MECHI namba 118 ya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe Februari 26
mwaka huu itapangiwa tarehe nyingine.
Uamuzi wa kuiondoa mechi hiyo
iliyokuwa ichezwe Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umefanywa ili
kuipa fursa zaidi Yanga kujiandaa kwa mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi Al Ahly ya Misri itakayofanyika Jumamosi (Machi 1 mwaka huu).
No comments:
Post a Comment