STRIKA
USILIKOSE
Monday, August 25, 2014
As Vita, TP Mazembe hakuna mbabe Esperance yaua
WAKATI Esperance ya Tunisia ikimaliza mechi zake za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa heshima kwa kuilaza Al Ahly Benghaz ya Libya kwa bao 1-0, wapinzani wa soka wa DR Congo AS Vita na TP Mazembe zenyewe zimeshindwa kutambiana baada ya kutopka suluhu mjini Kinshasa.
Pambano la Mazembe na Vita lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kutokana na upinzani wa timu hizo mbili za Kongo ambazo zote zimeshafuzu hatua ya Nusu Fainali kutoka kundi A lilishuhudia dakika 90 zikiisha milango ikiwa migumu.
Katika mechi hiyo watanzania wanaoichezea TP Mazembe Mbwana Samatta na Ulimwengu Thomas aliyeingizwa kipindi cha pili wakijitahidi kuipigania timu hiyo wakishirikiana na wenzao lakini bila mafanikio.
Kwa matokeo hayo Mazembe wamemaliza kileleni kwa tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa licha ya kuwa na pointi 11 sawa na wapinzani wao hao.
Katika mechi nyingine ya kundi B Esperance ya Tunisia ilikamilisha ratiba yake kwa kuilaza ndugu zao wa Libya Al Ahly Benghaz na kuishia kukamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7.
Katika mechi nyingine za kukamilisha ratiba kwa Kombe la Shirikisho, Sewe Sport ya Ivory Coast iliinyuka Nkana Red Devils kwa mabao 3-0, huku Al Ahly ya Misri ilibanwa nyumbani na Etoile du Sahel na kutoka suluhu licha ya kwamba imeshafuzu Nusu Fainali ikiungana na Sewe.
Mechi nyingine AC Leopards ya Congo iliifumua ASEC Memosa kwa mabao 4-1 na Real Bamako ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Coton Sport ambayo iliungana na Leopards kufusu hatua ya nusu fainali kutoka kundi B.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment