STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 12, 2015

Messi azikata maini zinazomnyemelea, adai haiendi kokote

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/72166000/jpg/_72166204_hi020543910.jpg
Siendi Kokote
NYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa haendi kokote wakati kukiwa na taarifa za kuhusishwa kunyemelewa na Chelsea na Manchester City.
Messi alisema klabu hizo zinazodaiwa kutaka kumnyakua 'wote ni waongo' na kwamba atasalia katika klabu yake ya Barcelona.
Mshambuliaji huyo wa Argentina ambaye jana alifunga bao la tatu wakati timu yake ikishinda nyumbani 3-1 dhidi ya Mabingwa watetezi alidai taarifa zote kwamba anataka kuondoka Nou Camp ni uzushi.
"Sijaulizwa chochote kuhusu kusalia hapa kwa sababu sitaki kwenda kokote kwa sasa," alisema Messi.
Aliongeza kuwa anasikia kwamba amefanya mazungumzo na klabu za Chelsea na Manchester City kwa ajili ya kujiunga na Ligi Kuu tya England na kudai 'klabu zote hizo ni waongo'.
Akihojiwa na kituo cha TV ya klabu hiyo katika kipindi cha El Marcador alisema
"Nimesikia kwamba nimefanya mazungumzo na Chelsea na (Manchester) City....lakini ni uongo mtupu."
Taarifa kwamba kuna ufa mkubwa baina ya Messi na Kocha wake, Luis Enrique zimechochea taarifa za ama Messi au kocha huyo kung'oka Nou Camp.
Messi amekanusha pia taarifa kwamba amekuwa sehemu ya kutimuliwa kwa majkocha na wachezaji ndani ya klabu hiyo kwa kudai hakuna kitu kama hicho.
"Kuna taarifa nyingi juu ya mahusiano mabovu baina ya (Pep) Guardiola, (Samuel) Eto'o, (Zlatan) Ibrahimovic Bojan (Krkic) hakuna ukweli wowote," alisema.
Mchezaji huyo alisema amechoka kusikia habari za uzushi kuhusu yeye.

Waziri Mahanga azindua kitabu cha Marehemu Steven Kanumba

NAIBU Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga,  jana amezindua rasmi kitabu cha marehemu Steven Charles Kanumba, Kinachoitwa ''Steven Charles Kanumba: The Great Fallen Tree''  kilichoandikwa na Emmanuel Zirimwabagabo, raia wa Congo anayeishi nchini Canada.
Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu kama marehemu Kanumba na si kulalamika kila siku,  jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.
Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha Kanumba, ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kukisambaza dunia nzima.
Alisisitiza kwamba vizazi vijavyo ambavyo havikumuona vitamfahamu muigizaji huyo nguli wa Tanzania kupitia kitabu hicho kilichozungumzia maisha yake yote ya enzi za uhai.
Wasanii mbalimbali wa filamu walihudhuria uzinduzi huo huku bendi ya Malaika chini ya Christian Bella ilitumbuiza kusindikiza uzinduzi huo.
(Na Gabriel Ng'osha/GPL).

Nani kuwa Mwanasoka Bora wa FIFA leo, Ni Ronaldo au Messi?

http://static.goal.com/672500/672581_herol.jpg 
KITENDAWILI cha Nani kuwa Mwanasoka Soka wa Dunia wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA Ballon d'Or 2014 kinatarajiwa kutenguliwa leo wakati mshindi atakapotangazwa.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kutoka Ureno, Lionel Messi Muargentina anayeichezea Barcelona na kipa Manuel Neuer Mjerumani wa klabu ya Bayern Munich ndiyo wanaochuana kwenye tuzo hizo.
Messi anayeshikilia rekodi ya kunyakua tuzo hizo mara nne safari hapewi nafasi kubwa kama Ronaldo ambaye anaishikilia kwa sasa tuzo hiyo.
Hata hivyo kitendo cha kuvunja rekodi mbalimbali na kuifikisha timu yake kwenye fainali inampa nafasi ya kumuangusha Ronaldo, ingawa haitegemewi.
Wafuatiliaji wa soka wanaamini wachezaji wote watatu walioingia kwenye fainali wanastahili kunyakua tuzo hiyo, huku kipa Neuer akipigiwa chapuo kwa kuiwezesha timu yake ya taifa kutwaa ubingwa wa Dunia katika fainali za Kombe la Dunia za Brazil.
Je ni Messi, Ronaldo au Neuer atakayenyakua tuzo hiyo hiyo leo huko Uswisi zitakapotolewa.

Mwana Mfalme aahidi makubwa FIFA atakapochaguliwa

http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Ali+Bin+Al+Hussein+FIFA+Ballon+Gala+2012+NI3gHmXp6hll.jpgMGOMBEA Urais katika uchaguzi ujao wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Prince Ali bin Al Hussein amejinadi kuwa atakuwa atalifanya shirikisho hilo kuwa la uwazi na uwajibikaji kama atachaguliwa kugombea kumshinda rais wa sasa Sepp Blatter katika Uchaguzi huo.
Prince Ali mwenye umri wa miaka 39 alitangaza mipango yake ya kugombania nafasi hiyo mapema wiki hii na kuapa kusafisha jina la shirikisho hilo ambalo hivi sasa limechaguzi kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi. Mwana mfalme huyo wa Jordan amesema kama taasisi FIFA imekuwa ikifanya mambo yake kwa siri hivyo anadhani wakati umefika wa kubadilisha suala hilo na kulileta kwa wakati tunaoishi sasa wa ukweli na uwazi. Uchaguzi wa FIFA unatarajiwa kufanyika Mei 29 mwaka huu
Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limekuwa likighubikwa na kashfa ya rushwa juu ya mchakato wa upatikanaji wa wenyeji wa fainali mbili za Kombe la Dunia za 2018 zitakazofanyika Russia na zile za 2022 zitakazochezwa Qatar.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Wakala wa Ronaldo atwaa tuzo kwa mara ya 5 mfululizo

http://globesoccer.wpengine.netdna-cdn.com/wp-content/uploads/2014/05/Globe-Soccer-Awards-2371.jpgWAKALA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya wakala bora kwa mara ya tano mfululizo ijulikanayo kama Globe Soccer Awards.
Wakala huyo Jorge Mendes amepewa tuzo hiyo kwa kutambua mafanikio yake kama wakala wa wachzaji mojawapo akiwa Ronaldo.
Mendes ambaye kwa mara kwanza kunyakuwa tuzo hiyo ilikuwa mwaka 2010 amekuwa akiwasimamia wachezaji bora kabisa duniani ambapo mbali ya Ronaldo mwingine ni James Rodriguez na hata meneja wa Chelsea Jose Mourinho.
Ronaldo ndio aliyenyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na Globe Soccer huku meneja wa Madrid Carlo Ancelotti akinyakuwa tuzo ya kocha bora.

Mchungaji auwawa Kanisani akiendesha ibada

Security officers examin the lifeless body of an assistant pastor George Karidhimba Muriki of the Maximum Revival Ministries Church after he was shot dead by...
maafisa wa Polisi wakimsaidia msaidizi wa mchungaji aliyeuwawa nje ya kanisa hilo (Picha:AP)
WATU wenye silaha wasiofahamika walimfyatulia risasi na kumuuwa mchungaji mmoja wakati wa ibada kanisani siku ya jumapili katika mji wa Mombasa nchini Kenya  maahala ambako polisi wanapambana na vijana wa ki-islam wenye msimamo mkali.
Mauaji hayo yalitokea ndani ya mlango mkuu wa kuingilia kwenye kanisa la Maximum Revival Centre katika mtaa wa majengo. 
Mashahidi wanasema polisi waliwazuia watu wenye silaha kuingia ndani ya kanisa na kuuwa waathirika Zaidi. Watu hao wenye silaha hawajafahamika  lakini kundi la wanamgambo wa Al-Shabab kutoka nchi jirani ya Somalia limeshambulia malengo kadhaa nchini Kenya. Kundi hilo la Al-Shabab liliapa kulipiza kisasi kwa majeshi ya Kenya kuwepo nchini Somalia kwa ajili ya kusaidia  wanajeshi wa serikali dhidi ya wanamgambo hao.
VOA

Messi, Suarez, Neymar wafunga Barca wakiua Atletico Madrid

Lionel Messi, Neymar and Luis Suarez
Nyota wa Barcelona wakishangilia ushindi wao
Lionel Messi, Neymar and Luis Suarez
Furaha tupu kwa wakali wa Nou Camp
WASHAMBULIAJI nyota wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wote walifunga wakati timu yao ikiiadhibu mabingwa watetezi wa La Liga, Atletico Madrid kwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi hiyo ya Hispania.
Neymad alianza kufungua karamu ya mabao kwa wenyeji waliokuwa uwanja wa Nou Camp katika dakika ya 12 baada ya kumalizia kazi nzuri ya  Suarez kabla ya Suarez kufunga b ao la pili dakika ya 35 kwa kazi nzuri ya Messi.
Wenyeji walipata bao la kufutia machozi lililofungwa na Mario Mandzukic katika dakika ya 57 kwa mkwaju wa penati baada ya Messi kucheza madhambi langoni mwake dhidi ya Jesus Gamez.
Hata hivyo mshambuliaji huyo anayenyemelewa na Chelsea, alisahihisha makosa kwa kutumbukiza wavuni bao la tatu dakika tatu kabla ya pambano hilo kumalizika na kuifanya Barcelona kuwapumulia Real Madrid kwa tofauti na pointi moja, wenyewe wakiwa na 41 wakati Real wakiwa na 42.
Atletico Madrid wameendelea kusalia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 38 baada ya kucheza mechi  18 kama Barcelona, huku Real Madrid akiwa na mecho moja mkononi kwani imecheza mechi 17 tu.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Athletic Bilbao ilikubali kipigo cha 2-1 nyumbani dhidi ua Elche, Granada ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Real Sociedad inayonolewa na kocha David Moyes na leo usiku Rayo vallecano itakuwa wenyeji wa Cordoba katika mfululizo wa ligi hiyo inayozidi kushika kasi.

Juventus yaifyatua Napoli 3-1, yazidi kujikita kileleni

Paul Pogba akishangilia na wenzake
VINARA wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A, Juventus imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuikung'uta Napoli wakiwa ugenini kwa mabao 3-1.
Bao la Paul Pogba katika dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya Llorente liliwashtua wenyeji ambao walienda mapumziko wakiwa nyuma kabla ya kuzinduka kipindi cha pili baada ya iguel Britos kusawazisha dakika ya 64.
Dakika ya 69 wageni waliongeza bao la pili kupitia Martin Cacerea aliyemaliza pande la Andrea Pirlo na katika dakika za lala salama Arturo Vidal aliifungia Juventus bao la tatu na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 43 na kuzidi kuwakimbia wapinzani wa AS Roma waliomalizishwa sare ya 2-2 nyumbani na Lazio mapema jana.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Sampdoria ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Empoli.

Ali Baucha, Ney wa Mitego waja na Vululu

BAADA ya kutamba na 'Chimpododo' na 'Zumzum' aliomshirikisha K-One, dansa wa zamani na mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Ali Baucha anajiandaa kuachia wimbo wake mpya uitwao 'Vululu'.
Baucha aliiambia MICHARAZO kuwa wimbo huo mpya ambao umerekodiwa katika studio za Baucha Records, ameimba akishirikiana na Ney wa Mitego.
"Katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2015, nipo mbioni kuiachia kazi yangu mpya iitwayo 'Vululu' niliyoimba na msanii Ney wa Mitego, kila kitu kimekamilika kilichobakia ni siku ya kutoka hadharani," alisema Baucha.
Baucha alisema wimbo huo wa 'Vululu' ni miongoni mwa kazi mpya zilizotengenezwa na studio zake za Baucha Records.
Alisema kazi nyingine zitakazoachiwa ni pamoja na wimbo mpya wa K-One alioimba na Suma Lee na kazi mpya ya Fizzo aliyesumbua mwaka jana na '24 Hours' ambaye safari hii ataimba na Walter Chilambo

Rama Pentagone wa Twanga Pepeta Tajiri Penzi

MUIMBAJI mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Ramadhan Mhoza 'Pentagone' amefyatua wimbo wake binafsi uitwao 'Tajiri Penzi'.
Wimbo huo uliorekodiwa kwa mtayarishaji Amaroso ni utambulisho wa albamu binafsi ya muimbaji huyo wa zamani wa bendi ya Double M Sound, Levent Musica na Extra Bongo.
Akizungumza na MICHARAZO, Pentagone alisema wimbo huo ulio katika mahadhi ya rhumba ni kati ya nyimbo zitakazokuwa katika albamu yake aliyopanga kuitoa baadaye mwaka huu.
"Katika kutimiza ahadi yangu kwa mashabiki, nimetengeneza wimbo mpya uitwao 'Tajiri Penzi' ambao upo katika miondoko ya rhumba na ni kazi yangu binafsi nje ya Twanga Pepeta," alisema.
Pentagone alisema kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kutengeneza video ya wimbo huo kabla ya kuanza kurekodi nyimbo nyingine kukamilisha albamu yake ya kwanza itakayokuwa na jumla ya nyimbo sita au nane

Manchester United yapigwa nyumbani, yaporomoka EPL

Dusan Tadic (second right) pounces upon the rebound and converts coolly to hand Southampton the lead against Manchester United
Dusan Tadic akifunga bao pekee la Southampton
Southampton captain Jose Fonte led from the back for Southampton and kept Robin van Persie from having any impact on the game
van Persie akiwania mpira na Jose Fonte
Juan Mata (right) missed a number of good chances to level the scores shortly after Southampton went ahead against United
Juan Mata akijaribua kufunga bao
United captain Wayne Rooney cut a dejected figure as he left the pitch after the full time whistle was blown
Nahodha Wayne Rooney akiwa haamini kama wamepigwa kidude nyumbani
KLABU ya Manchester United licha ya kucheza uwanja wa nyumbani na ikiwa imefarijika kwa kurejea dimbani kwa baadhi ya nyota wake waliokuwa majeruhi imeshindwa kufurukuta baada ya kuchapwa bao 1-0 na Southampton katika mechi ya Ligi Kuu ya England.
Bao pekee la wageni ambao ni maarufu kama 'Watakatifu' lililowanyong'onyesha Mashetani Wekundu liliwekwa kimiani katika dakika ya 69 na Dusan Tadic na kuwafanya Southampton kukwea hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo wakiiengua Manchester United.
Ushindi umeifanya Southampton ambayo imelipa kisasi cha kufungwa nyumbani mwezi uliopita kwa mabao 2-1 na wapinzani wao kufikisha pointi  39, mbili zaidi ya ilizonazo vijana wa Luis Van Gaal licha ya zote kucheza mechi 21 kila moja.
Pia ni ushindi wa kwanza wa vijana wa Ronald Koeman katika uwanja wa Old Trafford tangu miaka 27 iliyopita kitu ambachop kimempa faraja kubwa koxcha huyo Mholanzi aliyewahi kuwa msaidizi wa Van Gaal.