Miss Tabata 2013, Dorice Mollel akitabasamu baada ya kuvikwa taji la shindano la Redd's Miss Ilala 2013 |
Miss Tabata 2013, Dorice Mollel (kati) akiwa na warembo wenzake waliongia Tatu Bora baada ya kushinda taji la Redd's Miss Ilala 2013 usiku wa jana. |
Mshindi wa Redd's Miss Ilala akiwa na tabasamu pana baada ya kutwaa taji hilo |
MISS
Tabata 2013, Dorice Mollel (22) usiku wa kuamkia leo aliwashinda
warembo wengine 13 na kunyakua taji la Redds Miss Ilala 2013 katika shindano iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam.
Dorice alimrithi
Noela Michael ambaye alishinda taji hilo mwaka jana pia akitokea kitongoji hicho cha Tabata.
Dorice
alizawadiwa 1.5milioni/-, na mshindi wa pili Alice Isaac (Dar City Centre)
alipata 1milioni /-.
Mshindi wa
tatu katika shindamo hilo ni Clara Bayo (Dar City Centre) ambaye alizawadiwa 700,000/-. Mshindi wanne Pendo
Lema (Tabata) alizawadiwa 400,000/- na watano
Shamim Mohamed alipata 300,000/-.
Mrembo
Juanita Kabunga kutoka Tabata alizawadiwa 500,000/- baada ya kushinda Miss
Talent na Kabula Kibogoti pia kutoka Tabata alishinda taji la Miss Rio and Spa
na kuzawadiwa 200,000/- na ajira ya kudumu kwenye kampuni hiyo.
Warembo
waliosalia kila moja alipata kifuta jasho cha 200,000/-.
Warembo hao
ni Clara Paul, Anna Johnson, Irene Mwelolo, Rehema Mpanda, Martha Gewe, Diana Joachim, Natasha
Mohamed, Kazumbe Mussa, Kabula Kibogoti
na Juanita Kabunga.