Kocha wa Kagera Sugar, King Abdallah Kibadeni |
USHINDI wa mabao 3-1 iliyopata Simba jana kwenye pambano lao dhidi ya Ruvu Shooting, imewapa presha Kagera Sugar ambao wameenguliwa katika nafasi ya tatu waliyokuwa wanaishikilia mpaka jana.
Kocha wa Kagera Sugar, Abdallah Kibadeni, alisema ushindi wa Siomba umekuwa mwiba kwao kwa vile wanatishia ndoto zao za kuwepo kwenye Tatu Bora msimu huu.
Kagera wamelazimika kuwapisha Simba kutokana na kuzidiwa pointi mbili, Simba kwa ushindi wa jana imefikisha pointi 42, wakati Kagera wamesaliwa na zao 40.
Timu zote zimesaliwa na mechi mbilimbili kabla ya kufunga msimu, ambapo Kibadeni alisema watapigana kuhakikisha wanashinda zote, huku wakiiombea mabaya Wekundu wa Msimbazi.
"Kipigo cha Polisi na ushindi wa Simba jana umetuvurugia mipango yetu, lakini bado hatujakata tamaa na kumaliza katika Tatu BOra kwani tuna michezo miwili kama Simba, tutahakikisha tunashinda,:" alisema Kibadeni nyota wa zamani wa Simba, Majimaji Songea na Taifa Stars.
Katika mechi ya jana Wekundu wa Msimbazi, alipata ushindi kwa mabao ya Amri Kiemba aliyeanza kuifungia dakika ya
14 na kudumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili Ruvu walisawazisha dakika ya saba tu ya kuanza kipindi hicho kupitia kwa Abdulrahman Mussa kabla ya Edward
Christopher na Ismail Mkoko kuiongezea Simba mabao mengine baadaye.
Kikosi cha Simba kitashuka dimbani tena keshokutwa kwa kuumana na Mgambo Shooting ya Tanga inayohitaji pointi moja tu kuzishusha rasmi daraja Toto African na Polisi Moro.
Timu hiyo ya Mgambo ndiyo inayoshikilia roho za timu hizo mbili ambazo zina uwezo wa kufikisha pointi 25 ambazo maafande hao wa Mgambo wanazo mkononi kwa sasa.Kikosi cha Simba kitashuka dimbani tena keshokutwa kwa kuumana na Mgambo Shooting ya Tanga inayohitaji pointi moja tu kuzishusha rasmi daraja Toto African na Polisi Moro.
No comments:
Post a Comment