Kun Aguero akitupia kitu kambani jana huku Dzeko(10) akimshuhudia |
Aguero alikuwa majeruhi kwa muda mrefu tangu mwishoni mwa mwaka jana na alirejea tena akicheza mechi yake ya kwanza jana usiku na kutunga bao la nne katika dakika ya 73 na kuifanya Citry kuzidi kuwa na safu kali kama ya wembe kutokana na kasi yao ya kufunga idadi kubwa ya mabao msimu huu.
City ilianza kuhesbabu bao lake la kwanza kwenye dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza kupitia Alvaro Negredo aliyekuja kuongeza la pili dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi hicho.
Edin Dzeko aliiongezea City bao la tatu dakika ya 67 kabla ya Kun kufunga bao lake na kwenye dakika ya 79 Dzeko alipigilia msumari wa mwisho katika 'jeneza' la Blackburn na kuifanya City kusonga mbele.