Simba iliyokufa Taifa mbele ya maafande wa JKT Ruvu |
Azam iliyoshindwa kurejea kileleni baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 |
JKT walioitafuna Simba uwanja wa Taifa |
Prisons walioendeleza maajabu yake katika duru la pili |
Simba inayonolewa na kocha Zdrakov Logarusic 'Loga' ilijikuta ikipoteza pointi 10 katika mechi ya nne baada ya maafande wa JKT Ruvu chini ya kocha Fred Felix Minziro kushtukiza kwa kipigo hicho leo jioni.
Mabao ya Husseni Bunu katika dakika ya 13 na Emmanuel Switta dakika ya 44 na 53 yalitosha kuinyong'onyesha Simba iliyokuwa inarejea nyumbani jijini Dar es Salaam baada ya kupata matokeo mabovu ugenini ikiambulia pointi mbili katika mechi zake tatu.
Hata hivyo vijana wa Simba walipambana na wapinzani wao waliokuwa pungufu na kufanikiwa kurejesha mabao mawili yalifungwa kwa mikwaju ya penati na Amissi Tambwe moja likiwa la penati dk 74 na 86.
Kwa kipigo hicho Simba imesalia kwenye nafasi ya nne ya msimamo ikiwa na pointi zake 32, tatu pungufu na Mbeya City ambayo nayo jana ililala mbele ya Coastal Union ya Tanga kwenye mfululizo wa ligi hiyo.
Katika mechi nyingine iliyochezwa uwanja wa Chamazi, Prisons Mbeya imeendelea kujikongoja baada ya kuibana Azam na kulazimisha sare ya mabao 2-2.
Bao la kusawazisha la Prisons lilifungwa zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mchezo huo kuisha wakati Azam wakiamini wameibuka na ushindi na pengine kurejea kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya jana kushushwa na Yanga iliyoifumua Ruvu Shooting kwa mabao 7-0.
Wageni Prisons ambao wanafikisha mechi ya tano bila kupoteza mchezo wowote ikijikusanyia jumla ya pointi 11 ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwana na Omega Seme kabla ya Aggrey Morris kuisawazisha.
Kipre Tchetche aliiongozea Azam bao la pili ilikiwa bao lake la 10 kabla ya kuja kutolewa kwa kadi nyekundu kutokana na kupewa kadi ya njano ya pili.
Laurian Mpalila aliiokoa Prisons isiadhirike baada ya kufunga bao la pili na la kusawazisha zikiwa zimeshalia dakika mbili kabla ya kumalizika kwa pambano hilo na kufanya timu hizo zigawane pointi moja moja.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014
P W D L F A GD PTS
01.Yanga 17 11 05 01 41 12 29 38
02.Azam 17 10 07 00 31 12 19 37
03.Mbeya City 19 09 08 02 24 16 08 35
04.Simba 19 08 08 03 35 19 16 32
05.Kagera Sugar 19 06 08 05 16 15 01 26
06.Coastal Union 19 05 10 04 14 09 05 25
07.Mtibwa Sugar 19 06 07 06 23 23 00 25
08.Ruvu Shooting 19 06 07 06 20 26 -06 25
09.JKT Ruvu 19 07 01 11 16 29 -13 22
10.Prisons 18 04 08 05 17 18 -01 20
11.Mgambo 19 05 05 09 12 27 -15 20
12.Oljoro 20 02 09 09 15 30 -15 15
13.Ashanti 18 03 05 10 15 30 -15 14
14.Rhino Rangers 19 02 07 10 12 23 -11 13
Wafungaji:
17- Tambwe Amisi (Simba)
10- Kipre Tchetche (Azam)
09- Elias Maguri (Ruvu Shooting) Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu (Yanga)
08-Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Mrisho Ngassa (Yanga)
07- Peter Michael (Prisons)
06- Themi Felix (Kagera Sugar), Mwegani Yeya (Mbeya City)
05- Tumba Sued (Ashanti Utd), Jerry Santo (Coastal Union)
04- Jerry Tegete (Yanga), Jonas Mkude, Betram Mombeki (Simba), Bakar Kondo, Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerome Lambele (Ruvu Shooting), Abdallah Juma (Mtibwa Sugar)
03- Haruna Chanongo, Ramadhani Singano (Simba), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu) Humphrey Mieno, Mcha Khamis (Azam), Amir Omary (Oljoro), Jeremia John (Mbeya City), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Simon Msuva (Yanga), Emmanuel Switta(JKT Ruvu), Laurian Mpalila (Prisons)
No comments:
Post a Comment