Suarez na Ivanovic katika pambano lao la jana kabla ya kutiana meno |
MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool, Luis Suarez ameadhibiwa na klabu yake kwa kitendo alichokifanya katika pambano lao la Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea kwa kumng'ata Branislav Ivanovic.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay, kupitia akaunti yake ya Twitter alithibitisha kulimwa faini na klabu yake huku akimuomba radhi beki huyo wa Chelsea wakati wakichuana uwanjani katika mechi yao ya jana iliyoisha kwa kushindwa kutambiana kwa kutoka sare ya mabao 2-2.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliandika mapema leo kwenye akaunti yake hiyo ya Tweitter kwamba kwa kutoridhishwa na kitendoa lichokifanya jana, Liverpool imemtwanga faini na kuomba klabu fedha hizo zitumike kuwasaidia waliokumbwa na janga la Hillsborough. Nawaomba radhji mashabiki wa Liverpool na Ivanovic mwenyewe."
Liverpool kupitia mtandao wake umethibitisha juu ya kumtwanga faini Suarez japo haikuweka hadharani kiwango cha faini hiyo.
Suarez anajiandaa kukumbana na adhau ya muda mrefu kutoka kwa FA kwa kitendo hicho kilichoelezwa kwamba hakikubaliki. Mchezaji huyo alishwahi kufungiwa mechi 8 na FA na kutwangwa faini kubwa kwa kitendo cha kibaguzi alichomfanyia beki wa Manchester United, Patrick Evra.
Mchezaji huyo jana alikuwa mtu wa matukio kwani licha ya kufunga bao dakika za nyongeza za pambano hilo na kuisaidia Liverpool kuepuka kipigo, pia ndiye aliyesababisha penati iliyoipa Chelsea uongoi baada ya kuushika mpira langoni mwake wakati akiokoa kona.
Pia ndiye aliyesababisha bao la kwanza la Liverpool lililofungwa na Daniel Sturridge dakika za awali za kipindi cha pili kabla ya kufanya kituko cha kuung'ata mkono wa Mserbia, Ivanovic, ambaye katika pambano la jana alimbana vilivyo Suarez asilete makeke yake.
Hii siyo mara ya kwanza kwa Suarez kufanya kitendo hicho cha kuuma mtu uwanjani, kwani alishwahi kufungiwa mezi saba kwa kumuuma beda kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal wakati akiichezea Ajax mwaka 2010.
Chama cha wachezaji soka wa kulipwa (PFA) kimetangaza kutoa ofa kwa Suarez ili asaidwe kukabiliana na hasira awapo uwanjani.