama tisa baada ya michezo minane kukamilika.
Lakini Rodgers bado ana matumaini ya kuimarihsa kikosi chake mwezi Januari ili kuweza kupata nafasi nyingine ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu mwingine.
Kikosi hicho jana kilikumbana na kipigo cha aibu toka kwa Real Madrid baada ya kufungwa 3-0 ikiwa ni marfa ya kwanza tangu mwaka 2009 ambapo timu hiyo ilikuwa ikiwatambia Mabingwa hao wa Ulaya.

Tanzania yapaa FIFA, cheki orodha mpya ya Oktoba

Pambano lililoibeba Tanzania katika orodha mpya ya FIFA
SHIRIKISHO la Kandanda Duniani, FIFA limetangaza viwango vipya vya soka ambapo Tanzania imepanda kwa nafasi tano, huku Ujerumani ikiendelea kung'ang'ania nafasi ya kwanza.
Kwa mujibu wa orodha mpya Tanzania iliyokuwa ya 115 katika orodha ya mwezi Septemba, imepanda hadi nafasi ya 110 hii ni kutokana na ushindi wake wa mabao 4-1 dhidi ya Benin.
Hata hivyo ni kwamba Uganda imeendelea kuwa juu ya nchi zote wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), pamoja na kushuka kwa nafasi tano hadi ya 84.
Algeria ndiyo kinara wa nchi za Afrika ikikamata nafasi ya 15 duniani, wakati Mabingwa wa Dunia Ujerumani imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani ikiziongoza Argentina na Colombia wanaoifuata.
Orodha hiyo inaoonyesha  Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ufaransa, Uruguay, Ureno na Hispania ndizo zinazofunga 10 Bora, ilihali Ivory Coast waliokuwa wakiiongoza kwa muda mrefu Afrika ikiporomoka hadi nafasi ya 25 Duniani.
Ghana imeshuka kwa nafasi mbili hadi ya 35, wakati Misri imepanda kwa nafasi 23 hadi ya 38 na Cameroon imepanda kwa nafasi mbili hadi ya 40, ikifuatiwa na Senegal na Nigeria ambazo zote zimeporomoka kwa nafasi tano. 
Benin iliyopigwa 4-1 nq Tanzania yenyewe imeporomoka toka nafasi ya 78 hadi 86.
ANGALIA 30 BORA DUNIANI:    1    Germany
    2    Argentina
    3    Colombia
    4    Belgium
    5    Netherlands
    6    Brazil  
    7    France
    8    Uruguay
    9    Portugal  
    10    Spain  
    11    Italy  
    12    Switzerland
    13    Chile  
    14    Croatia
    15    Algeria
    16    Costa Rica
    17    Mexico
    18    Greece
    19    Ukraine
    20    England
    21    Romania
    22    Czech Republic
    23    USA
    24    Slovakia
    25    Côte d'Ivoire
    26    Bosnia and Herzegovina
    27    Ecuador
    28    Iceland
    29    Austria
    30    Russia

HATARI! Dawa za kulevya zenye thamani ya Sh. Bil 300 zanaswa Dar

GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya madawa yaliyokamatwa.
 
DAWA za Kulevya aina ya Heroin zenye ujazo wa kilo 7 zenye thamani ya zaidi ya Sh. Bil 300 zimenaswa jijini Dar es Salaam.
Watu hao wamekamatwa maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia Jumanne hii.
Wafanyabiashara wanaoshikiliwa na Kitengo hicho ni Mwalami Mohamed Chonji, Mariki Zuberi, Taka Adam, Rehan Musso na Abdul Abdallah ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Kitengo hicho,Godfrey Nzowa amesema,kukamatwa kwa watu hao kunafuatia taarifa kutoka kwa raia wema waliowatilia shaka watu hao.
     Aidha, kamishna Nzowa ameendelea kuwataka wananchi kuachana na Biashara hiyo haramu, ikiwa ni pamoja na kutoa wito kwa wakulima wanaozalisha bangi kuacha mara moja, kwa kuwa zao hilo ni miongoni  mwa dawa za kulevya.
Zaidi ya kilo mia tatu za Heroin zimekamatwa na kitengo  hicho tangu kuanza kwa mwaka huu.Hali hiyo inayopunguza kasi ya biashara hiyo hapa nchini.
 
 
Baadhi ya Dawa za kulevya zilizowahi kukamatwa na GODFREY NZOWA


GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya)


Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 


Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 


Mizani iliyokuwa inatumika kupimia Dawa za kulevya.


Kifaa kimojawapo ambacho wamekamatwa nacho watuhumiwa hao wa Dawa za Kulevya.


Dawa za kulevya  zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300 


GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya dawa za kulevya yaliyokamatwa.

Atletico Madrid moto chini, Juve yafa Galatasaray wanyukwa x4

Captain Diego Godin celebrates scoring Atletico Madrid's fourth goal against Malmo with teammate Joao Miranda
Nahodha Diego Godin akifurahia bao lake wakati Atletico Madrid wakiiangamiza Malmo
Pajtim Kasami
Muuaji aliyeizamisha Juventus akishangilia bao lake
Reus
Dortmund wakipongeza
Reus

ATLETICO Madrid imeendelea rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote nyumbani kwake baada ya usiku wa kuamkia leo kuwatungua Malmo ya Sweden mabao 5-0, huku Juventus ikilala ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Olympiacos.
Vijana wa Diego Simeone waliocheza mechi ya fainali za michuano hiyo msimu uliopita walipata mabao yake kupitia kwa Koke, Mandzukic, Griezmann, Godin na Cerci na kufanya Atletico kufikisha pointi 6 sawa na Olympiacos waliowanyoa Juvetus.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo   Bayer Leverkusen walishinda nyumbani mabao 2-0 dhidi ya Zenit, Monaco ikang'ang'aniwa nyumbani na Benfica kwa kutoka suluhu, Galatasaray wakafa nyumbani kwa mabao 4-0 kichapo walichopewa na Borussia Dortmund.

Liverpool yafa nyumbani, Ronaldo acha bhana, Arsenal chupuchupu

Cristiano Ronaldo scored the opener for Real Madrid at Liverpool

Cristiano Ronaldo and Mario Balotelli ahead of the Liverpool-Real Madrid game

Cristiano Ronaldo scored the opener for Real Madrid at Liverpool
Ronaldo akifunga bao la kwanza la Real Madrid
Karim Benzema scored twice in the first half for Real Madrid against Liverpool
Benzema akishangilia moja ya mabao yake jana
Mario Balotelli was taken off at half time for Liverpool against Real Madrid
Balotelli akiwa na Pepe
Lukas Podolski
Pongezi zako kaka!
Anderlecht 1-0 Arsenal
Najar akiwatungua Arsenal
CHRISTIANO amemfikia Lionel Messi katika orodha ya wanaokimbilia kuvunja rekodi ya mabao inayoshikiliwa na Raul ya mabao 71 baada ya kuisaidia Real madrid kuinyuka Liverpool 3-0 ikiwa kwao.
Ronaldo alifunga bao la kuongoza dakika ya 23 likiwa ni bao la 69 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na mechi 105 na kuwa sawa na Messi aliyecheza mechi 88 tu na kusaliwa mabao mawili kumfikia Raul.
Katika pambano hilo lililoshuhudiwa mshambuliaji wa kiitalia, Mario Balotelli akitolewa wkaati wa mapumziko na kubadilishana jezi na beki Pepe Karim Benzema alifunga mabao mawili.
Benzema anayesifiwa na Ronaldo kuwa ndiye namba 9 bora duniani alifunga dakika ya 30 na 41 na kuwazamisha vijana wa Brendan Rodgers aliyenukuliwa hatamvumilia tena Balotelli kwa alichokifanya uwanjani jana.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo la B, Ludogorets Razgrad imeichapa bao 1-0 Basel, huku katika mechi nyingine Arsenal ilitakata ugenini baada ya kuilaza Anderlecht mabao 2-1.
Mabao ya 'usiku' ya Kieran Gibbs na mtokea  benchi, Lukas Podolski yaliiokoa Arssenal isizame Brussels, Ubelgiji.
Wenyeji walipata bao dakika ya 72 kupitia Andy Najar kabla ya Gibbs kufunga dakika 88 na Podolski asiye na furaha Emirates kwa sasa kufunga dakika za nyongeza.
Arsene Wenger amedokeza kuwa hawana mpango wa kumuuza Mjerumani huyo mwenye asili ya Poland japo mwenyewe amekuwa akisisitiza kuwa Januari ataondoka Emirates akatafute mahali atakapoaminiwa na kucheza kwa raha zake.