KLABU ya Manchester
United inajiandaa kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza kwa kutaka kumsajili winga mahiri wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Angel Di Maria.
Meneja
wa Madrid Carlo Ancelotti amebainisha kuwa Di Maria, 26 tayari ameshawaaga wachezaji wenzake kuelekea katika
uhamisho wake huo.
Inakadiriwa kuwa United italazimika kuilipa Madrid
kitita cha paundi milioni 75 kama wanahitaji saini ya winga huyo.
Iwapo United itafanikiwa kutoa kitita hicho watakuwa wamevunja rekodi ya usajili
iliyowekwa na Chelsea wakati walipomsajili Fernando Torres kwa paundi
milioni 50 kutoka Liverpool mwaka 2011.
Usajili mkubwa uliowahi kuweka
rekodi na kufanywa na United ulikuwa ni wa Rio Ferdinand ambaye alitua
Old Trafford kwa paundi milioni 29.1 akitokea Leeds mwaka 2002.
Muargentina huyo alitua Madrid akitokea Benfica kwa ada ya paundi milioni 36 mwaka 2010
na kufanikiwa kushinda taji la La Liga mwaka 2012 na Ligi ya Mabingwa
Ulaya msimu uliopita.
United iliyoanza Ligi Kuu ya England kwa kuchechemea ikivuna pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali inahitaji kuimarisha kikosi ili kuepuka aibua ya msimu uliopita ilipoambulia patupu na kushika nafasi ya saba katika msimamo.
No comments:
Post a Comment