BAADA ya Liverpool kumpotezea na kuamua kumsajili Mshambuliaji mtukutu kutoka AC Milan, Mario Balotelli, Mcameroon, Samuel Eto'o anajiandaa kutua kwa mahasimu wa Liverpool, Everton imethibitika.
Eto'o aliye huru baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na Chelsea, inaelezwa yupo hatua ya mwisho kutua kwa kikosi cha kocha Roberto
Martinez.
Nyota huyo wa zamani wa klabu za Real Madrid, Barcelona, Inter Milan na Chelsea, alikuwan akitajwa kuelekea Anfield baada ya Jose Mourinho kumchunia Stamford Bridge.
Mshindi huyo wa tuzo ya klabu bingwa Ulaya, Eto’o amekuwa
akihusishwa na vilabu kadhaa kiangazi hii lakini taarifa za hivi punde
zinaonekana wazi kuwa Everton maarufu kama Toffees wameshindwa mbio za
kupata huduma yake.
Eto'o 33 amehifadhi rekodi nzuri ya kufunga
zaidi ya magoli 300 na Martinez anataka mtu wa kutumainiwa nyuma ya
mshambuliaji wake Romelu Lukaku.
Arouna
Kone amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi na
bado ataendelea kukosekana ilhali Steven Naismith akiwa ndio
mshambuliaji namba mbili.
Eto’o
atalazimika kupunguza kiasi cha malipo anayotaka cha pauni £130,000 kwa
wiki endapo atakabidhiwa mkataba wa miaka miwili ambao inaonekana ni
kama Everton imefanya usajili kwa fedha fedha nyingi msimu huu wa
uhamisho.