STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 17, 2013

Da! Hemed, Mlela waja kivingine katika I Know U

Hemed (kushoto) akimtishia bastola Mlela
Hemed na Mlela wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya kuumizana huku mama yao akiwaangalia kwa huzuni
Kasha la filamu mpya ya bifu la kina Mlela na PHD inayotarajiwa kuingia mtaani keshokutwa Jumatano.
LILE bifu lililowahi kufukuta kwa kasi mithiri ya moto wa kifuu baina ya ‘tozi’ wawili ndani ya tasnia ya filamu, Hemed Suleiman ‘PhD’ na Yusuf Godfrey Willard Mlela ‘Mlela’ linadaiwa kuibuka upya na kuzidisha uhasama baina ya wasanii hao.
Aidha, alisema bifu hilo lilidhihirika hivi karibuni wakati wawili hao walipokutanishwa kuigiza filamu moja, kwani mara kwa mara walijikuta wakifanya kweli kwenye baadhi ya vipande vya ugomvi na mapigano jambo lililompa wakati mgumu muongozaji wa filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni kuanzia Desemba 18 mwaka huu iliyopewa jina la I Know You.

“Walikuwa na muda mrefu sana bila kukutana, tukadhani bifu lao halipo tena, lakini hivi karibuni walikutana kwenye filamu iliyoandaliwa na Mtitu Game 1st Quality, wakawa wanafanya kweli kwenye baadhi ya sehemu za majibizano na mapigano huku wakifanyiana fujo mbalimbali huku kupigana vijembe vya wazi,” alisema rafiki huyo.

“Ni kweli tulikuwa na utofauti, ule mvutano wa zamani bado ulikuwepo, kila mmoja hakutaka kuwa dhaifu kwa mwenzake, utaona baadhi ya vipande tulivyofanya kweli,” alisema Mlela ambapo simu ya Hemed iliita bila kupokelewa licha ya mwandishi wetu kuipiga mara kwa mara.

Naye Meneja matayarishi wa Kampuni ya Game st Quality Ltd, Noel Amani ‘Futo’ alisema filamu ya I know You iliwapa wakati mgumu sana kutokana na bifu la wasanii hao kuonekana waziwazi.
“Walitumbua sana, kuna wakati walifokeana kweli, kukunjiana ngumi hata hivyo kuna baadhi ya vipande walivyofanya kweli tumelazimika kuviacha ili kuleta uhalisia zaidi. Kila mmoja anaamini yuko juu ya mwenzake,” alisema Futo.

Tanzanite waagwa kutimka kesho Sauzi

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura akikabidhi bendera kwa madada wa Tanzanite leo (Picha zote: Lenzi ya Michezo)
Wakisikiliza nasaha kabla ya kuondoka kesho kwenda kuiwakilisha Tanzania
Kocha Kaijage (kati) akizungumza huku Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, akisikiliza kwa makini
Tunaenda kupigana na lolote linaweza kutokea tuombeeni tu
nahodha wa timu naye akitoa yake
TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itaondoka kesho kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kufunzu kombe la dunia huku ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri.

Katika mechi ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa nyumbani wa Taifa wa Dar es Salaam, Tanzanite ilichapwa mabao 4-1, hivyo inahitaji kushinda katika mchezo huo kuanzia mabao 5 ili iweze kusonga mbele. 

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Boniface Wambura alisema jana kuwa timu hiyo wakiongoza na kiongozi mmoja wa msafara wataondoka kuanzia saa nne na nusu kwa ndege ya Fast Jet.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo wa marudiano Kocha wa Tanzanite Rogasian Kaijage alisema wana matumaini ya kufanya vizuri kwa vile walirekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mechi ya kwanza dhidi ya timu hiyo.

“Mchezo uliopita  ulikuwa na mapungufu kidogo, lakini kwa sasa tumeshayarekebisha na tuna imani ya kufanya vizuri jambo la muhimu ni watanzania kutuombea,”alisema.
Kaijage alisema licha ya kufanya vibaya katika mechi ya kwanza wanahitaji kupewa moyo na sio kulaumiwa kwa kupoteza mchezo mmoja, kwa vile huweza kuwakatisha tamaa wachezaji.

Kwa upande wake, Nahodha wa timu hiyo Fatma Issa aliomba watanzania kuacha kuwakatisha tamaa na badala yake wawape moyo na kuwaombea ili kurudi na ushindi.
Alisema “tunaahidi kufanya vizuri kwasababu tayari Kocha amerekebisha mapungufu, jambo la muhimu nawaomba watuombee,”.

Aliwataka watanzania kutovunjika moyo kwa matokeo mabaya yaliyopita na kuongeza kuwa kutokana na marekebisho makubwa yaliyofanywa wana imani ya kufanya vizuri.

Cheki Extra Bongo wakijifua na Muumin kwa ajili ya maonyesho ya sikukuu ya X-mass, Mwaka Mpya

Muumin akiimba na waimbaji wa Extra Bongo
Kilio ooo ooo Kiliooo Kilio cha Baba yangu.....Ndivtyo wanavyoimba waimbaji Muumi, Adam Mbombole na Kabatabo

Mnaimba hivi...si mnajua mimi ndiye Kocha wa Dunia?

Ephraem Joshua mzee wa Kanyaga Twende akicharaza gitaa mazoezini

Wakionyesha umahiri wao

Mfaume Rhythm akicharaza gita la kati ya Rhythm mazoezni leo
Sebastian Lukandikja akipapasa kinanda huku akiangaliwa na mwanamuziki mwingine
Ephraem Joshua (solo) na mcharaza gitaa la Bass Hosea Mgohache wakifanya mambo mazoezini
Mkaanda Chips, Mpogoro Mashine akifanya mautundu yake huku, msaidizi wake, Sunady Mukinga (kati) akifuatilia kwa makini na mwenzake

Rais JK atuma salamu za Rambirambi kwa Rc Mwanza

Breaking News: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza (Mabina) auwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe

Taarifa zaidi, soma hapa => http://bit.ly/18O5nYu
Marehemu Mabina enzi za uhai wake
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist  Ndikilo kufuatia vifo vya watu wawili vilivyotokea tarehe 15 Desemba,2013 katika Kitongoji cha Kanyama Kata ya Kisesa Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza.
Rais ametuma salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa kufuatia vifo vya BW. Clement Mabina na Tenery Malimi vilivyotokea baada vurugu zilizosababishwa na mabishano ya ardhi.
Rais amemuomba Mkuu wa Mkoa kuwatahadharisha wananchi kutokuchukua sheria mikononi mwao na pia kuwa waangalifu na matumizi ya silaha za moto.
“Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na taarifa za vifo vya wananchi hao wawili (2) vilivyosababishwa na mgogoro wa Ardhi ambao ungeweza kupata suluhu kwa njia za amani. Ni vema wananchi kuwa na subira na kuwa waangalifu katika kutatua migogoro yao”. Rais amesema na kuongeza kuwa “ ni vema subira na busara zikawa ndio muongozo wa kutatua migogoro yetu katika jamii badala ya hasira”.
Aidha, Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa amfikishie salamu zake za dhati kwa familia na ndugu wa Marehemu Mabina pamoja na Wazazi na ndugu wa Marehemu Tenery Malimi, ambao walifariki kutokana na vurugu hizo.
          “Amewaomba familia zote mbili ziwe na subira wakati huu mgumu kwa kuondokewa na wapendwa wao na kuviacha vyombo vya dola kuchukua hatua kwa kufuata taratibu zilizopo”.  Kwa ndugu Mabina, Chama cha Mapinduzi kimepoteza mmoja wa viongozi wake mahiri na wa kutumainiwa.  Aidha, kwa marehemu Tenery taifa limepoteza mmoja wa vijana wake wanaochipukia ambae angejaaliwa kuishi angeweza kutoa mchango muhimu kwa maendeleo ya jamii na nchi yetu.
 Mabina amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu mwaka 2000 – 2005, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, mwaka 2007 – 2012.
Rais ameziombea nyoyo za marehemu wote Mungu azilaze  mahali pema peponi Amen.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Desemba,2013

Uchaguzi wa Simba kufanyika Januari


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage
MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden Rage ameibuka na kufafanua baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakielekezwa kwake hasa sakata la kusajiliwa kwa Emmanuel Okwi na mahasimu wao Yanga na kuweka bayana ili kuondoa mzozo wa fitina Msimbazi, huenda akautisha uchaguzi mkuu Januari.
Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unatakiwa kufanyika Mei mwakani, lakini kwa vile hali inaonekana tete ndani ya klabu hiyo Mwenyekiti huyo alisema amekutana na viongozi wa matawi na kuzungumza nao na kutoa pendekezo la kuitiosha uchaguzi mkuu mapema tofauti na unavyotakiwa.
"Nimekutana nao na lengo kuu ni kuzungumza hali iliyopo ndani ya klabu na kama tatizo ni mimi basi nipo tayari kuitisha uchaguzi hata Januari ili Simba iingie duru la pili ikiwa na amani na utulivu na iliyokamilika safui mpya ya uongozi kwa maana ya Mwenyekiti, Makamu na Kamati ya Utendaji mpyam," alinukuliwa Rage.
Rage alisema kuwa tofauti yake na wenzake ni msimamo wake wa kupigania haki za klabu na hasa kutaka kila kitu kifanyike klabu na kwa uwazi.
Kuhusu sakata la Okwi analotupiwa lawama kwamba alisaidia kutua kwake Jangwani, Rage alisema ni kutaka kumbebesha lawama usiomhusu kwani kwa kipindi kirefu akikuwa nje ya nchi na kama Okwi alikuwa ni muhimu Simba Kamati ya usajili ingemsajili kama ilivyofanywa kwa wachezaji wengine watatu.
Kamati hiyo ya Simba imewasajili makipa Ivo Mapunda, Yew Berko na beki wa Gor Mahia, Donald Musoti na Rage alihoji mbona hao walisajiliwa na vipi Okwi asingesajiliwa na badala ya wanachama kumtupia lawama zisizo na maana yoyote.
Wanachama wa Simba wakiongozwa na tawi la Mpira Pesa limekuwa likimshutumu Rage kuhusu suala la Rage kwamba aliwacheza shere na kuapa kwamba wangeenda nyumbani kwake mara baada ya pambano lap na Yanga na Nani Mtani Jembe siku ya jumamosi kushinikiza kujiuzulu au kuzionyesha fedha za usajili za mchezaji huyo aliyeuzwa Etoile du Sahel ya Tunisia kabla ya kurejea kwao Sc Villa Yanga ilipoenda kumnasa.
Kuhusu uchaguzi huo ujao, Rage alisema hana mpango wa kuwania nafasi yoyote katika klabu hiyo na hasa kutokana na kuchoshwa na vurugu ndani ya Simba ambazo zimemlenga yeye binafsi kila mara hasa mtu mmoja tu aliyemtaja kuwa hohehahe.
"Sintagombea uongozi wala kutetea kiti changu, ili kuachia wengine waiongoze Simba iwapo kama mimi ni tatizo," alisema Rage na kusisitiza kuwa fedha za Okwi hazijalipwa na wala hazijalipwa hivyo wanachama wa Simba watulie.

Extra Bongo, Muumini wawarejesha 'Mafahali Watatu' Tanzania

Mwinjuma Muumin 'Kocha wa Dunia' (kushoto) akiwa na waimbaji wa Ectra Bongo kwenye mazoezi ya bendi hiyo kujaindaa na maonyesho maalum ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya
BENDI ya Extra Bongo inatarajia kukumbishia 'Mafahali Watatu' wa muziki wa dansi nchini watakaposhirikiana na Mwinjuma Muumin 'Kocha wa Dunia' katika maonyesho ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Muumini ambaye alikutwa na MICHARAZO mchana wa leo akifanya mazoezi na wanamuziki wa Extra Bongo ataungana na bendi hiyo katika maonyesho hayo yatakayofanyika jijini Dar es Salaam na mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mkurugenzi wa Extra Bongo aliiambia MICHARAZO kujiunga kwa Muumini katika bendi yao kwa maonyesho hayo itawakumhusha watanzania kundi lao la 'Mafahali Watatu' lililokuwa likiundwa na yeye (Ally Choki), Banzastone na Muumini.
Choki alisema onyesho la kwanza la pamoja na Muumini litafanyika Mkesha wa Krismasi na siku ya sikukuu hiyo kwenye ukumbi wa Meeda kabla ya kufanya hivyo mkoani Shinyanga na Bukoba.
"Mkesha wa Krismasi tutakamua Meeda Club. Sinza Mori na siku ya Krismasi yenyewe tutakuwa Chikaz Pub kabla ya kabla ya kuvamia Geita kuzindua ukumbi mpya wa Omega Splended Resort Mkesha na siku ya Mwaka Mpya na Januari 2 kuelekea Kahama, Shinyanga na siku inayofuata kufanya vitu vyetu Bukoba," alisema Choki
Choki alisema katika maonyesho yote hayo watatumia kutambulisha nyimbo zao mpya tatu za 'Mgeni', 'Wanawake Wanapendeza' na 'Hafidh'.
Muumini mwenyewe alisema anajisikia furaha kujumuika pamoja na wana Extra Bongo na hasa Choki akikumbushia enzi zao za Double Extra bendi iliyotisha Tanzania.