Mwinjuma Muumin 'Kocha wa Dunia' (kushoto) akiwa na waimbaji wa Ectra Bongo kwenye mazoezi ya bendi hiyo kujaindaa na maonyesho maalum ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya |
Muumini ambaye alikutwa na MICHARAZO mchana wa leo akifanya mazoezi na wanamuziki wa Extra Bongo ataungana na bendi hiyo katika maonyesho hayo yatakayofanyika jijini Dar es Salaam na mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mkurugenzi wa Extra Bongo aliiambia MICHARAZO kujiunga kwa Muumini katika bendi yao kwa maonyesho hayo itawakumhusha watanzania kundi lao la 'Mafahali Watatu' lililokuwa likiundwa na yeye (Ally Choki), Banzastone na Muumini.
Choki alisema onyesho la kwanza la pamoja na Muumini litafanyika Mkesha wa Krismasi na siku ya sikukuu hiyo kwenye ukumbi wa Meeda kabla ya kufanya hivyo mkoani Shinyanga na Bukoba.
"Mkesha wa Krismasi tutakamua Meeda Club. Sinza Mori na siku ya Krismasi yenyewe tutakuwa Chikaz Pub kabla ya kabla ya kuvamia Geita kuzindua ukumbi mpya wa Omega Splended Resort Mkesha na siku ya Mwaka Mpya na Januari 2 kuelekea Kahama, Shinyanga na siku inayofuata kufanya vitu vyetu Bukoba," alisema Choki
Choki alisema katika maonyesho yote hayo watatumia kutambulisha nyimbo zao mpya tatu za 'Mgeni', 'Wanawake Wanapendeza' na 'Hafidh'.
Muumini mwenyewe alisema anajisikia furaha kujumuika pamoja na wana Extra Bongo na hasa Choki akikumbushia enzi zao za Double Extra bendi iliyotisha Tanzania.
No comments:
Post a Comment