|
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Eng. Mercelin Magesa |
WAKALA wa Ufundi na Umeme (TEMESA) umesema hakuna ufisadi wowote ambao
umefanyika katika mchakato mzima wa ununuzi wa Kivuko cha Mv Dar es
Salaam.
Kauli hiyo Temesa imetolewa na Mtendaji Mkuu wa wakala
huo Mhandisi Marcelin Magesa ikiwa ni siku moja baada ya Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuilalamikia Serikali kwa
uamuzi wake wakununua Kivuko hicho wakati hakina tija kwa jamii.
Magesa
alisema maandalizi ya awali ya ununuzi wa Kivuko hicho yalishirikisha
wadau wote ambapo lengo lake ni kutoa huduma ya usafiri wa majini katika
ukanda wa bahari ya Hindi.
Mtendaji Mkuu huyo alisema mpango wa
ununuzi wa Kibuko hicho uliwasishwa katika Bunge la Bajeti la mwaka
2012/13 ambapo ulitengewa fedha ambapo fedha zingine zilitengwa bajti ya
2013/14 na 2014/15.
"Napenda kuweka wazi suala hili kwani juzi
habari zilizotoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari zinaonesha kuwa
kuna mapungufu lakini utaratibu ulifuatwa kwa kutangazwa zabuni ambapo
kampuni ua Ms. Johs Gram-Hanssen ya Denmark ndio ilishinda zabuni ya
ujunzi wa Kivuko hicho kwa dola za Kimarekani 4,980,000 sawa na fedha za
Tanzania sh.bilioni 7.916,955,000," alisema Magesa.
Alisema
ujenzi wa Kivuko cha Mv Dar es Salaam, ulifanyika hatua kwa hatua ambapo
kilifanyiwa ukaguzi mara nne Novemba 2013, Februari 2014, Julai 2014 na
Septemba 2014 ambapo kiliingizwa majini kufanyiwa majaribio.
Magesa
alisema kutokana na utaratibu wa ukaguzi huo ni dhahiri kuwa Kivuko
hicho ni kipya, na kauli kuwa sio kipya zinahitaji kupuuzwa.
Mtendaji Mkuu alisema lengo la Kivuko hicho ni kupunguza msongamano ambao umekuwa ukiongezeka katika jiji la Dar es Salaam.
Alisema
kwa sasa Temesa inaendelea kutoa huduma za usafiri nchini katika vituo
mbalimbali 28 ambapo tangu mwaka 2012 wamenunua vivuko vitano vipya.
Mhandisi
huyo alivitaja vivuko hivyo kuwa ni Mv Kilambo, Mv Mafanikio vinavyotoa
huduma Mtwara, Mv Malagarasi Kigoma, Mv Tegemeo Mwanza na Mv Dar es
Salaam