* Muuaji naye auawa, kumbe mgonjwa wa akili
* Alijaza damu kwenye ndoo
|
Add caption |
|
mwili wa maremu mtoto Jamali aliechinjwa na ustadhi mbagala charambe mianzini |
|
mwili wa marehem ustadhi mohamed kurangwa aliemchnja mtotoukishushjwa katika hospitali ya Temeke |
|
baadhi ya wakazi wakichungulia nyumba lililotokea tukio la mauaji ya kikatili |
USTAADH Mohamed Kurangwa (36), aliyemuua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nzasa Jamal Salum (12) kisha naye kuuawa, ametajwa kuwa alikuwa ana matatizo ya akili.
Kurangwa alimuua Jamal mwanafunzi wa darasa la tano juzi jioni nyumbani kwake Mbagala Charambe Mianzini, kwa kumchinja na kuweka kichwa cha marehemu huyu kwenye miguu ya mtoto huyo, kisha kuupeleka mwili wake choo cha nyumba anayoishi, muuaji.
Muuaji huyo alizoa damu ya Jamal na kuijaza kwenye ndoo kisha kuiweka pembeni ya nyumba yake kabla ya kuingia chumbani kwake, kujifungia na kusoma Koran.
Ustaadhi Kurangwa ambaye aliuawa na wananchi, wakati wa uhai wake alikuwa Imam wa msikiti wa Kareem ulioko Charambe.
MATATIZO YA AKILI
Mdogo wa muuaji Daudi Kurangwa alisema kati ya mwaka 1996-1997 marehemu kaka yake alishawahi kuugua ugonjwa wa akili na kutibiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Alieleza kuwa baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali alikuwa akiendelea kutumia dawa kwa kipindi lakini aliziacha baada ya kuhisi amepona.
“Kati ya Juni na Julai mwaka jana aliugua tena na kutibiwa katika hospitali ya Temeke,” alisema na kuongeza kuwa hata hivyo juzi Kurangwa hakuwa na dalili zozote za ugonjwa huo kumrudia.
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Polisi Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia tatizo la akili , alisema polisi inaendelea na uchunguzi na kueleza kuwa kuna taarifa kuwa muuaji kipindi cha nyuma aliwahi kuugua maradhi ya akili na kwamba kwa hivi karibuni alikuwa ni mzima na hajawahi kuonekana kama anaumwa.
Kamanda Shana alisema ukweli wa tukio hilo haujafahamika na kwamba Kanda Maalum ya Dar es Salaam imeunda kikosi kazi cha kuchunguza tukio hilo.
USHUHUDA WA RAFIKI
Akizungumza na NIPASHE Jumapili nyumbani kwa wazazi wa marehemu Jamal, rafiki wa mtoto huyo aliyenusurika kifo, Ramadhani Hamisi (11) anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Chemchem, alisema kabla ya kuchinjwa Ustaadhi Kurangwa alianza kumchoma visu mfululizo shingoni..
Ramadhani alisema anaishi na mjomba wake katika nyumba ya Ustadh huyo iliyoko Mianzini Njiapanda, sehemu ambapo imamu huyo alimchinja Jamal
“Siku ya tukio nilimuomba marehemu Jamal, anisindikize kwenda nyumba kuchukua kalamu, ilikuwa saa 10:30 baada ya kupata kalamu hiyo ndani ya chumba tunachoishi na mjomba tulifunga mlango na kuanza kuondoka.
“Wakati nafunga mlango marehemu Jamal alikuwa jirani yangu akiwa ameshika madaftari na kalamu,” alisema Ramadhani kwa uchungu.
Aliendelea kueleza kuwa mara Ustadh Kurangwa alitokea akiwa na baiskeli, alipowaona aliiweka pembeni na kuja karibu nao akafungua pazia la mlango wa chumba chake, lakini wakati wanataka kuondoka, ghafla alimkamata Jamal na kuanza kumchoma kisu sehemu mbalimbali shingoni.
"Nilimshuhudia akimchoma kisu mara nyingi, Jamal alilia akisema nisamehe Ustadh, nisamehe Ustadh," aliongeza mtoto huyo huku akitokwa na machozi.
Ramadhani alikimbia hadi nyumbani kwa Jamal na kumueleza mama yake kuhusu tukio hilo na yaliyoendelea nyuma hakuweza kuyashuhudia tena.
JAMAL ACHINJWA
Mjumbe wa nyumba kumi wa Mtaa wa Mianzin, Ester Msumba, aliyesema alikuwa wa kwanza kushuhudia tukio hilo, alieleza kuwa alifika eneo la mauaji baada ya kumsikia mwanamke mmoja akipiga mayowe kuomba msaada baada ya kuona kiwiliwili cha mtoto kimelala na kichwa chake kimewekwa miguuni.
Alisema mwanamke huyo alikwenda kwenye madrasa ya Ali Munawar kumpeleka mtoto wake kwa ajili ya kumuanzishia masomo ya ziada, kwa vile licha ya kufundisha dini eneo hilo alilokuwa anaishi Kurangwa linatoa mafunzo hayo ya ziada.
"Baada ya kusikia sauti ya yule mama nilikimbilia eneo la tukio, hapo nilikuta hali ni mbaya kwani niliona mwili wa mtoto umelazwa chooni na kichwa chake kiliwekwa miguuni kwake," alisema msumba.
Alisema wakati wa mauaji hayo sauti ya mtoto Jamal haikusikika hivyo ilikuwa vigumu kupata msaada.
Msumba alisema pamoja na mwili huo, alishuhudia ndoo iliyokuwa na damu iliyochanganywa na maji kitu kilichoashiria muuaji alikinga damu hiyo kuzuia isitapakae na kusambaa chini.
Sakafu ya choo hicho ilikuwa imejaa damu na familia ilizuiliwa kukitumia kwa muda kupisha uchunguzi.
Baada ya kufanya tukio hilo, Ustadh Kurangwa, alikwenda chumbani kwake na kujifungia huku akisoma Kuran.
"Baada ya kumtafuta kwa muda mtu aliyefanya unyama huo, tuligundua amejifungia ndani tulipomchungulia tulimuona akisoma Kuran huku kanzu yake ikiwa imetapakaa damu," alisema mjumbe huyo.
USTADHI KURANGWA AUAWA
Wananchi walimvamia chumbani baada ya kubomoa dirisha na kumshambulia kwa matofali na mawe hadi alipopoteza fahamu na kumvua nguo kisha kumtoa nje na kumpiga hadi alipokata roho.
WAZAZI WA JAMAL
Habiba Selemani (27) mama mzazi wa marehemu Jamal akizungumza na gazeti hili alisema anamuachia Mungu kifo cha mwanawe.
"Namuachia Mungu kwanini tukio hili afanyiwe Jamal," alisema mama mzazi, hata hivyo, alikumbukia kuwa kabla ya kifo chake alikuwa anacheza na mdogo wake mwenye miezi sita na kumvisha nguo alipomaliza aliniaga kwamba anakwenda kucheza.
"Aliniambia anakwenda kucheza lakini kwa mshangao alinieleza kuwa anaona nyota nyingi, sikujali nilimuacha aende zake," aliongeza kusema.
Kwa upande wake Salimu Ally, ambaye ni baba mzazi, alisema amepokea msiba huo mshituko mkubwa na hakuamini kilichotokea kwani ni tukio la kinyama.
Alieleza kuwa juzi jioni wakati anakaribia nyumbani aliwaona wanawake wanaingia kwenye nyumba hiyo yalikofanyika mauaji ya mwanae na kushangaa kwani walikuwa wanatoka na kulia.
Ally alisema hakujua kilichotokea na kwamba mawazo yake yalikuwa kufika nyumbani kwanza.
“Nilipofika nilimkuta mke wangu analia hajitambui ndipo mpangaji mwenzangu aliponieleza kuwa mwanangu Jamal kachinjwa niliumia sana , sikuweza kuamini,” alisema kwa huzuni.
Alikanusha kuwa marehemu mtoto wake alikuwa anasoma kwenye chuo cha Ustaadh huyo na pia hawafahamiani japo Kurangwa alimwita na kuingia naye ndani kisha kumchinja.
Mwili wake ungezikwa jana saa 10 jioni baada ya kupatiwa kibali cha polisi kuchukua maiti kutoka hospitali ya Temeke.
Chanzo:NIPASHE JUMAPILI