Kikosi cha Azam kilipopelekea Kombe lao la Kagame Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete |
Azam chini ya kocha Stewart Hall imejichimbia humo ikiwa na kikosi chake chote isipokuwa Allan Wanga aliyepo Kenya alipoenda kwa matatizo, huku Mganda Brian Majwega akiwa ametemwa rasmi kikosini.
Mabingwa hao wanajaribu kusaka ushindi kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Ngao ya Hisani kwani tangu mwaka 2012 haijawahi kushinda mbele ya Simba na Yanga waliowatungua mara mbili mfululizo ikiwamo mwaka 2013 walipowafunga bao 1-0 na mwaka jana kuwafumua mabao 3-0.
Azam inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam Jumanne baada ya kuwepo kwa taarifa ya ziara ya TP Mazembe kufutwa rasmi, na kabla ya kutimka visiwani inaelezwa kuwa huenda ikaiita URA ambayo leo inashuka Uwanja wa Taifa kucheza na Simba katika pambano la kirafiki la kimataifa, ili angalau kuwapa makali ya kuikabili Yanga ambayo ina hasira ya kung'olewa kwenye Kombe la Kagame kwa matuta.