STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 21, 2012

AIRTEL YAKABIDHI T-SHIRT 400 NA MILIONI TANO KWA AJILI YA MASHINDANO YA RIADHA YA ROCK CITY


Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi moja kati ya T-shirt mia nne Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel walikabidhi T-shirt mia nne pamoja na milioni tano kusaidia mbio hizo.


Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi moja kati ya T-shirt mia nne Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel walikabidhi T-shirt mia nne pamoja na milioni tano kusaidia mbio hizo.
Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni tano Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu, Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu ya udhamini wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 28 Oktoba. Airtel pia walikabidhi T-shirt mia nne zitakazotumika katika mbio hizo.

AIRTEL yaahidi kuendelea kusaidia maendeleo ya michezo nchini

KAMPUNI ya mawasiliano nchini ya Airtel imeahidi kuendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya vijana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika hafla fupi ya kukabidhi shilingi milioni tano pamoja na T-shirt mia nne kama udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu zenye kauli mbiu ‘tukuze utalii wa ndani kupitia michezo’, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwemo riadha ili kukuza maendeleo ya vijana.
“Udhamini wetu wa shilingi milioni tano pamoja na T-shirt mia nne katika mbio za Rock City mwaka huu unalenga katika kusukuma maendeleo ya vijana kupitia michezo kwa kuwa tunaamini kuwa michezo imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajira duniani.
“Tunaahidi kuendelea kusaidia michezo mingine kwa kuwa pia tunaamini kupitia michezo mbalimbali tunaweza kutangaza vivutio vyetu vya utalii duniani. Mfano nzuri ni mbio za mwaka huu za Rock City Marathon zitakazowakutanisha wanariadha mbalimbali kutoka nchi jirani,” aliongeza Bi. Matinde.
Akipokea hundi na T-shirt hizo, Mratibu wa mbio hizo kutoka katika kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bi. Grace Sanga aliishukuru kampuni ya Airtel kwa kuendelea kusaidia mbio za Rock City na kuyahasa mashirikia na makampuni mengine kuiga mfano wa kampuni hiyo.
“Tunaishukuru Airtel kwa msaada wao kwa kuwa msaada huu utatusaidia tujiandae vizuri na Rock City Marathon ya mwaka huu itakayofanyika Oktoba tarehe 28 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,” alisema Grace.
Grace alisema kuwa mbali na Airtel wadhamini wengine ni pamoja na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Parastal Pension Fund (PPF), Geita Gold Mine, African Barrick Gold, Air Tanzania Company Ltd (ATCL), Mamlaka ya Taifa ya Mbuga za Wanyama nchini (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Nyanza Bottles, New Africa Hotel na New Mwanza Hotel.
Aidha, Bi Sanga aliwaasa wanariadha kujitokeza na kuanza kujisajili ili kushiriki katika mbio hizo na kusema kuwa fomu za usajili zinapatikana katika ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo katika jengo la ATCL ghorofa ya tatu, ofisi za Bodi ya Utalii jengo la IPS ghorofa ya tatu, Dar es Salaam, na zinapatikana katika tovuti ya www.rockcitymarathon.blogspot.com.
CPI ilitangaza kuwa atakayeibuka kinara katika mbio za kilometa 21 mwaka huu kwa wanaume na wanawake atazawadiwa shilingi milioni moja na laki mbili wakati mshindi wa pili ataweka mfukoni shilingi laki tisa na mshindi wa tatu ataondoka na shilingi laki saba.

No comments:

Post a Comment