Waandamanaji ambao ni madereva wa pikipiki mkoani Arusha,wakiwa
wamefunga barabara ya Moshi Arusha katika eneo la Ngulelo huku
wakionyesha moja ya mabango waliokuwa nao.
Madereva wa bodaboda wakiziba barabara kuu ya Arusha Moshi na kufanya magari zaidi ya 100 kushindwa kupita kwa saa 3
Askari wa FFU wakifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya madereva hao waliokuwa wamefunga njia
Dereva pikipiki ambaye hakujulikana mara moja jina lake akitaka kupasua
kioo cha gari dogo baada ya dereva wa kagi hilo kutaka kupita eneo
walilosuia.
MADEREVA pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zaidi ya
300,jijini hapa wameandamana na kufunga barabara kuu ya Moshi Arusha kwa zaidi
ya saa 3 ,katika eneo Ngulelo jijini hapa , wakilituhumu jeshi la polisi kumwachia
mtuhumiwa wa mauaji anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwenzao bila hatia.
Madereva hao wakiwa na pikipiki zao, walifunga barabara
hiyo kuanzia majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana kwa mawe na magogo
hali iliyolazimu jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kati na
kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto .
Kwa mujibu wa mmoja wa waendesha pikipiki,Jonathan Emanuel
,Mkazi wa Ngulelo wilaya ya Arumeru,maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya
mwenzao aliyemtaja kwa jina la Hilari Elias (36)mkazi wa Oldadai, aliyeuawa kwa
kupigwa risasi septembe 15 mwaka huu
akiwa barabarani eneo la baraa akimsafirisha
abilia aliyekuwa amemkodi.
Madereva hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kulaani jeshi la polisi kumwachilia
mtuhumiwa wa mauaji(jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha na
mmiliki wa garage ya kutengeneza magari
na mkazi wa Baraa jijini hapa ,walilituhumu jeshi la polisi
mkaoni hapa kwa kucheza mchezo mchafu wa kumwachulia mtuhumiwa
aliyempiga risasi dereva mwenzao na kumsababishia kifo chake.
Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha basi eneo la
Ngulelo majira ya saa 2 asubuhi kuelekea mjini katika chumba cha maiti katika
hospitali ya mkoa Mount Meru kuuchukua mwili wa merehemu na baadaye yalielekea
nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo madereva hao kwa pamoja walivunja lango la kuingilia na kuharibu mali
za mtuhumiwa ikiwemo gari lake lililovunjwa vioo vyote pamoja na vyoo vya
nyumba hiyo.
Aidha baada ya tukio hilo madereva hao walifunga
barabara katika eneo la Ngulelo kwa mawe na magogo wakishinikiza mkuu wa mkoa wa Arusha ,Magesa Mulongo kufika
eneo hilo na kuwasikiliza kwani walikuwa hawana imani na jeshi la polisi huku
wakidai ya kuwa mtuhumkiwa wao naonekana akirandaranda mitaani.
Katika eneo hilo pamoja na kufunga barabara hiyo,madereva
hao walivunja vioo vya magari kwa kupiga
mawe vioo vya magari na kuharibu baadhi
ya magari yaliyokuwa yakijaribu kupita kwa nguvu wakati wamefunga
barabara hiyo,huku wakipaza sauti kwa kupiga yowe wakiwa wamelala
barabarani huku wakitaka mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo afike
kuwasikiliza kilio chao kwani hawana imani na jeshi la polisi.
Hata hivyo polisi baada ya kufika eneo la tukio,
waandamanaji hao walianza kupiga yowe huku wakirushia mawe gari la polisi ambao walilazinika kuondoka
kwa kasi kwa lengo la kujinusulu, ambapo baadae walirejea wakiwa na nguvu
mpya na kuanza kuwafyatua mabomu zaidi
ya 10 na kufanikiwa kuwasambaratisha na kufungua njia .
Akisimulia chanzo cha mauaji hayo,Jonathan Emanuel alieleza
kuwa siku ya tukio marehemu akiwa na dereva mwenzake walikodishwa na
abilia wawili kwa lengo la kuwapeleka
nyumbani kwao,lakini wakiwa njiani waliliona gari aina ya Escudo kwa mbele yao
na kujaribu kulipita.
Alisema kuwa marehemu alijaribu kulipita gari hilo
lakini dereva wa gari hilo ambaye ni
mtuhumiwa alimzuia kwa kuziba na kusimama ambapo alimuuliza alikuwa anakimbilia
wapi.
‘’huyo dereva wa escudo alimzuia marehemu kupita kwa
kuziba njia na kumhoji kuwa kwanini anakimbia na alikuwa nakimbilia wapi’’alisema
Alisema kuwa kulitokea majibishano baina ya marehemu na mtuhumiwa ndipo
mtuhumiwa huyo alipochomoa bastola na kumfyatulia risasi kifuani na kufariki
dunia papo hapo huku abilia wake akiduwaa asijue la kufanya.
Madereva
hao wanadai kuwa jeshi la polisi mkoani Arusha wameshindwa kuwatendea
haki kwa kumbana mtuhumiwa ambaye anaonekana mtaani huku akitamba kuwa
yeye ni zaidi yao na kwamba hawezi kufungwa kama wanavyofikiria.
Tukio
hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani
Arusha,Liberatus Sabasi na kueleza kuwa polisi bado wanaendelea na
uchunguzi wa
tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi hapo baadae,na mwili wa
merehumu huyo umezikwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwap en o la
Oldadae.