STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 22, 2013

Golden Bush Fc yawazima Veterani x2


vijana wa Golden Bush Fc waliotoa kipigo kwa Veterani

WAKALI wa soka la veterani jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani juzi ilishindwa kutamba mbele ya vijana wao Golden Bush Fc baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika pambano la kujipima nguvu kujiandaa na pambano lao dhidi ya wapinzani wao, Wahenga Fc litakalochezwa Ijumaa.
Timu ya Golden Bush vijana wanaoongoza kundi lao katika Ligi ya TFF Kinondoni iliwazima wazee wao hao licha ya kucheza nyota wa zamani wa Simba na Yanga, akiwemo Shaaban Kisiga, Athuman Machuppa, Said Swedi 'Panucci' na wengine kwa kupata mabao yake kupitia kwa Mrisho na Zola.
Wazee wa soka, Golden Veterani walipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Shaaban Kisiga.
Pamoja na kipigo hicho Mlezi wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' amesema wapo tayari kutoa pigo kwa wapinzani wao Wahenga siku uya Ijumaa katika pambano linalosubiriwa kwa hamu.
Ticotico alisema kikosi chao kipo imara na kwamba wameridhia pia ombi la wapinzani wao kumtaka Noel Katepa kuichezea Wahenga katika pambano lao la Ijumaa.
"Aidha Golden Bush wamekubali kwa Kauli moja ombi la Wahenga kutaka mchezaji wao Noel Katepa arudi kwao haraka iwezekavyo kwani tunacho kikosi kikali ambacho tumeshakiweka wazi," alisema Ticotico.
Mlesi huyo ambaye pia ni mmoja wa washambuliaji mahiri wa timu hiyo ya veterani, alikitaja kikosi kitakachoshuka dimbani Ijumaa wakati wa kuadhimisha miaka 49 ya Muungano kuwa golini atakuwepo;
Aman Simba, beki wa kulia Said Swedi, akisaidiana na Faraj, Steve na mkoba atasimama Salum Swedi 'Kussi', Godfrey Bonny atasimama dimba la kati huku winga wa kulia atakuwa yeye mwenyewe Ticotico, huku katyi ya Kisiga na Shija Katina watamiliki dimba la kati kwa mbele, na mshambuliaji wa kati atakuwa 
Herry Morris, na namba 10 atacheza Athuman Machuppa na winga wa kushoto atakuwa Sadik Muhimbo.

No comments:

Post a Comment