Wachezaji wa Bilbao wakishangilia mabao yao dhidi ya Barcelona |
Suarez akijitahidi kuipiugania Barcelona, lakini wapi walilala 4-0 |
Messi hakufurukuta kabisa |
SIKU chache baada ya kufanikiwa kushinda UEFA Super Cup kwa mbinde kwa kushinda mabao 5-4 dhidi ya Sevilla, mabingwa wa Hispania, Barcelona imetoa ishara mbaya ya kwamba msimu huu huenda ikawa urojo baada ya usiku wa jana kupigwa 4-0.
Barca wamekumbana na kipigo hicho kwenye pambano la Super Cup la Hispania kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa La Liga na klabu ya Athletico Bilbao waliokuwa uwanja wa nyumbani.
Mabao matatu ya Aritz Aduriz na jingine la Mikel San Jose kwenye Uwnaja wa wa San Mames Barria, yalitosha kuizima Barcelona licha ya kuwa na nyota wake kadhaa akiwamo Messi na Luis Suarez.
San Jose alianza kumtungua kipa Marc-Andre ter Stegen
dakika ya 13 kabla ya Aduriz kufunga mabao mawili ya haraka haraka
dakika za 53 na 62.
Aduriz
akakamilisha hat-trick yake kwa bao la mkwaju wa penalti, baada ya beki
Dani Alves kumchezea rafu.
No comments:
Post a Comment