|
Simba |
|
JKT Ruvu |
|
Mbeya City iliyolala Morogoro |
BAADA ya kuwaweka roho juu mashabiki wao, Simba jioni ya leo imezinduka mbele ya JKT Ruvu baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 2-1 na kupanda hadi nafasi ya saba.
Mabao mawili ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Dan Sserunkuma yameisaidia Simba kupata ushindi wake wa tatu katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja wa Taifa na Simba walianza kuandika bao mapema kabla ya JKT Ruvu kurejesha na kwenda mapumziko matokeo yakiwa bao 1-1.
Bao la Simba lililofungwa na Sserunkuma liliwekwa kimiani katika dakika ya pili tu ya pambano hilo akiunganisha krosi pasi ya Emmanuel Okwi.
Hata hivyo JKT Ruvu walikuja kusawazisha bao hilo dakika ya 19 kwa George Minja kuunganisha kwa kichwa mpira wa Jabir Aziz na kufanya timu ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa.
Sserunkuma aliihakikishia Simba ushindi baada ya kufunga bao la pili katika dakika ya tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kewa kichwa akiwahi mpira wa krosi ya Okwi na kusaidia Simba kulipa kisasi kwa maafande hao ambao waliwafunga mabao 3-2 walipokutana mara ya mwisho.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 16 na kuchupa kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya saba.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Mtibwa Sugari imejikuta ikichupa hadi nafasi ya pili ya msimamo ikiziengua Yanga na JKT Ruvu baada ya kupata suluhu ya bila kufungana dhidi ya Coastal Union.
Mtibwa Sugar ilipata sare hiyo uwanja wa Mkwakwani Tanga na kufikisha pointi 18 sawa na ilizonazo Yanga waliokuwa wa pili ambao wanashuka hadi nafasi ya tatu japo kesho itashuka dimbani kuumana na Ndanda na kuwa na nafasi ya kukwea kileleni.
Nayo timu ya Polisi Moro imefanikiwa kuinyuka Mbeya City bao 1-0 ikiwa ni sikui chache tangu Mbeya City kutoka kuilaza Simba 2-1 katikati ya wiki kwenye mechi yao ya kiporo kilichochezwa uwanja wa Taifa.
Mjini Mbeya wenyeji Prisons ililazimishwa sare ya 1-1 na wageni wao Kagera Sugar katika mchezo unaodaiwa ulikuwa mkali na wa kusisimua wenyeji walianza kuzinguliwa kwa bao la Rashid Mandawa kabla ya kuchomoa dakika 15 kabla ya kumalizika kwa pambano hilo kupitia Nurdin Chona..
Katika mfululizo wa ligi hiyo kesho, Yanga itaikaribisha Ndanda kwenye uwanja wa Taifa wakati Ruvu Shooting wataialika Stand United ya Shinyanga kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.